- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Wilayah Sudan: Jukwaa la Kadhia za Umma
“Miaka 103 tangu Kuvunjwa kwa Khilafah... Maumivu na Matumaini ya Umma wa Kiislamu”
Kama sehemu ya amali za Rajab, juu ya ukumbusho wa kuvunjwa kwa Khilafah, na chini ya jkichwa “Miaka 103 tangu Kuvunjwa kwa Khilafah... Maumivu na Matumaini ya Umma wa Kiislamu,” Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan ilifanya, na ndani ya msururu wa vikao vitatu vya mwezi wa Rajab katika mji wa Gadharef. Hizb ilifanya kongamano la kwanza kati ya vikao hivyo mnamo siku ya Jumamosi, 8 Rajab 1445 H sawia na 20/01/2024 M.
Mzungumzaji wa kwanza, Ndugu Awad Muhajir, Mwanachama wa Hizb ut Tahrir, alizungumzia kuhusu historia ya Waislamu katika zama za Khilafah, ambayo misingi yake iliwekwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na maswahaba zake, jambo lililowatoa kutoka kwa udhalilifu na kugawanyika hadi kwenye izza na tamkini. Waliiongoza dunia na kueneza haki kote duniani. Kisha hali ikabadilika kwa namna ambayo haikumfurahisha muumini, kwani tukawa vipande dhaifu na nchi za kikatuni zinazoendeshwa na mkoloni kafiri Magharibi kama ipendavyo, na ikachochea vita baina ya serikali hizi dhidi ya wao kwa wao, na hata ndani ya nchi moja, ambapo Muislamu alilazimishwa kushambulia damu, heshima na mali ya ndugu yake Muislamu kwa visingizio vilivyotengenezwa na Kafiri Magharibi ili kutumikia maslahi yake, na kisha Wamagharibi wakalalamika, wakidai kuhifadhi haki za binadamu, wakitoa mfano wa vita vya Sudan, Yemen, Libya na kwengine kama mifano.
Mzungumzaji wa pili, Ustadh Maysara Yahya Muhammad Nour, Mwanachama wa Hizb ut Tahrir, alizungumzia kuhusu uwezo wa Khilafah kubadili ulisia huu mbovu kama ilivyoubadilisha nyuma, akitaja hali za dhiki na migogoro ambayo Waislamu walipitia na jinsi Khilafah ilitatua kwa mafanikio kutokana na kushikamana kwao na Uislamu na fahamu zake zinazotaka kurudishwa mambo kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na si kama watawala vibaraka wa leo wanavyoyumba kwa kukimbilia dini ya ukafiri na taasisi zake za kikoloni zilizoasisiwa kusimama dhidi ya Uislamu na watu wake.
Afisa wa jukwaa, Muhammad Abdul Qadir, Mwanachama wa Hizb ut Tahrir, alisimamia kongamano hilo kwa hali ya kipekee, akiwakaribisha waliohudhuria na kusambaza fursa na michangio. Jukwaa hilo lilishuhudia uhudhuriaji wa hali ya juu na uingiliaji kati mzuri, kwani Sheikh Ahmed Daoud, kiongozi katika kabila la Hausa, alishiriki katika uingiliaji kati, akitaka kuregea kwa usalama chini ya Uislamu, na kuwashukuru Hizb ut Tahrir kwa hafla hiyo muhimu. Jukwaa lilijaa michangio mingine, kama vile wa Sheikh Omar Shuaib na wengineo, na maswali yao, ambayo wazungumzaji waliyajibu kwa ufahamu kamili na utambuzi wa kina.
Kwa kumalizia, Ustadh Muhammad Abdel Qader amewashukuru waliohudhuria kwa kuukubali mwaliko huo na kumuomba Mwenyezi Mungu kuuweka katika mizani ya matendo yao mema na kuukirimu Ummah wetu kwa kurudi Khilafah Rashida kwa njia ya Utume ambayo Mola wetu Mtukufu ameiahidi na Mtume wake Mtukufu (saw) ametoa bishara yake.
Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan
https://www.hizbuttahrir.today/sw/index.php/dawah/sudan/3717.html#sigProIddb98b1c29f