- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki
Kongamano la Kiuchumi Mjini Tatvan Suluhisho la Kiislamu kwa Mgogoro wa Kiuchumi
Hizb ut-Tahrir / Wilayah Uturuki iliandaa kongamano la kiuchumi katika kituo cha kitamaduni mjini Tatvan, katika jimbo la Bitlis, lililopewa kichwa "Suluhisho la Kiislamu kwa Mgogoro wa Kiuchumi!" Sambamba na mnasaba wa kumbukumbu ya miaka 101 Hijria ya kuvunjwa Dola ya Khilafah mnamo tarehe 28 Rajab Tukufu 1342 H.
Hotuba ya ufunguzi wa kongamano iliwasilishwa na Ustadh Muhammed Amin Shiman (Msimamizi wa jarida la Kokludegisim katika jimbo la Bitlis), na kisha hotuba ikatolewa na mtaalamu wa uchumi wa Kiislamu, Ustadh Muhammed Hanafi Yaghmour, ambaye alitoa hotuba yenye kichwa "Masuluhisho ya Kiislamu ya migogoro ya kiuchumi" ambayo yalijumuisha suluhisho la Kiislamu kwa mzozo wa kiuchumi unaoikabili Uturuki, ambao unazidi kila uchao katika vipengee 10 "mfumko wa bei na gharama ya maisha, sekta ya viwanda, sera ya viwanda na nini cha kufanya, kufufua kilimo na mifugo, kutoa nafasi za kazi na kupunguza ukosefu wa ajira, dhulma katika ugavi wa mapato, uchumi usio na utozaji kodi, bili chungu na kuchochea biashara, na kulinda mali ya umma, akiba, taratibu, taasisi za kimataifa na kufutwa kwa mikataba."
Baada ya kuonyesha kanda ya video, Ustadh Abdullah Imamoglu (Imam na khatibu) alizungumza na kutoa mada kuhusu “utabikishaji wa masuluhisho ya Kiislamu.” Aligusia masuluhisho ya mfumo wa uchumi wa Kiislamu na jinsi ya kuutabikisha. Imamoglu aliwakumbusha Waislamu kwamba Uislamu, kama unavyolingania maadili mema, pia umekuja na masuluhisho ya matatizo ya kiuchumi na kwamba Uislamu ni mfumo kamili wa maisha uliotabikishwa katika kipindi cha karne 13.
Kongamano hili lilihitimishwa kwa kumuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu aharakishe kusimama kwa Dola ya Khilafah Rashida, itakayoutabikisha mfumo huu upya.
Kwa Mengi zaidi Bonyeza Hapa
Jumapili, 12 Rajab Tukufu 1443 H sawia na 13 Februari 2022 M
https://www.hizbuttahrir.today/sw/index.php/dawah/uturuki/2175.html#sigProId1988855471
Kwa Maelezo Zaidi Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki:
Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki
Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki
Ukurasa wa Twitter wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki
Akaunti ya Instagram ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki