Jumanne, 06 Muharram 1447 | 2025/07/01
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:

Matembezi ya Ukombozi: “Msafara wa Uthabiti Umesonga, Msafara wa Askari na Uanze!

Matembezi yaliyohudhuriwa na umati mkubwa wa watu yalioandaliwa na Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia yalitoka katika mji mkuu wa Tunis, baada ya swala ya Ijumaa, mnamo tarehe 20 Juni 2025 M kuanzia Msikiti wa Al-Fath chini ya kichwa: “Msafara wa Uthabiti Umesonga, Msafara wa Askari na Uanze!

Matembezi hayo yaliinua mabango, bango kuu likiwa na kichwa cha matembezi, na bango jengine likiandikwa “Enyi majeshi ya Waislamu, Umma wenu unakuombeni nusra... Mashahidi 56,800, watoto 18,000 na wanawake 12,600. Je, ni lini mtawanusuru?” Wahudhuriaji pia waliimba kauli mbiu wakati wote wa matembezi hayo wakiyataka majeshi kuvunja mipaka, kupindua viti vya utawala, kutangaza jihad huko Palestina, na kusimamisha Khilafah Rashida. Maarufu zaidi kati ya kauli mbiu hizi zilikuwa:

“Umma unataka kutangazwa jihad...Umma unataka kuangushwa viti vya utawala ... Umma unataka kufunguliwa kwa mipaka”, “Netanyahu, sikiliza, sikiliza...Khilafah yetu itaregea...Ewe Amerika, sikiliza, sikiliza...Khilafah yetu itaregea...Ewe Mzayuni, sikiliza, sikiliza...Khilafah yetu itaregea”, “Enyi majeshi ya Waislamu, jihad iko Palestina”.

 Maandamano hayo yalizunguka barabara kuu za mji mkuu unaoelekea Barabara ya Al-Thawra, ambapo amali hiyo ilihitimishwa mbele ya ukumbi wa michezo wa Manispaa kwa hotuba iliyotolewa na Ustadh Al-Sadiq Al-Turki, ambapo alielezea kwamba Gaza “Haiko tu chini ya mzingiro wa umbile la Kiyahudi, lakini pia imezingirwa na Waarabu kupitia utashi rasmi wa kisiasa, na uratibu wa kufedhehesha wa usalama na uratibu wa kimataifa, hauyumbishi na kilichotokea kwa msafara wa uthabiti ni jinai nyingine zilizoongezwa kwenye rekodi rasmi ya khiyana ya tawala za Kiarabu, zinazoongozwa na tawala za Misri na Jordan.” Vile vile amesisitiza kuwa, “Umma umepita hatua ya upole na lazima uchukue hatua ya kuwaondoa vibaraka hao na kwamba ni muhimu kuregesha upya maisha kamili ya Uislamu, kuhamasisha majeshi na kuvunja mzingiro huo.

Hivyo basi, Hizb ut Tahrir/Wilayah Tunisia inaendelea na wito wake wa wazi na wa kukaidi katika mazingira haya ambayo watu wa Gaza, Palestina, Sudan, na Waislamu wengine wanaodhulumiwa wanapitia. Inaendelea na wito wake kwa wenye ikhlasi katika majeshi ya Misri, Jordan, Uturuki, Pakistan, na majeshi mengine yenye nguvu kunusuru wito wa Uislamu na kusimamisha dola yake, ambayo itaiokoa Gaza, kuikomboa Palestina, kusimamisha utawala wa Mwenyezi Mungu duniani, na kubeba ujumbe wa mwongozo kwa walimwengu.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Tunisia

Ijumaa, 24 Dhu al-Hijjah 1446 H sawia na 20 Juni 2025 M

- Picha za Amali ya Matembezi -

 

- Alama Ishara za Amali -

#طوفان_الأقصى

#الجيوش_إلى_الأقصى

#الأقصى_يستصرخ_الجيوش

#AksaTufanı

#OrdularAksaya

#ArmiesToAqsa

#AqsaCallsArmies

Kwa maelezo zaidi tafadhali zuru mitandao ya Hizb ut tahrir / Wilayah Tunisia:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia

Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia

Tovuti Rasmi ya Jarida la Tahrir

Ukurasa wa Facebook wa Jarida la Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu