Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Haja ya Mageuzi ya Kweli

Habari:

Saudi Arabia itakuwa mwenyeji wa mashindano ya kitaalam ya gofu kwa wanawake kwa mara ya kwanza mnamo Novemba katika uwanja wa Royal Greens Golf & Country Club mjini Jeddah. (Reuters 29/9/2020)

Maoni:

Katika miaka ya hivi karibuni Saudi Arabia imewafungulia watalii, matamasha, hafla za michezo na kufanya mabadiliko kwa sheria zake ambazo zimeonekana kuhitaji 'mageuzi' mengi.

Vigezo vya mageuzi ni duni na kupimwa kwa viwango vilivyowekwa na jamii ya ulimwengu. Tunaona pia jinsi shughuli zinazounda fursa za ukuaji wa kiuchumi zinaangaziwa zaidi wakati mageuzi yanaporipotiwa. Katika muundo wa Kibepari, ambapo pesa hutengezwa, mtu anapaswa kupongeza kitu chochote ambacho kitazalisha pesa, kama michezo na utalii.

Mageuzi ya kweli na ya msingi yanahitajika sana katika ulimwengu wa Kiislamu. Tunaona ufisadi, mapendeleo, ukwepaji wa sheria na tofauti kubwa kati ya matajiri na maskini. Mageuzi msingi huja wakati maadili msingi na mawazo ya jamii yanachunguzwa na kujadiliwa na sio kwa mashindano ya michezo, utalii na kurekebisha baadhi ya sheria.

Saudia ni jamii ya Kiislamu lakini hukmu na sheria zake hazilingani na imani ya watu hao. Ina nidhamu ya kifalme uliowekwa na Waingereza baada ya kugawanya ardhi zilizotawaliwa na Khilafah Uthmani (Ottoman) na kupeana ngawira kwa watawala vibaraka wao. Tangu wakati huo sisi sote tunajua utajiri wa mafuta ulitolewa na taifa hili kwa ajili ya ukuaji wa viwanda vya Magharibi. Saudia ilikuwa mwema kuyasambaza na sheria, hukmu na ada zake za ndani zinaweza kuwa za nyuma na za zamani kama vile walivyotaka. Hakuna yeyote aliyejali.

Mbele ya karne ya 21, Saudi inasonga mbele kulingana na mwelekeo wa Amerika. Mapato yanazalishwa kando na uzalishaji wa mafuta kwani akiba itaisha na pia kuna njia mbadala za kutosha mahali kwengineko. Hii ni kwa kuunda vivutio vya watalii na picha laini juu ya uvumilivu kwa wanawake na shughuli zao. Kwa hivyo, mageuzi yanategemea kutumikia ajenda fulani na hayaji kutoka kwenye fikra sahihi.

Mageuzi ya kweli kwa Saudia au ardhi yoyote ya Kiislamu yatakuja wakati msingi wa mahusiano ya jamii utasahihishwa. Watu binafsi, ambao ni Waislamu wanapaswa kuangalia imani yao wenyewe na sheria zake kutawala jamii. Uhusiano kati ya wao kwa wao na yale ambayo jamii inayaona kuwa muhimu na yanayofaa kufanywa pia yanahitaji kuja kutoka katika kiwango hicho hicho.

Waislamu zama za nyuma, waliupeleka Uislamu katika ardhi nyingi na walibeba ujumbe wenye nguvu wa dawah kwa ulimwengu wakati Uislamu ulipotumiwa kama kipimo cha mafanikio. Utabikishaji wa nidhama ya Kiislamu ya utawala, Khilafah ya Kiislamu kwa njia ya Utume, uliruhusu jamii ya Kiislamu kuwa taa inayoongoza kwa mataifa mengine kutokana na uwazi wake wa fikra na kujua dhamira yake.

Waislamu, kama Ummah, wana jukumu la kupeleka Uislamu kwa wengine, kuwasilisha ajenda ya mageuzi ya kweli kwa wengine. Kuwasilisha kusudi la maisha na jinsi ya kujitahidi katika maisha haya, kumridhisha Mwenyezi Mungu (swt) kama alama ya mafanikio ya kweli. Ummah wetu una misheni ambayo inahitaji kuongozwa sio kwa ajenda ya kikoloni ya Kimagharibi bali kwa Quran na Sunnah.

Tunayo mengi zaidi kuliko michezo na utalii ya kuonyesha kwa ulimwengu. Leo, hakuna uongozi halisi au mwongozo na mfumo wa Kirasilimali unausonga ulimwengu. Mageuzi yake yalikuja wakati ulipotabanni sheria za kisekula na hili limesababisha muozo na mateso katika jamii zake wenyewe. Kwa kuchukua mfano wake wa mageuzi, hatuwezi kupata mafanikio ya kweli na mabadiliko ya kweli tunayohitaji.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Nazia Rehman

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu