Jumatano, 11 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/13
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Je, Amerika Itabadilisha Sera ya Petro-Dolari?

Imeandikwa na Dkt. Muhammed Jilani
Chanzo: Al-raiah.net

(Imetafsiriwa)

Kushuka kwa mahitaji ya #mafuta kufuatia ongezeko la uzalishaji mafuta nchini Saudia na Urusi na vita vya bei kati ya nchi hizo mbili, vimeangusha bei ya pipa la mafuta katika soko la Texas Magharibi kuanguka chini ya dolari moja. Hii inamaanisha kwamba wazalishaji mafuta walilazimika kulipa dolari 37 kwa kila pipa, kwa kila mnunuzi ambaye aliweza kuuza tena ama kuhamisha mafuta kutoka hifadhi ilioko Amerika.

Ilikuelewa mwelekeo huu wa mchakato wa kihistoria, ambao umetokea kwa mara ya kwanza katika historia ya biashara ya mafuta, lazima vitu vingi vitajwe. Kwanza tulitaja majibu ya utawala wa Amerika ambayo hayafiki daraja ya kushtua na majanga kama ilivyo tarajiwa katika suala hili. Rais wa Amerika Trump amesema kwamba serikali yake itanunua mapipa milioni 75 kuongezea katika hifadhi ya Amerika. Kisha akaomba bunge la Congress kuidhinisha kampuni za mafuta, kufidia hasara zao ili wasiathirike na hasara. Kisha akasisitiza kuwa janga la mafuta ni la mda.

Katika Jaribio la kuelewa hali halisi na kuangalia mbele kwa yajao, lazima tukumbuke uhusiano wa kihistoria kati ya mafuta na dolari tangu 1973. Baada ya ulimwengu kuenuka kutoka kwa Vita vya Pili vya Dunia, Amerika ilifanya kazi ya kubuni hali ya kisiasa kiulimwengu kupitia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na miungano ya kimataifa, na kiuchumi kupitia makubaliano ya Bretton woods, Taasisi ya Fedha ya Kimataifa na Benki ya Dunia, ambazo ziliunganisha dolari kwa dhahabu kwa bei maalumu yaani wakia (Ounce) moja ya dhahabu sawa na takriban dolari 35. Kisha sarafu za nchi zingine zikanasibiswa na dolari, ili hizi nchi zinunue dolari mwanzo kisha ndio waibadilisha kuwa dhahabu kama wanataka. Amerika hivyo ikadhamini hitajio la dolari kwa mataifa, na kutafuta kwao kuipata dolari ili kulipia madeni kwa kutumia hio dolari ama kupitia uuzaji wa mali na huduma dhidi ya dolari. Kisha rasmi Amerika ikapata ruhusa na leseni kupeana kiasi kikubwa cha dolari kwa kisingizio cha kukidhi mahitaji ya ulimwengu.

 Hata hivyo, baada ya takribani miaka 25, Amerika ikaona inakumbwa na utata ambao unaweza kuleta mgogoro halisi na mgogoro huu uliashiriwa na kuwepo kwa kiwango kikubwa cha dolari zilizo peanwa na Shirikisho la Hifadhi la Benki ya Amerika, kwanza kwa upendeleo, kisha kwa faida ya Amerika. Ikiwa nchi yeyote itakusanya dolari za Kimarekani, kisha iendelee kubadilisha kuwa dhahabu na hizo dolari badala ya kununua mali ama huduma, Amerika itajipata katika mazingira magumu ya kupoteza hifadhi yake ya dhahabu.

Ili kujiondoa katika mgogoro huu, Amerika ikaona iondoe makubaliano ya Bretton Woods. Nixon, mnamo Agosti 1971, akafanya uamuzi wa rais wa upande mmoja kusimamisha ubadilishaji wa dolari kwa dhahabu kulingana na makubaliano ya Bretton Wood, dhahabu ikizingatiwa kama bidhaa ya kibiashara kama bidhaa zingine.

Hata hivyo kutenganishwa kwa dolari na dhahabu kulizusha mgogoro wa kisiasa na wa kiuchumi kwa Amerika, ukaanzisha nchi za ulimwengu ambazo hazina motisha ya kupata dolari. Hivyo uwezo wa Amerika kuingiza kiasi kikubwa cha dolari kingepungua na kila dolari iliopeanwa na hifadhi ya shirikisho hainge pata njia kwenye soko la kiulimwengu ambapo badala yake, itatengeneza hali ya mfumko wa bei kiuchumi, ikiongezea gharama katika uchumi wa Amerika. Hivyo basi, sera mpya ya kifedha ya kiulimwengu ilikuwa muhimu ili kuhifadhi nafasi ya dolari kiulimwengu kama Amerika ilikuwa na ingali inachukulia umuhimu wa ulimwengu kwa dolari kama sababu yake kupeana kiasi kikubwa cha dolari ili kujihifadhia utajiri wa kiuchumi kwa biashara zake na vitendo vya kikoloni kutawala ulimwengu.

Amerika ilipata njia yake kutokana na hitajio la haraka la ulimwengu la kawi na hivyo chimbuko kubwa la kawi linawakilishwa na mafuta. Endapo Amerika itadhamini kuwa yatauzwa kwa dolari pekee, itadumisha umuhimu wa dolari ulimwenguni na kuendelea kuzalisha dolari kwa viwango vikubwa, angaa sawia na kiwango cha dolari zinazo hitajika kununua na kuuza mafuta. Na Amerika kuanzia vita vya 1973 ikachukua mkondo wa kupandisha bei ya mafuta kwanza kupitia uhusiano wake na Saudi Arabia na kisha ikaweza kukamilisha makubaliano mnamo Agosti 1973 ambayo kwayo Saudi Arabia ilikubali kuuza mafuta kwa dolari pekee na kisha nchi wanachama wa OPEC kujiunga na uuzaji wa mafuta kwa dolari pekee. Na ikawa ni wajib kwa kila taifa linalotaka kununua mafuta liwe na viwango vya kutosha vya sarafu ya dolari katika biashara za mafuta. Hii yamaanisha kuwa nchi hizi zililazimika kukubali mikopo ya dolari au kununua dolari kutoka masoko ya kifedha, au kwa njia nyengine zozote.

Kitu muhimu ni kwamba Amerika ilihakikisha muendelezo wa kupatikaniwa kwa Dolari, na Hazina ya Fedha ya Amerika ikawahakikishia muendelezo wa uzalishaji wa dolari, bila kujali kama kuna ukuwaji wa kiuchumi ndani ya Amerika ama hakuna. Ili kuwezesha mchakato wa uzalishaji wa dolari bila vikwazo, raisi wa zamani wa Amerika Reagan mnamo 1983 akaweka huru dolari kutoka kwa kikwazo chengine, ambacho kilikuwa ni ukuwaji wa kiuchumi.

Tangu 1973, hakujakuwa na taharuki, uasi, ama upinzani kwa biashara ya mafuta kwa kutumia dolari hadi hivi karibuni, ambapo mwenendo na rai zimezuka miongoni mwa baadhi ya nchi ulimwenguni, kama vile Urusi na Uchina, na mara nyengine mirengo inayo nadi kujiweka mbali na biashara ya mafuta kwa dolari. Ni kweli kwamba nyingi ya mirengo hii ni kama ujanja tu, hata hivyo hakuna shaka kwamba kuna wasiwasi na sera za Amerika, na wasiwasi huu unaendelea kuongezeka kwa athari za janga la Korona, miporomoko ya kifedha na kiuchumi inatarajiwa, haswa katika soko la mafuta, baada ya hitajio la mafuta kushuka kwa kiasi kikubwa kwa zaidi ya 30%.

Wachanganuzi wa kiuchumi na kisiasa wameongea kuhusu mpango mpya wa kiulimwengu katika hali ya kisiasa na pia kiuchumi. Wakati Kissinger alipoongea kwenye makala yake katika maandishi ya Wall Street mnamo 2/4/2020 kuhusiana na kubadilika kwa hali ya kiulimwengu ya kisiasa, wengine waliongelea kuhusiana na kubadilika kwa mfumo wa fedha kiulimwengu. Greg Rosalsky, mwandishi wa Jarida la Amerika la NPR, aliandika katika makala mnamo Aprili 21/2020, “Kwa Nini Hazina ya Fedha ya Amerika (Federal Reserve) Inatumia Mabilioni ya Dolari Kote Ulimwenguni?”, “Hazina (federal) kukubali nafasi yake kama mkopeshaji wa mwisho pekee wa kiulimwengu imewakilisha kitu kama mapinduzi katika mfumo wa fedha wa kiulimwengu.” Makala hayo yanaongea kuhusu kufungua mfumo wa laini za simu za swap na Hazina ya Fedha ya Amerika kati yake na benki kuu za kiulimwengu (Benki 14) ambapo benki hizi zitapewa viwango vikubwa vya dolari kwa ubadilishanaji wa kiwango cha sarafu na pesa za nchi zao. Hazina inafanyakazi ya kuunganisha benki kuu zingine 170, ambapo inafanyakazi ya kusambaza na kugawanya dolari trilioni 20 kote ulimwenguni.

Inaonekana kana kwamba Hazina ya Fedha ya Amerika inafanya kazi juu ya mpango mbadala kutoka kwa kile kilicho julikana kwa zaidi ya miaka 25 kama dolari za petroli, yaani, dolari dhidi ya mafuta. Katika hali ambapo bei za mafuta zitaanguka na kutulizwa katika bei ya chini ya dolari 10 kwa pipa, kiwango cha dolari ambazo Hazina hiyo inaweza kuzalisha kitapungua vibaya mno. Ni wazi kwamba kila uchao uzalishaji wa mafuta ulimwengu, huwa ni mapipa milioni 100 ya mafuta katika hali ya kawaida. Kama bei kwa kila pipa ni dolari 100, kisha Hazina ya Fedha ya Amerika ingepeana na kuchapisha dolari bilioni 10 kwa siku, sawasawa na dolari trillion 3.65 kila mwaka. Na ikiwa bei itashuka mpaka dolari 10 kwa pipa, basi baki ya Hazina kwa uuzaji wa mafuta itashuka mpaka dolari bilioni 365 peke yake. Hii inamaanisha sera za petro-dollar zitakua mzigo juu ya mfumo wa Hazina ya Fedha ya Amerika badala ya kuwa sababu ya nguvu na nishati. Matokeo yake, ni lazima kwa kazi mbadala ama kufanya kazi kurudisha bei ya mafuta kupanda kama ilivyotokea baada ya mgogoro wa kiuchumi mwaka wa 2008.

Baadhi ya wachanganuzi wamesema kwamba Hazina hiyo inafanyakazi kubadilisha jukumu la Benki na Taasisi ya Fedha ya Kimataifa katika mchakato wa ukopeshaji kiulimwengu, kiasi ya kwamba hatimaye Hazina hiyo inapeana Ulimwengu na mikopo mingi iliohusiswa na dolari. Hii inamaanisha kwamba ikiwa makubaliano yataafikiwa na benki kuu 170 za Kiulimwengu, Hazina hiyo itaweza kupeana zaidi ya dolari trilioni 10 kila mwaka, idadi ambayo ni kiasi kikubwa mno kuliko kile ilicho kuwa ikitoa kwa ubadilishanaji wa mafuta. Kwa hali yeyote ile, inaonekana kwamba Amerika inafanya kazi na msemo wa Kiyemen, “Ikiwa uko sawa, funga ndoa na upate punda, ama vyenginevyo pigia goti familia”, ambao unamaanisha kwamba kushuka kwa bei ya mafuta hadi chini ya dolari 10 na hata chini ya sufuri, kama ilivyo tokea mnamo Jumatatu 20/4/2020, kungezuia nchi kama Urusi na China hata kutokana tu na kufikiria kuachana na dolari katika biashara ya mafuta, na Amerika huenda ikadhamini muendelezo wa mtiririko wa dolari na uchapishaji na uzalishaji wake bila ya kizuizi chochote. Vinginevyo, itakuwa inajitayarisha kwa badali mbaya mtangulizi wake, kujumlisha dolari katika mkabala na madeni, mikopo ya nyumba na uwezo wa mataifa na watu, uporaji mali yao huru na watu kote duniani utawafanya watumwa na wadeni wa familia za benki za Majimbo.

Ukweli ni kuwa ulimwengu hautakuwa huru kutokamana na maovu ya Amerika, Urasilimali wake na riba, isipokuwa Uislamu urudishe fedha, uchumi na mfumo wa kisiasa chini ya uongozi wake wa haki kwa ulimwengu.

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumamosi, 16 Mei 2020 06:52

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu