Jumanne, 21 Rajab 1446 | 2025/01/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilaya Bangladesh:

Matukio ya Kuashiria Kumbukumbu ya 98 ya Kuvunjwa kwa Khilafah!

Hizb ut Tahrir / Wilaya Bangladesh imezindua msururu wa amali katika tukio la kumbukumbu ya 98 Hijria ya Kuvunjwa Dola ya Khilafah, kuwakumbusha Waislamu kumbukumbu hii uchungu ya Dola ya Kiislamu mnamo Rajab 28 Muharram 1342 H sawia na 3 Machi, 1924 M, Ummah wa Kiislamu ungali unateseka kwa kuipotea kwake; na kuwashajiisha Waislamu kufanya kazi kwa bidii pamoja na Hizb ut Tahrir na kuwataka watu wenye nguvu na uwezo kuipa nusra Hizb ut Tahrir kurudisha tena maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Ijumaa 22, Rajab 1440 H  -  29 Machi, 2019 M

Kukosekana kwa Dola ya Khilafah ndio Sababu ya Kuendelea kwa Mauaji ya Halaiki ya Waislamu kama ilivyo nchini New Zealand na Ukandamizaji wa Waislamu kote  Ulimwenguni.

Enyi Waislamu, Itisheni Nusra kwa Hizb ut Tahrir Mara Moja kutoka kwa Maafisa wa Jeshi Wenyewe Ikhlasi kwa ajili ya Kusimamisha Tena Khilafah

*Miaka 98 iliyopita, katika mwezi huu wa Rajab (28 Rajab, 1342 H),  Waislamu walipoteza ngao yao Dola ya Khilafah, na kuanzia muda huo, kwa ushirikiano wa kifedheha na watawala vibaraka wa nchi za Waislamu, Mabepari makafiri wameendeleza ukandamizaji katika nchi za Waislamu na unyanyasaji wa kinyama kwa Waislamu kote ulimwenguni. Hivi leo, hakuna usalama wala amani kwa Waislamu ndani ya ardhi zao wenyewe wala ng'ambo.

*Ni Dola ya Khilafah inayo kuja pekee ndiyo itakayo ulinda Ummah wa Kiislamu kutokana na uovu wa Mabepari Makafiri, na itaibuka kuwa ndiyo Dola imara na kiongozi usoni mwa ardhi hii kupitia kuwaunganisha Waislamu na majeshi yao. “Imamu pekee ndiye Ngao, nyuma yake mnapigana na mnajikinga kwake.” [Sahih Muslim].

Enyi Maafisa Wenye ikhlasi katika Jeshi, hadi lini mtanyamaza Kimya dhidi ya unyama huu kwa Ummah wa Kiislamu! Chukueni msimamo wenu katika upande wa Waislamu. Ipeni Nusra Hizb ut Tahrir kwa ajili ya Kusimamisha Tena Khilafah.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ

 “Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa” [Al Anfaal:24]

 

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoIjumaa, 10 Aprili 2020 16:16

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu