- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:
Matembezi ya Ukombozi: "Majeshi ya Afrika Kaskazini lazima yarejeshe jukumu lao katika kuikomboa Palestina"
Matembezi ya 44 mfululizo yalifanyika tangu kuanza kwa Vita vya Kimbunga cha Al-Aqsa, yakianzia mbele ya Msikiti wa Al-Fatah katika mji mkuu wa Tunis, hadi barabara ya Al-Thawra, ambayo yaliitishwa na Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia kwa watu wa Al-Zaytouna, na kichwa chake kilikuwa “Majeshi ya Afrika Kaskazini lazima yajiandae dori yao katika kuikomboa Palestina,” na kama yaliyotangulia, yalihudhuriwa na umati mkubwa wa watu wa Tunisia ya kijani kibichi, yalizunguka katika barabara za mji mkuu zinazoelekea Barabara ya Al-Thawra, ambapo wahudhuriaji waliimba kauli mbiu, ya muhimu zaidi ikiwa: “Enyi watawala wa aibu, Gaza iko chini ya moto,” “Enyi, majeshi ya Umma, tuondoleeni mzigo,” “Pigeni takbira, pigeni takbira kwa sauti kubwa majeshi yako hai, hayatakufa,” “Jihad, jihad na majeshi yako tayari” waliinua mabango bango kuu likiandikwa kichwa cha matembezi hayo, na jengine idadi ya mashahidi, na kwenye mabango mengine, “Enyi jeshi la Tunisia, kuweni wa kwanza kusonga kuikomboa Palestina.” Matembezi yalikamilika kwa kalima iliyotolewa na Ahmad shababu wa Hizb ut Tahrir aliyetaja ndani yake majeshi ya Afrika Kaskazini yana dori yao ya kihistoria katika mapambano juu ya Msikiti uliobarikiwa wa Al-Aqsa na na kutekeleza wajibu wao waliofaradhishiwa na Mwenyezi Mungu juu yao katika kuwanusuru ndugu zao Waislamu ambayo Mujahid Saladin al-Ayyubi, Mwenyezi Mungu amrehemu, aliishi nao kwa watu wa Afrika Kaskazini wakati wa kukomboa Al-Qudsi kutoka kwa Makruseda pia aliwahimiza juu ya ulazima wa kusimamisha dola ya Khilafah Rashida ya pili ambayo kwayo Palestina itakombolewa, na kwayo tutakomesha kunyongeshwa, kuteswa na kuuawa kwa Waislamu, na kwayo Umma wa Uislamu utaregea kuwa Umma bora kabisa uliowahi kuletwa kwa ajili ya wanadamu, uliobeba ujumbe wa Uislamu kuwa ni rehema kwa walimwengu.
Hivi ndivyo Hizb ut Tahrir ilivyo katika kila sehemu inapopatikana, isiyo ufa katika haki, thabiti juu ya misingi yake inayotokana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna za Mtume wake (saw), na haiondoki kutokana nayo hata inchi moja mpaka Mwenyezi Mungu aidhinishe kwa nusra yake.
((وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ، بِنَصْرِ اللَّهِ ۚ يَنصُرُ مَن يَشَاءُ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ)).
“Na siku hiyo Waumini watafurahia nusura ya Mwenyezi Mungu. Humsaidia amtakaye. Naye ni Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu.” [Ar-Rum: 4-5]
Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Tunisia
Ijumaa, 04 Safar Al-Khair 1446 H sawia na 09 Agosti 2024 M
- Sehemu ya Amali ya Matembezi -
https://www.hizbuttahrir.today/sw/index.php/dawah/tunisia/4152.html#sigProIdceb93c8f4b
- Alama Ishara za Amali -
#طوفان_الأقصى
#الجيوش_إلى_الأقصى
#الأقصى_يستصرخ_الجيوش
#AksaTufanı
#OrdularAksaya
#ArmiesToAqsa
#AqsaCallsArmies
Kwa maelezo zaidi tafadhali zuru mitandao ya Hizb ut tahrir / Wilayah Tunisia:
Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia
Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia