Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Indonesia:

Suluhisho la Matatizo ya Uyghur inahitaji amri moja chini ya Uongozi wa Khalifah:

Mwanachama wa Hizb ut Tahrir Indonesia (HTI), Ustaadh Rokhmat S Labib alisema kwamba suluhisho kwa Wauyghur ni kuwa na amri ya utawala mmoja. "Suluhisho la matatizo yote ya Waislamu wa Uyghur ni kwamba yapasa twende pamoja. Lazima kuwepo na amri moja chini ya uongozi wa Khilafah," aliongea katika Mjadala wa Wazi wa Gazeti la Umat: “Waislamu wa Uyghur wanalilia msaada, wako wapi Viongozi wa Kiislamu?” siku ya Jumatano (26/12/2018) katika Gedung Joang 45 Menteng, katikati mwa Jakarta.

Kabla ya hapo, mbele ya Ubalozi wa China, Rokhmat S Labib alisema Waislamu ni Ummah mmoja, iwapo ndugu Waislamu watadhulumiwa, watu watakasirika.

“Waislamu wameungana kwa msingi wa Imani moja na lazima wachukie pindi wanapoona mmoja wa ndugu yao anateswa na kudhalilishwa kule Uyghur”, alisema haya katika Shughuli ya Kuhamasisha Uokozi wa Uighur mbele ya Ubalozi wa China siku ya Ijumaa (21/12/2018), Jakarta.

Kwa mujibu wa Rokhmat, katika Uislamu, iwapo Waislamu wataomba msaada kwetu ni lazima tuwasaidie kwa sababu wao ni sehemu ya Waislamu.

"Yawapasa watu kufahamu kwamba Waislamu ni Ummah mmoja na Waislamu watakuwa imara iwapo tutakuwa na Khilafah”, alihitimisha.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Indonesia

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumamosi, 08 Agosti 2020 19:24

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu