Jumamosi, 19 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Salamu kutoka kwa Amiri wa Hizb ut Tahrir, Mwanachuoni Mkubwa

Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

Kwa Wanaozuru Kurasa zake Mtandaoni kwa Mnasaba wa Idd ul-Adha Al-Mubaraka ya Mwaka 1444 H sawia na 2023 M

(Imetafsiriwa)

Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu na rehma na amani zimshukie Mtume wa Mwenyezi Mungu, na jamaa zake na maswahaba zake na waliomfuata.

Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, La Ilaha Ila Allah, Allahu Akbar, Allahu Akbar, Wa lilah Alhamd

Kwa Ummah zima wa Kiislamu kwa jumla… Umma bora ulioletwa kwa wanadamu ambao unaamrisha Ma’roof (mema) na unakataza Munkar (maovu) na unamuamini Mwenyezi Mungu Al-Aziz Al-Hakim...

Kwa wabebaji dawa haswa... Mwenyezi Mungu alete ushindi kupitia mikono yao, na Mwenyezi Mungu awanusuru kusimamisha dola ya Kiislamu, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume...

Kwa wageni watukufu wa kurasa za mtandaoni, wanaotafuta kheri ambazo zinabeba, wakifanya bidii kutafuta haki na kuwanusuru watu wake.

Kwao wote,

Assalamu Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh

Ninakupongezeni kwa mnasaba wa Idd ul-Adha iliyobarikiwa…na ninamuomba Mwenyezi Mungu Al-Qawi Al-Aziz kwamba Idd hii iwe ni ufunguo wa kheri na baraka kwa Waislamu wote.

Ndugu na dada wapendwa, nawasalimu na kuwaombeeni dua ya kheri kwenu, nikimuomba Mwenyezi Mungu Al-Qawi Al-Aziz awaondolee Waislamu wote dhiki na janga, na kwamba mwezi huu mtukufu uwe ndio mwezi mtukufu wa mwisho kuwashukia Waislamu huku kukiwa hakuna Dola inayoleta izza kwa Uislamu na watu wake, hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Muweza.

Mwenyezi Mungu azikubalie ibada zenu na akufanyeni miongoni mwa wale aliowasifu Mwenyezi Mungu (swt) katika aya hii:

[رِجَالٌ لا تُلْهِيهِمْ تِجَارَةٌ وَلا بَيْعٌ عَنْ ذِكْرِ اللَّهِ وَإِقَامِ الصَّلاةِ وَإِيتَاءِ الزَّكَاةِ يَخَافُونَ يَوْماً تَتَقَلَّبُ فِيهِ الْقُلُوبُ وَالْأَبْصَار * لِيَجْزِيَهُمُ اللَّهُ أَحْسَنَ مَا عَمِلُوا وَيَزِيدَهُمْ مِنْ فَضْلِهِ وَاللَّهُ يَرْزُقُ مَنْ يَشَاءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ]

“Watu ambao biashara wala kuuza hakuwashughulishi na kumdhukuru Mwenyezi Mungu, na kushika Sala, na kutoa Zaka. Wanaikhofu Siku ambayo nyoyo na macho yatageuka. * Ili Mwenyezi Mungu awalipe bora ya waliyo yatenda, na awazidishie katika fadhila zake. Na Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila ya hisabu.” [An-Nur: 37-38]

                                                                                           Ndugu Yenu,

10 Dhu al-Hijjah 1444 H                                                          Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah  

Sawia na 28 Juni 2023 M                                                                 Amiri wa Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu