- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:
Matembezi “Ardhi ya Palestina ni ya Kiislamu na Haina Nafasi ya Mazungumzo!”
Maandamano ya 34 mfululizo, tangu kuanza kwa Kimbunga cha Al-Aqsa, yalifanyika mbele ya Msikiti wa Al-Fatah katika mji mkuu wa Tunis, ambayo yaliitishwa na Hizb ut Tahrir/Wilayah Tunisia kwa watu wa Zaytouna na kichwa chake kilikuwa “Ardhi ya Palestina ni ya Kiislamu na Haina Nafasi ya Mazungumzo!” Kama ilivyokuwa hapo awali, yalihudhuriwa na umati mkubwa wa watu waliozunguka katika barabaraza za mji mkuu zinazoelekea barabara ya Al-Thawra, mabango yaliinuliwa na kichwa cha maandamano hayo kiliandikwa kwenye bango kuu, huku mengine yakiwa na takwimu za mashahidi na majeruhi. Wakati huo umati ulipiga takbira "Allahu Akbar" na kauli mbiu, na muhimu zaidi ilikuwa “Kwa tunakuitikia, tunakuitikia tunakuitikia ewe Rafah”... “Rafah inawalingania Wamisri kumwangusha Sisi aliyelaaniwa”... “Rafah inawalingania Waislamu, ghera iko wapi, dini iko wapi?”... “Rafah inawalingania Wamisri fauluni kwa Bustani za Pepo yenye neema”... “Rafah inawalingania watu huru, ni nani atakayevunja mzingiro huu? ” Usalama uliingilia kati mwisho wa maandamano na kuzuia kubebwa kwa bango, ambalo lilikuwa na picha iliyowajumuisha pamoja Rais wa Marekani Biden, Al-Sisi, Bin Salman, mtawala wa Qatar, na mtawala wa Imarati.
Maandamano hayo yalihitimishwa na kalima iliyotolewa na mmoja wa mashababu wa hizb mbele ya ukumbi wa manispaa ulio kwenye Barabara ya Al-Thawra, ambapo alizungumza kuwa Marekani ni adui wa kwanza wa Uislamu na Waislamu na ndio muungaji mkono mkuu wa umbile la Kiyahudi katikati ya kushindwa na usaliti wa watawala wa Kiislamu, hususan mhalifu Al-Sisi, na kwa njia hiyo akawataka watu watiifu wenye madaraka katika majeshi ya Kiislamu kuwapindua watawala hao na kusimamisha Khilafah Rashida ili Umma na dunia nzima iondolewe kutoka na uhalifu wa Mayahudi na Mkuruseda Magharibi, na ulimwengu utafurahia uadilifu mkubwa wa Uislamu.
Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Tunisia
Ijumaa, 01 Dhu al-Hijjah 1445 H sawia na 07 Juni 2024 M
- Sehemu ya Amali ya Matembezi -
https://www.hizbuttahrir.today/sw/index.php/dawah/tunisia/4025.html#sigProId78cc98fef6
- Alama Ishara za Amali -
#طوفان_الأقصى
#الجيوش_إلى_الأقصى
#الأقصى_يستصرخ_الجيوش
#AksaTufanı
#OrdularAksaya
#ArmiesToAqsa
#AqsaCallsArmies
Kwa maelezo zaidi tafadhali zuru mitandao ya Hizb ut tahrir / Wilayah Tunisia: