Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Indonesia:

Hizb ut Tahrir Yasisitiza Ufaradhi wa Khilafah katika Mwezi wa Rajab

Rajab ni mwezi mtukufu. Ni katika mwezi huu ambapo kuna matukio makubwa kwa Waislamu. Tukio la Isra na Mi’raj la Mtume (saw), kufunguliwa kwa Baitul Maqdis Palestina na Salahuddin al-Ayyubi nako kulitokea katika mwezi huu wa Rajab. Pia katika mwezi huu, hususan tarehe 28 Rajab, 1342 H, kulitokea tukio kubwa la kuvunja moyo: Kukomeshwa kwa Nidhamu ya Khilafah kulikofanywa na Mustafa Kemal, wakala wa Uingereza, aliye laaniwa na Mwenyezi Mungu (swt). Tangu wakati huo, Ummah wa Kiislamu umepoteza taasisi muhimu ya kisiasa ya kutekeleza sharia za Kiislamu kwa ukamilifu ambayo huunganisha Ummah na huwalinda wenyewe na dini ya Kiislamu.

Kwa sababu hii, Hib ut Tahrir / Indonesia, imebeba ajenda katika mwezi wa Rajab kukumbuka Isra na Mi’raj ya Mtume Muhammad (saw), na wakati huo huo kuukumbusha Ummah wa Kiislamu juu ya ufaradhi na mahitaji ya Waislamu katika kusimamisha Khilafah.

Amali hii lilifanyika kwa wakati mmoja katika miji mbalimbali nchini Indonesia mnamo siku ya Jumapili (Machi 17, 2019), kwenye mikoa 34, kutoka Banda Aceh hadi Papua. Amali hii ilihudhuriwa na viongozi na wanazuoni ambao hupambana pamoja na Hizb ut Tahrir.

Katika amali hii, wazungumzaji walikumbushia zaidi matatizo mbalimbali ya Ummah yanayo tokana na kukosekana kwa Khilafah, wajibu wa kuiregesha tena, na hatua za kufuata katika kuipigania. Washiriki pia waliombwa kuwaombea dua Waislamu wengi waliokufa nchini New Zealand kutokana na vitendo vya kinyama vya magaidi waliowaua Waislamu ndani ya Misikiti katika siku tukufu ya Ijumaa. Ilielezwa na wazungumzaji kwamba mauwaji haya si kwamba yanatokea New Zealand pekee bali kila sehemu, kutokana na kukosekana kwa taasisi ya Khilafah inayowalinda Waislamu.

Afisi ya Habari Hizb ut Tahrir / Indonesia

Click to enlarge image 2019_03_17_INDO_KHLFH_ACTV_PICs_1.jpg

Click to open image!

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 26 Julai 2020 20:34

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu