- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Malaysia:
“Fungeni Viwanda vya Pombe” – Uwasilishaji wa Hizb ut Tahrir wa waraka ulikataliwa na Waziri wa Masuala ya Kidini lakini wengine wawili walipokea.
Ikiwa inaelekea mwishoni mwa majuma mawili ya kampeni yenye anwani “Fungeni Viwanda vya Pombe” iliyo tekelezwa na Hizb ut Tahrir / Malaysia (HTM), Chama kimekabidhi waraka kwa wizara tatu, kikiwasihi kufunga viwanda vyote vya pombe vilivyopo kote nchini Malaysia, ili iwe ni njia ya kukabili tatizo la madereva walevi pamoja na matatizo mengine yanayo husiana na pombe.
Ujumbe wa Chama ukiongozwa na Msemaji wake Ustaadh Abdul Hakim Othman uliwasili sehemu ya kwanza, yaani afisi ya Waziri katika Idara ya Waziri Mkuu (Masuala ya Kidini), lilikuwa jambo la kuudhi na kukera pale ambapo afisi ilipo kata miadi ya HTM. Kama inavyo pasa, miadi hiyo tayari ilikuwa imetangulia kufanywa. Matokeo yake, hakuna hata mwakilishi mmoja aliye tumwa na wizara kupokea waraka na badala yake ujumbe ukashauriwa kukabidhi waraka kwa afisa wa ulinzi.
Katika maoni yake wakati wa mkutano na wanahabari ambao uliitishwa mara tu baada ya kukabidhi, Msemaji wa HTM alielezea kuvunjika moyo kwake na yaliyo tokea. "Inawezekana vipi Waziri kusubutu kusema hakukuwa na miadi iliyo fanywa, wakati HTM ina maelezo yote ya mhusika ambaye HTM ilizungumza naye wakati wa kuweka miadi hiyo, na mhusika huyo alikuwepo pale afisini wakati ujumbe wa HTM ulipo wasili?”, alilaumu Abdul Hakim.
Katika waraka huo, HTM ilimtaka Waziri wa dini kupaza sauti kwa uwazi, na kwa kujiamini, kwamba uwepo wa viwanda vya pombe nchini Malaysia na uzwaji waziwazi Rijs (uchafu) hiyo katika maduka mengi kote nchini ni haram. Kwa hiyo yapasa kufungwa maramoja pasi na kulegeza msimamo wala udhuru, kwa sababu huu ndiyo msingi wa kusababisha ajali kwa madereva walevi. Hata hivyo, inasikitisha sana kwamba Waziri amebaki kimya kuhusu jambo hili, na kusubutu kukataa kupokea waraka huo.
Matokeo yake, ujumbe wa HTM ulienda katika eneo jengine, afisi ya Waziri katika Idara ya Waziri Mkuu (Masuala ya Bunge na Sheria), kukabidhi waraka kama ule, ukimsisitiza Waziri wa Sheria kutabikisha Sheria za Kiislamu katika suala hili na masuala mengine. Ujumbe wa HTM ulipokelewa kwa utulivu kabisa na mwakilishi wa Waziri huyu. Majadiliano mafupi yalifanyika baina na Msemaji wa HTM na mwakilishi wa Waziri juu ya uwajibikaji wa Waziri na suluhisho lilitolewa na HTM juu ya suala hili.
Kisha, Ujumbe wa HTM ulielekea katika sehemu ya mwisho ambayo ni Wizara ya Biashara za ndani na Maswala ya Watumiaji. Hapa tena ujumbe ulipokelewa kwa amani kabisa, na mwakilishi wa Waziri ambaye alipokea waraka, aliahidi kuukabidhi kwa Waziri yeye mwenyewe. Kukafanyika majadiliano mafupi baina ya wawili hawa, na Abdul Hakim akasisitiza kwa mwakilishi sababu msingi wa uwepo wa madereva walevi kihakika inatokana na Wizara hii, kwamba ndiyo yenye mamlaka kamili ya kutoa na kufuta leseni kwa viwanda na maduka yote ya pombe nchini Malaysia.
“Hata ingawa tunafahamu kwamba serikali haitafunga viwanda vyote hivyo vya pombe kwa kuwa serikali hii haikuasisiwa na kuhukumu kwa Uislamu, ni wajibu wetu kuwahesabu kwa ukiukaji wao wa Sheria hii Tukufu, na sambamba na hilo, sisi, Hizb ut Tahrir tunafanya kazi kusimamisha tena Khilafah ili kutabikisha Sheria hii Tukufu kwa ukamilifu”, alisema Abdul Hakim katika taarifa yake.
18/6/2020
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Malaysia
https://www.hizbuttahrir.today/sw/index.php/dawah/malaysia/903.html#sigProId263115f473