- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir/ Wilayah Pakistan: Silsila, “Kauli za Wanazuoni kuhusu Khilafah”
Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir inafuraha kuwasilisha kwa wafuasi wake na wageni wa kurasa za Afisi Kuu ya Habari silsila ya video yenye kichwa, “Kauli za Wanazuoni kuhusu Khilafah” iliyotolewa na Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir/Wilayah Pakistan.
Tafadhali Tegea...
#Ulema4Khilafah
[Kipindi 1]
Imam Ahmad, aliyefariki mwaka 241 H, katika “Musnad,” yake amesema kwamba, “Mtume (saw) amesema,
«إِذَا خَرَجَ ثَلاَثَةٌ فِي سَفَرٍ فَلْيُؤَمِّرُوا أَحَدَهُمْ»
‘Wanapotoka watu watatu katika safari, basi wachague mmoja wao kuwa Amir.’” Ibn Tamiyyah alieleza, “Hivyo basi, Mtume (saw) alitoa amri ya kuwekwa amiri juu ya kundi linalofanya safari, ambalo ni la lazima kwa aina zote za makundi. Hii ni kwa sababu Mwenyezi Mungu (swt) ameamrisha kuamrisha mema na kukataza yale ambayo ni munkar. Hili linaweza tu kufanywa kwa nguvu na utawala... Kuhusiana na hili ilisimuliwa, ‘Mtawala ni kivuli cha Mwenyezi Mungu (swt) katika ardhi.’”
Jumapili, 27 Safar 1446 H - 01 Septemba 2024 M
[Kipindi 2]
Katika “Sunan” yake, ad-Darimi, ambaye alifariki mwaka 255 H, alisimulia kutoka kwa Umar (ra) ambaye alisema, “Hakuna Uislamu, bila ya jamaa. Hakuna jamaa, bila ya Imarah. Hakuna Imarah, bila ya utiifu. Yeyote anayefanywa kuwa mtawala na watu wake, kwa mujibu wa Fiqh (ufahamu wa kisheria wa Dini), kuna uhai kwa ajili yake na kwao. Yeyote anayetawalishwa na watu wake, kwa mujibu wa isiyokuwa Fiqh, ni maangamivu kwake na kwao.”
Jumatatu, 28 Safar 1446 H - 02 Septemba 2024 M
[Kipindi 3]
Imam Mawardi, aliyefariki mwaka 450 H, alisema katika kitabu chake “al-Ahkam as- Sultaniyyah,” kwamba, “Imamah inaasisiwa ili kuchukua urithi baada ya Utume, katika kulinda Dini na siasa za dunia.
Hufungwa juu ya yule mwenye kutekeleza wajibu ndani ya Ummah. Ni faradhi kwa Makubaliano ya pamoja (Ijma’a).”
Jumanne, 29 Safar 1446 H - 03 Septemba 2024 M
[Kipindi 4]
Imam Al-Khateeb al-Baghdadi, aliyefariki mwaka 463 H, alisema, katika “Tarikh Baghdad,” kwamba, “Muhajirina na Answari walikubaliana kwa kauli moja juu ya Khilafah ya Abu Bakr (ra).
Wakamwambia, ‘Ewe Khalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw).’ Hakukuwa na mtu wa ziada aliyetajwa pamoja naye. Inasemekana kwamba yeye (ra) alimrithi Mtume (saw) kwa mamlaka ya Waislamu thelathini elfu. Kila mmoja wao akamwambia Abu Bakr, ‘Ewe Khalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw).’ Walitosheka naye na wale waliokuwa baada yake, Mwenyezi Mungu (swt) awe radhi nao.”
Jumatano, 01 Rabi Al-Awwal 1446 H - 04 Septemba 2024 M
[Kipindi 5]
Mwanachuoni wa fiqh Abu Al-Fath ash-Shahrastaani, aliyefariki mwaka wa 548 H, amesema katika kitabu chake “Nihayat al-Aqdaam,” kwamba, “Na haikutokea kwa Abu Bakr (ra), wala kwa mtu mwengine yeyote, kwamba inajuzu kusiwepo na Imamu (Khalifa) ardhini.
Kwa hiyo yote haya ni ushahidi kwamba Maswahaba (ra), ambao ndio waliotangulia, wote walikuwa wanakubaliana kwamba lazima kuwe na Imam. Hivyo, hiyo ni Ijma’a (Makubaliano ya Pamoja). Ni ushahidi wa kukatikiwa wa faradhi ya Imamah (Khilafah).”
Alhamisi, 02 Rabi Al-Awwal 1446 H - 05 Septemba 2024 M
[Kipindi 6]
Imam an-Nawawi, aliyefariki mwaka 676 H, alisema katika kitabu chake “Al-Manhaj Sharh Sahih Muslim,” kwamba, “Ilithibitishwa kwa Makubaliano ya Pamoja (Ijma’a) kwamba Waislamu lazima wamchague Khalifa. Ufaradhi wake unatokana na Shariah, na sio fikra za kibinadamu.”
Ijumaa, 03 Rabi Al-Awwal 1446 H - 06 Septemba 2024 M
[Kipindi 7]
Ibn Taymiyyah (rh), ambaye alifariki mwaka 728 H, alisema katika kitabu chake, “Majmuu’ al-Fatawa,” kwamba, “Ni faradhi kujua kwamba usimamizi wa watu ni miongoni mwa faradhi kuu za Dini.
Zaidi ya hayo, hakuna Dini wala maisha ya dunia bila hayo. Wana wa Adam (as) hawawezi kufikia maslahi yao, isipokuwa kwa kukusanyika. Hii ni kutokana na mahitaji ya pamoja baina yao. Ni jambo lisiloepukika kwamba wanahitaji mamlaka, wanapokusanywa kwa pamoja.”
Jumamosi, 04 Rabi Al-Awwal 1446 H - 07 Septemba 2024 M
[Kipindi 8]
Ibn Khaldun, ambaye alifariki mwaka 808 H, alisema katika “Al Muqaddimah,” kwamba, “Kumteua Imam (Khalifa) ni faradhi.
Ni faradhi katika Shariah, inajulikana kwa Ijma’a (Makubaliano ya Pamoja) ya Maswahaba (ra) na Taba’iyn. Maswahaba (ra) wa kipenzi chetu Mtume (saw), waliharakisha kumpa Bay’ah Abu Bakr (ra), baada ya kifo chake (saw). Walimkabidhi jukumu la Khilafah kusimamia mambo yao. Ndivyo ilivyokuwa, katika kila zama. Watu hawakuachwa katika machafuko, katika zama zozote. Ilitatuliwa kwa makubaliano ya pamoja, kutokana na dalili ya ufaradhi wa kumteua Imam (Khalifa).”
Jumapili, 05 Rabi Al-Awwal 1446 H - 08 Septemba 2024 M
[Kipindi 9]
Allama Zain al-Din al-Ansari, aliyefariki mwaka wa 926 H, alisema katika kitabu chake, “Ghayat ul-Wasul,” kwamba, “Ni wajibu kwa watu kumteua Imam (Khalifa) ambaye anatimiza maslahi yao, kama vile kulinda mipaka, kuandaa majeshi na kuwatiisha maadui na wezi. Ni Ijma’a (Makubaliano ya Pamoja) ya Maswahaba (ra), baada ya kifo cha Mtume (saw), kumteua Imam (Khalifa). Waliliona hili kuwa faradhi muhimu zaidi. Walilitanguliza juu ya mazishi ya Mtume (saw). Watu katika kila zama walitenda ipasavyo.”
Jumatatu, 06 Rabi Al-Awwal 1446 H - 09 Septemba 2024 M
[Kipindi 10]
Ibn Hajar al-Haytami, aliyefariki mwaka wa 974 H, alisema katika kitabu chake, “Al-Sawa’iq Al-Muhriqah,” kwamba, “Jueni pia kwamba Maswahaba (ra) walikuwa na Ijma’a (Makubaliano ya Pamoja) kwamba kumteua
Imam (Khalifa), baada ya mwisho wa zama za Utume, ni faradhi. Zaidi ya hayo, waliifanya kuwa faradhi muhimu zaidi ya zote. Walijishughulisha na faradhi hii juu ya kumzika Mtume (saw).
Jumanne, 07 Rabi Al-Awwal 1446 H - 10 Septemba 2024 M
[Kipindi 11]
Ibn Hazm, aliyefariki mwaka wa 458 H, alisema katika “al-Fasl fil-Milal wal-Ahwa’ wan-Nihal,” kwamba, “Ahl Sunnah wote, Mashia wote, Murji’ah wote na Khawarij wote, wameafikiana juu ya faradhi ya Imaamah (Khilafah). Ni faradhi kwa Ummah kumteua Imamu muadilifu, anayesimamisha hukmu za Mwenyezi Mungu ﷻ miongoni mwao, na anayesimamia mambo yao ya kisiasa kwa hukmu za Shariah alizozileta Mtume (saw).”
Jumatano, 08 Rabi Al-Awwal 1446 H - 11 Septemba 2024 M
[Kipindi 12]
Imam Al-Qurtubi, aliyefariki mwaka 671 H, alisema katika Tafsiri yake kwamba, “Ayah 30 ndani ya Sura Al-Baqarah” ni msingi wa kumteua Imamu na Khalifa, anayesikilizwa na kutiiwa. Mambo yanaunganishwa kupitia kwake. Ahkam (sheria) za Khalifa zinatekelezwa kupitia kwake. Hakuna ikhtilafu juu ya ufaradhi wa hilo, si miongoni mwa Ummah, wala miongoni mwa Maimamu Mujtahidina.”
Alhamisi, 09 Rabi Al-Awwal 1446 H - 12 Septemba 2024 M
[Kipindi 13]
Ibn Hajar Al Asqalani, aliyefariki mwaka 852 H, alisema katika “Fath al-Bari,” kwamba, “Al-Nawawi na wengineo walisema, wao (Maulamaa) walikubaliana kwa kauli moja kwamba ni lazima ateuliwe Khalifa, mmoja baada ya mwengine. Uteuzi wake lazima ufanywe na wale waliopewa mamlaka (ahl ul hal wal ‘aqd). Lazima kuwe na Khalifa mmoja tu, ambaye lazima achaguliwe kwa kushauriana. Hii ni ikiwa mashauriano haya yanafanywa kati ya idadi ndogo au isiyo na kikomo ya watu. Vile vile walikubaliana kwamba kuchaguliwa kwa Khalifa ni faradhi iliyolazimishwa na Shariah. Sio kitu kilichowekwa na akili.”
Ijumaa, 10 Rabi Al-Awwal 1446 H - 13 Septemba 2024 M
[Kipindi 14]
Abu’l Ma’ali Al-Juwayni, aliyefariki mwaka 478 H, alisema katika “Ghiyath Al-Umam”, kwamba, “Imaamah (Khilafah) ni mamlaka kuu na uongozi kamili. Inahusu mambo yote ya kibinafsi na ya umma yanayohusiana na Dini na dunia... Imeamuliwa kwamba kuteuliwa kwa Imam (Khalifa) ni faradhi. Wengi wa Maulamaa wako juu ya hili. Ufaradhi wa uteuzi unatokana na Shariah iliyopitishwa”.
Jumamosi, 11 Rabi Al-Awwal 1446 H - 14 Septemba 2024 M
[Kipindi 15]
Najm ad-Deen an-Nasafee, aliyefariki mwaka 538 H, alieleza katika “Al-Aqaid,” kwamba, “Waislamu lazima wawe na Imamu (Khalifa), ambaye atatekeleza hukmu, kusimamisha Huduud (mfumo wa adhabu), atalinda mipaka, atayahami majeshi, atakusanya Zakah, atawaadhibu waasi, wanyakuzi, na wanyang'anyi barabarani, atasimamisha swala za Ijumaa na Idd mbili, atasuluhisha migogoro baina ya waja, atakubali ushahidi wa mashahidi katika mambo ya haki za kisheria, atawaozesha vijana na maskini ambao hawana familia, na atagawanya ngawira.”
Jumapili, 12 Rabi Al-Awwal 1446 H - 15 Septemba 2024 M
[Kipindi 16]
Jamaluddin Al Ghaznawi, ambaye alifariki mwaka 593 H, alisema katika “Usuluddin,” kwamba, “Waislamu lazima wawe na Imamu (Khalifa) ambaye atashughulikia maslahi yao kupitia utabikishaji wa hukmu zao, na kusimamiisha Hudud zao (kanuni ya adhabu), kuyahami majeshi yao, na kukusanya Zaka na kuzitumia kwa wanaostahiki. Kwa hivyo, ikiwa hawana Imamu (Khalifa), itapelekea ufisadi kutawala ardhini.”
Jumatatu, 13 Rabi Al-Awwal 1446 H - 16 Septemba 2024 M
[Kipindi 17]
Adud ad-Deen al-Eejee, aliyefariki mwaka 756 H, alisema katika “Al-Mawaqif,” kwamba, “Kuteuliwa kwa Imamu ni faradhi juu yetu kinususi... ni faradhi kwetu kutokana na sababu mbili; kwanza, Makubaliano ya pamoja (Ijma’a) ya Waislamu, kupitia riwaya nyingi za tawwatur, katika kizazi cha kwanza baada ya kifo cha Mtume (saw), kwani Waislamu walikataa kuwa bila ya Imamu... pili, inazuia madhara yanayohisika. Ni faradhi kupitia Makubaliano ya Pamoja.”
Jumanne, 14 Rabi Al-Awwal 1446 AH - 17 Septemba 2024 M
[Kipindi 18]
Ash-Shawkani, aliyefariki mwaka 1250 H, alisema katika “al-Sayl al-Jarrar,” kwamba, “Maswahaba (ra) alipofariki Mtume (saw) walilitanguliza suala la Imamah na kuteuliwa kwa Imam (Khalifa) juu ya kila kitu chengine, kwa kiasi ambacho suala hili liliwashughulisha, kutokana na kumuandaa (saw) (kwa mazishi). Baadaye, Abu Bakr (ra) alipofariki, alikabidhi jukumu kwa Umar (ra). Kisha ‘Umar (ra) akalikabidhi kundi maarufu (la Sahaba (ra)). Wakati ‘Uthman (ra) alipouawa kishahidi, walitoa Bay’ah kwa Ali (ra) na baada yake kwa Hassan (ra). Waislamu waliendelea kwa njia hii, ambapo mamlaka ilikuwa moja, huku mambo ya Umma yakiwa yameshikamana.”
Jumatano, 15 Rabi Al-Awwal 1446 H - 18 Septemba 2024 M
[Kipindi 19]
Shamsuddin al-Ramli, aliyefariki mwaka 1004 H, alisema katika “Ghayatul Bayan,” kwamba, “Ni faradhi kwa watu kumteua Imamu (Khalifa), ambaye atashughulikia maslahi yao... kwa sababu ya Makubaliano ya Pamoja (Ijma’a) ya Maswahaba (ra) baada ya kifo cha Mtume (saw) juu ya kumteua Imamu. Hata waliiona kuwa ni faradhi muhimu zaidi, kiasi kwamba waliitanguliza juu ya mazishi ya Mtume (saw). Watu walikuwa juu ya hili katika kila zama.”
Alhamisi, 16 Rabi Al-Awwal 1446 H - 19 Septemba 2024 M
[Kipindi 20]
Imam Al-Juzayri, aliyefariki mwaka 1360 H, alisema katika “Fiqh ya Madhehebu Manne,” kuhusu Maimamu wanne, “Maimamu Mujtahidina, Mwenyezi Mungu (swt) awarehemu, walikubali kwamba Imamah (Khilafah) ni faradhi. Walikubaliana kwamba Waislamu lazima wamteue Imamu (Khalifa) ambaye atatekeleza ibada za Dini, na kuwapa haki waliodhulumiwa dhidi ya madhalimu. Wakaafikiana kuwa ni haramu kwa Waislamu kuwa na Maimamu wawili duniani iwe kwa kukubaliana au kutofautiana...”
Ijumaa, 17 Rabi Al-Awwal 1446 H - 20 Septemba 2024 M
[Kipindi 21]
Imam al-Ghazali, aliyefariki mwaka 505 H, alisema katika “Al-Iqtisaad fi al-i’tiqad” kwamba, “Kuonyesha kwamba kumteua Imamu ni faradhi... tunawasilisha dalili za kukatikiwa za Shari’ah kwamba ni faradhi. Hatutategemea tu Makubaliano (Ijma‘) ya Ummah. Badala yake, tunatoa angalizo kwenye msingi wa Makubaliano haya. Kwa hivyo tunasema, kupangilia mambo ya Dini kwa hakika ndio madhumuni ya Mleta Sheria ﷺ. Huu ni msingi wa uhakika, ambao hakuna mzozo unaoweza kufikiriwa. Tunaongeza juu yake msingi mwingine, ambao ni kwamba kupangilia mambo ya Dini, kunapatikana tu kupitia kwa Imamu, ambaye anatiiwa. Usahihi wa pendekezo kwamba kuteuliwa kwa Imam (Khalifa) ni faradhi unafuatia kutoka katika mambo haya mawili.”
Jumamosi, 18 Rabi Al-Awwal 1446 AH - 21 Septemba 2024 M
[Kipindi 22]
Imam al-Ghazali, aliyefariki mwaka 505 H, alisema katika “Fada’ih al-Batiniyya” kwamba, “Hebu na ifahamike kwa kizazi cha kwanza, jinsi Maswahaba (ra) walivyoharakisha baada ya kifo cha Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kumteua Imamu (Khalifa) na kufunga Bay'ah. Hebu na ifahamike jinsi walivyoamini kuwa ilikuwa ni faradhi (fard) iliyokamilika, sahihi na iliyoamrishwa, ya haraka na dharura. Hebu na ijulikane pia jinsi ambavyo hawakuakhirisha au kuchelewesha, kiasi kwamba waliacha kumtayarisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) (kwa ajili ya mazishi), kwa kujishughulisha nayo (kumteua Khalifa)... Hivyo ni yakini (qat’i) kwamba kuteuliwa kwa Imam ni jambo la lazima kwa ajili ya kuhifadhi Uislamu.”
Jumapili, 19 Rabi Al-Awwal 1446 H - 22 Septemba 2024 M
[Kipindi 23]
Imam Shafi’i, ambaye alifariki mwaka 204 H, alisema katika “Ar-Risaalah” kwamba, “Waislamu wana Makubaliano ya Pamoja kwamba kunaweza kuwa na Khalifa mmoja pekee. Mwenye kuhukumu ni mmoja (katika mzozo), Amiri ni mmoja (katika mambo) na Imamu ni mmoja (katika Dini). Kwa hiyo, wakamteua Abu Bakr (ra), kisha Abu Bakr (ra) akamteua Umar (ra), kisha Umar (ra) akawateua watu wa Shura kumchagua mmoja, hivyo Abdul Rahman (ra) akamchagua Uthman bin Affan (ra).”
Jumatatu, 20 Rabi Al-Awwal 1446 H - 23 Septemba 2024 M
[Kipindi 24]
Imaam Abu'Amr ad-Daanee, aliyefariki mwaka 444 H, alisema katika “Ar-Risalah Al-Waafiyah,” kwamba, “Kusimamishwa kwa Imam (Khalifa), mwenye nguvu na uwezo, ni Fardh (faradhi) kwa Ummah. Waislamu hawawezi kuwa wajinga, au kuzembea, juu ya faradhi hii. Kufunga mkataba wa Khalifa ni jukumu la wale waliopewa mamlaka (ahl ul hal wal ‘aqd), kutoka kwa Ummah, kama ilivyobainishwa na andiko kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Faradhi ya kusimamishwa ni moja ya faradhi ya kutoshelezana (kifayah). Kwa hivyo, ikiwa baadhi wataitimiza Faradhi hii, wengine wote wameondolewa faradhi hii.”
Jumanne, 21 Rabi Al-Awwal 1446 H - 24 Septemba 2024 M