Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:

Matembezi ya Ukombozi: “Kwa Khilafah, Majeshi yatasonga kuikomboa Palestina!”

Baada ya swala ya Ijumaa, matembezi ya hamsini na tatu yalifanyika katika mji mkuu, Tunis, mbele ya Msikiti wa Al-Fatah, matembezi makubwa yaliyoitishwa na Hizb ut-Tahrir / Wilayah Tunisia, kwa watu wa Al-Khadra, na yenye kichwa “Kwa Khilafah, Majeshi yatasonga kuikomboa Palestina.” ambapo yalizunguka katika barabara za mji mkuu zinazoelekea Barabara ya Al-Thawra, yakiinua mabango makubwa 7, la kwanza lilikuwa na kichwa cha maandamano na la pili liliandikwa, “Kwa Khilafah, tutalipiza kisasi Gaza na Lebanon.” katika la tatu, liliandikwa, “Kwa Khilafah, tunaunganisha Umma,” na kwenye la nne, liliandikwa, “Kwa Khilafah, sisi tunatekeleza Hukmu za Uislamu na kuregesha haki.” Bango la tano, liliandika, “Kwa Khilafah, tunaregesha uamuzi wetu,” na la sita, “Kwa Khilafah, Umma unapata tena fahari yake,” na la mwisho “Khilafah ya Kiislamu kuelekea Mfumo mpya wa Kimataifa,” ambapo wahudhuriaji waliimba kauli mbiu nyingi, zikiwemo, “Ewe Umma bilioni moja, kwa Khilafah, unalala mwanana,” “Kwa Khilafah na majeshi, Hapana Amerika wala Viti vya Enzi,” “Kwa Khilafah, tutarudisha tena Izza ya Umma,” “Kwa Khilafah, tutaregesha tena utukufu wa Umma,” “Enyi kizazi cha Salahuddin, ni nani atakayeinusuru Palestina?”, “Enyi Watawala wa Aibu Gaza iko chini ya Moto.” Matembezi hayo yalimalizika kwa tukio la kustaajabisha na la kuogopesha mbele ya Jumba la Michezo la Manispaa kwenye Barabara ya Al-Thawra, ambapo kijana mmoja wa Kiislamu alitoa hotuba yenye kichwa “Mwaka mmoja umeopita, Ewe Umma wa Uislamu,” katika ambayo alisisitiza kwamba hatua ya kwanza kuelekea... Ukombozi wa Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina) itakuwa kwa kupindua tawala vibaraka za khiyana kupitia maafisa wanyoofu wa Kiislamu, na hii haitatokea isipokuwa kwa hatua ya nguvu zote zilizo hai na kwa habari hii, alielekeza maneno fasaha kwa wanahabari, wanazuoni, vijana wa Umma, na wenye ikhlasi miongoni mwa majeshi ya Waislamu, na akamalizia kwa kauli mbiu iliyoimbwa na hudhuri kubwa, “Khilafah, Khilafah, Khilafah.”

Matembezi haya adhimu ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia yamewatia hofu wale wanaojiita wanamambo leo, na kuibua khofu zao kwa ajili ya ustaarabu wa dola yao, na huu ndio mpango wao Kila Hizb ut Tahrir inapozungumza kuhusu badali yake ya kihadhara, “Mfumo wa Uislamu... Khilafah,” wanaingiwa na hofu na uchochezi dhidi ya Hizb, na kila mara, alhamdulillah, wanagubikwa na udhalilifu na fedheha, kwa sababu watu wamewakataa huku wakitamani uadilifu wa mfumo mtukufu wa Uislamu, na sifa nje zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Tunisia

Ijumaa, 08 Rabi’ ul-Akhir 1446 H sawia na 11 Oktoba 2024 M

Sehemu ya Amali za Matembezi

Alama Ishara za Amali

#طوفان_الأقصى

#الجيوش_إلى_الأقصى

#الأقصى_يستصرخ_الجيوش

#AksaTufanı

#OrdularAksaya

#ArmiesToAqsa

#AqsaCallsArmies

Kwa maelezo zaidi tafadhali zuru mitandao ya Hizb ut tahrir / Wilayah Tunisia:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia

Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia

Tovuti Rasmi ya Jarida la Tahrir

Ukurasa wa Facebook wa Jarida la Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu