Jumamosi, 19 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Canada: Amali za Kukumbuka Kuvunjwa kwa Dola ya Khilafah

Ikiwa ni sehemu ya matukio ya kiulimwengu yaliyoandaliwa na Hizb ut Tahrir kukumbuka kuvunjwa kwa Khilafah (28 Rajab) ili kuuamsha Ummah wa Kiislamu na kunoa maamuzi yake.

Hizb ut Tahrir / Canada iliandaa matukio tofauti tofauti kukumbuka kuvunjwa kwa Dola ya Khilafah.

“Mtazamo juu ya Sababu za Kufeli kwa Mapinduzi ya Watu ndani ya Nchi za Kiarabu!” Na hotuba nyingine kwa kichwa “Kutoka katika Seerah tupate Mafunzo ya Kuleta Mageuzi  iliyokuwa imekita katika ugumu na uwazi wa mchakato wa mageuzi uliongozwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ndani ya Makkah and namna gani mapinduzi yanaweza kufaulu lau yatafuata njia yake.”

Mtume (saw) alikuwa katika mageuzi na yanathibitishwa naye. Maonyesho ya vitabu yalifanyika ambapo vitabu adhimu vya thaqafa ya Hizb viliwasilishwa na Hizb ut Tahrir.

Mapinduzi maarufu ndani ya ardhi za Kiarabu yamefeli kuleta mabadiliko ya ukweli. Ndani ya baadhi ya nchi, tawala fisadi zimebadilisha ngozi zao lakini dhati yao imebakia. Ndani ya nchi nyingine, tawala zimeshikilia mamlaka pasina kudhurika. Mapinduzi maarufu dhidi ya madhalimu na ufisadi zimetoa fursa za kuleta mageuzi msingi lakini Ummah umeipoteza kwa sababu haukutambua kwamba kuziondosha tawala hizi pasina kubeba mradi mpana kuhusu mustakbali wa Ummah wote utapelekea kubuni pengo ambalo litapatilizwa na nguvu za kikoloni. Kufuata mradi mpana ulio na mustakbali uliojengwa juu ya Aqeedah ya Kiislamu lazima iwe jambo la mwanzo kuliko jaribio lolote la mabadiliko lau Ummah unamatumaini yoyote ya kufaulu. Ni mradi wa Khilafah pekee ambao una msingi na mtazamo wa kutatua kwa ukamilifu changamoto ambazo Ummah unakumbana nazo.

Jumamosi, 27 Rajab Muharram 1439 H sawia na 14 Aprili 2018 M

 

- Rekodi ya Video iliyowasilishwa kipindi cha hotuba-

Rekodi ya video iliyoandaliwa na Hizb ut Tahrir / Canada iliwasilishwa kipindi cha matukio yaliyoandaliwa kukumbuka kuvunjwa kwa Dola ya Khilafah mnamo Rajab 1439 H (2018 M), kuhusiana na kufeli kwa mapinduzi maarufu ndani ya nchi za Kiarabu na sababu za kufaulu na ushindi lau zitafuatwa.

 

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 16 Februari 2020 13:12

Media

https://htmedia.htcmo.info/other/canada/2018/04/Rajab2018.mp4

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu