Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Afisi Kuu ya Habari: Kitengo cha Wanawake "Risala kutoka Mji wa Drogheda – Ireland

(Mji uliopokea Msaada kutoka kwa Dola ya Uthmani wakati wa Njaa ya Viazi)

Wakati wa miaka ya 1840, wakati Ireland ilipokuwa katika baa kubwa la njaa kubwa ambalo lilichukua roho za zaidi ya watu milioni moja, watu wake walipata neema na nafasi kubwa ya ukarimu kutoka katika dola iliyo mbali kwa masafa ya maelfu ya maili: Khilafah ya Uthmani. Dola hii, ambayo inatawaliwa kwa Uislamu, ilituma meli 3 zilizosheheni misaada kuwasaidia wenye njaa nchini Ireland, kwa nia ya kibinadamu inayotokana na mafundisho ya huruma ya Uislamu yenye kutoa wito wa kuwasaidia wanaofadhaika na wahitaji. Dola ya Uthmani wakati huo ilitaka kutoa msaada zaidi kwa watu wa Ireland, lakini serikali ya Uingereza iliizuia kufanya hivyo kwa sababu Ireland ilikuwa chini ya ubwana wa Uingereza wakati huo. Ujumbe huu uliandaliwa na dada mheshimiwa Dkt. Nasreen Nawaz / Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir, ambayo anasimulia historia ya tukio hili, ambalo liliipatia Khilafah Uthmani sifa ya kiulimwengu kutokana na ukarimu wake na hisia kubwa ya shukrani kutoka kwa watu wa Ireland, ambayo bado inatambuliwa hadi leo.

Alhamisi, 26 Dhu al-Hijjah 1442 H sawia na 05 Agosti 2021 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu