Enyi Askari katika Majeshi ya Waislamu, “Hivyo, hamna hata mtu mmoja miongoni mwenu aliye ongoka?” [Hud:78]
- Imepeperushwa katika Hizb ut-Tahrir
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Ni karibu mwezi mmoja sasa tangu uvamizi mkubwa wa wanyakuzi wa Kiyahudi huko Gaza, pamoja na Ukingo wa Magharibi, na Lebanon. Wamewauwa watu, wazee, wanawake na watoto, na wameharibu miti na mawe katika vitendo vilivyo zidi uhalifu wote na zaidi ya aina yoyote ya uvamizi! Ilhali watawala bado wamekaa kimya, na wanapozungumza, ni kuhesabu idadi ya waliokufa shahidi, kujeruhiwa, na maeneo yaliyoharibiwa.