- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir/ Uingereza: Kisimamo kwa ajili ya Waislamu wa Uyghur!
Wanachama wa Hizb ut Tahrir/ Uingereza walishiriki katika kisimamo cha kuwanusuru Waislamu wa Uyghur mbele ya Ubalozi wa China jijini London, na Ubalozi mdogo wa China jijini Manchester, Jumamosi tarehe 13/11/2021. Kundi la viongozi jamii ya Waislamu waliwakumbusha kuwa Umma wa Kiislamu ni mmoja na masaibu yao ni mamoja.
Dkt. Abdul Wahid na Ustadh Mazhar Khan, wanachama wa Hizb ut Tahrir, walitoa kalima zilizoangazia:
Kwanza, kwamba Wauyghur wa Turkestan Mashariki ni Ummah mmoja na kwamba tunaumia kwa maumivu yao. Pili, tumeonyesha uwongo na madai ya Wamagharibi hususan Amerika katika kuwakomboa na kuwaondolea dhulma. Ukweli ni kwamba China inafuata nyayo zao kwa kuwakoloni na kuwakandamiza watu. Tatu, ujumbe ulitumwa hadi China kwamba Waislamu si watu wachache wala maliasili na vifaa vyao bali dhulma tunayokabiliana nayo ni kutokana na kutokuwa na kiongozi mkweli wa kisiasa na kwamba uhalisia huu hautadumu wala hautasahaulika.
Maelfu ya Waislamu walihudhuria visimamo hivyo viwili, wakipaza sauti zao kwa Takbira na kuwataka Waislamu kuungana dhidi ya dhulma.
Imetayarishwa na: Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir/ Uingereza
Jumamosi, 08 Rabi al Akhir 1443 H - 13 Novemba 2021 M
- Dondoo za Amali ya Kisimamo -
- Kalima ya Dkt. Abdul Wahid -
- Kalima ya Ustadh Mazhar Khan -
- Mahojiano pamoja na Dkt. Abdul Wahid -
#Stand4Uyghurs
#TimeForIslam
#TimeForKhilafah
#HizbBritain
Kwa Maelezo Zaidi, Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir/ Uingereza
Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Uingereza
Facebook: Hizb ut Tahrir/ Uingereza
Twitter: Hizb ut Tahrir / Uingereza
YouTube: Hizb ut Tahrir/ Uingereza
https://www.hizbuttahrir.today/sw/index.php/dawah/uingereza/2014.html#sigProId846c965b8e