Ijumaa, 11 Muharram 1448 | 2026/06/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Syria

H.  1 Muharram 1448 Na: 03 / 1448 H
M.  Jumanne, 16 Juni 2026

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Matendo ya Watu wa Ash-Sham Yanathibitisha Kwamba Wao Ndio Wamiliki wa Halisi wa Nguvu na Wanapaswa Kuwa Nusra ya Kimaumbile Baada ya Utabikishaji wa Uislamu

(Imetafsiriwa)

Harakati maarufu katika majiji na miji kadhaa ya Syria, zinazojirudia kwa zaidi ya mnasaba mmoja baada ya kuanguka kwa utawala wa kihalifu uliokufa, hivi karibuni zaidi vuguvugu maarufu dhidi ya wale wanaoitwa Shabiha (majambazi), zinathibitisha ukweli kadhaa ambao haupaswi kusahaulika na watu wetu nchini Syria:

* Wanathibitisha kwamba Ummah ndio wenye kushikilia nguvu za kweli, na kwamba unapotenda kwa utambuzi na ikhlasi, matendo yake yana athari kubwa zaidi. Ni lazima tufahamu kwamba harakati hizi ni aina ya kuamrisha mema na kukataza maovu ikiwa zimeegemezwa juu ya yale yanayomridhisha Mwenyezi Mungu (swt).

* Zinafichua ukubwa wa pengo ambalo limejitokeza kati ya utawala wa mpito wa Syria jijini Damascus na msingi wa mapinduzi. Hii ni kutokana na shauku ya utawala wa mpito kutaka kuupumbaza mfumo wa kimataifa, huku Amerika ikiwa kileleni, na kutekeleza matakwa yake, ukitegemea msaada kutoka nje huku ukipuuza msingi wa kimaumbile wa nusra ya ndani, ambao umethibitisha ufanisi wake mara nyingi. Msingi huu unapaswa kuthaminiwa na kuungwa mkono, sio kutengwa na kafara zake kukataliwa.

* Pengo hili lilizidishwa na hisia za watu kwamba wahalifu wakuu wa mauaji dhidi yao wangeepuka adhabu, na wengine wangeweza kupata tena hadhi na mamlaka yao ya zamani. Watu walianza kuona haki ya mpito na "taratibu zake za utekelezaji" kama njia ya kufuja kafara zao na kuruhusu wahalifu kuepuka kuhisabiwa.

* Kufeli kusimamisha sheria ya Mwenyezi Mungu ndio chanzo kikuu cha matatizo yote, bila ya kujali uhalali unaotolewa, kama vile tofauti kati ya nadharia na vitendo, au kwamba tuko katika hali ya "udhaifu," ambayo wao wanaizingatia kuwa sababu ya kutotabikisha sheria ya Mwenyezi Mungu. Hata hivyo, hakika ya Qur'an Tukufu, kama alivyotueleza Mwenyezi Mungu (swt) ni kwamba: [وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكا]  “Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki” [Ta-Ha: 124], ambayo ndiyo sababu halisi ya hali ya kuchanganyikiwa na ugumu wa maisha tunayoishi dnai yake.

* Hakuna kitakachotuepusha na tatizo letu la sasa, wala kitakachotuletea izza na ushindi, wala kitakachotatua matatizo yetu, wala kitakachotuunganisha, isipokuwa mradi ulio wazi na uliobainishwa vizuri pekee unaotokana na itikadi yetu ya Kiislamu, unapokuwa ndio chanzo pekee cha katiba na sheria zinazotawala maisha yetu na kushughulikia matatizo yoyote yanayojitokeza kwa mujibu wa Shariah ya Mola wetu Mlezi, Aliyetukuka.

* Mradi huu si mkusanyiko wa malengo jumla au kauli mbiu za muda, bali ni masuluhisho ya kina yanayotokana na itikadi ya Kiislamu na yanayotokana na dalili za kina. Unasimamiwa na wanaume waliojitolea kwa Mwenyezi Mungu (swt), wanaofanya kazi ya kuutabikisha kivitendo katika uhalisia wa maisha, chini ya Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume. Hii ni ahadi ya Mwenyezi Mungu, ambayo bila shaka itatimia, na bishara njema ya mkweli na mwaaminifu, Mtume wetu Muhammad (saw), ambaye alitufahamisha kwamba baada ya utawala huu dhalimu tunaoishi chini yake, kutakuwa na Khilafah kwa njia ya Utume.

«ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللهُ أَنْ تَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا اللهُ إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ، ثُمَّ سَكَتَ» “Kisha kutakuwa na utawala dhalimu, na utadumu kwa muda Atakao Mwenyezi Mungu uwepo kisha atauondoa atakapo kuuondoa. Kisha kutakuwepo na Khilafah kwa njia ya Utume. Kisha (saw) akanyamaza”.

Khilafah ni mfumo wa utawala katika Uislamu; kupitia kwayo, Dini inasimamishwa na mfumo wa Kiislamu unatabikishwa kikamilifu. Ni mfumo wa maisha ambao Waislamu wa kabla yetu waliutekeleza kwa njia iliyo bora zaidi, na kuwafanya kuwa taifa bora lililoletwa kwa ajili ya wanadamu. Waliteka ardhi na walikuwa mabwana wa ulimwengu kwa karne nyingi. Hatutomridhisha Mola wetu Mlezi, kutimiza ahadi yake, na kupata bishara njema za Mtume wetu (saw) isipokuwa kwa kuutekeleza mradi huu mtukufu na kufanya kazi pamoja na wabebaji Dawah wenye ikhlasi na waliojitolea wa wito wa kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume. Tuna imani kwamba itasimamishwa hivi karibuni, Mwenyezi Mungu (swt) akipenda.

[وَعْدَ اللَّهِ لَا يُخْلِفُ اللَّهُ وَعْدَهُ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ]

“Ni ahadi ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu havunji ahadi yake. Lakini watu wengi hawajui.” [Ar-Rum: 6]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Syria

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Syria
Address & Website
Tel: +8821644446132 Skype: TahrirSyria
www.tahrir-syria.info
E-Mail: media@tahrir-syria.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu