Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Serikali Dhaifu na ya Khiyana ya Hasina Inavunja Shajaa ya Jeshi la Bangladesh kwa jina la Mazoezi ya Pamoja na Dola Adui ya India.

Habari:

Bangladesh na India zimeanza mazoezi ya siku tatu ya majini katika Ghuba ya Bengal kaskazini mnamo Jumamosi, kulingana na vyanzo vya kidiplomasia na ulinzi. Maafisa wa ulinzi wa Bangladesh walielezea ushiriki huo kama doria iliyoratibiwa ya baharini kando kando ya mpaka wa kimataifa wa baharini kwa manuari za nchi hizo mbili. Ni awamu ya pili ya mazoezi ya majini kaskazini mwa Ghuba ya Bengal. Ya kwanza ya aina yake yalifanyika mnamo 2019. 'Lengo la mazoezi haya ni kukuza utangamano na ustadi wa pamoja wa kufanya kazi kupitia kufanya anuwai ya mazoezi na operesheni za baharini,' Msemaji wa Jeshi la Wanamaji la India Kamanda Vivek Madhwal alisema. (New Age, Oktoba 3, 2020)

Maoni:

Ushiriki wa jeshi la majini la Bangladesh katika mazoezi ya pamoja na Dola adui ya Kishirikina ya India ni kitendo cha uongozi usioweza kujimudu haswa wakati India haijatulia kwa sababu ya mzozo wa hivi karibuni na China juu ya ubwana katika eneo hilo. Njia ambayo nchi kadhaa za kusini mwa Asia kama Nepal zinaamiliana na India inathibitisha jinsi nchi hii ilivyo dhaifu. Lakini serikali kibaraka ya Bangladesh bila aibu inasahilisha ajenda ya Amerika (Sera ya Kuamiliana na Mashariki) kuimakinisha India kama dola ya kikanda ili kukabiliana na China. Amerika haswa ina wasiwasi juu ya ghasia za hivi karibuni za China na India kwani zinaweza kuathiri mahitaji yake ya kimkakati ya muda mrefu katika eneo hilo. Wasiwasi huo ulionyeshwa na Waziri wa Kigeni wa Amerika Mike Pompeo kama vitendo vya "fujo sana" vya China (foreignpolicy.com, Julai 9, 2020). Kwa hivyo sasa, tunaona ushiriki wa Bangladesh na India katika mazoezi ya pamoja huko Ghuba ya Bengal miezi michache tu baada ya Jeshi la Wanamaji la India kushiriki mazoezi ya kijeshi na kikundi cha vita cha Jeshi la Wanamaji la Amerika karibu na Visiwa vya Andaman na Nicobar katika Ghuba ya Bengal yaliyolenga kuzuia Mpango wa upanuzi wa China.

Serikali dhaifu ya Hasina haina hata werevu wa kutosha kupatiliza fursa ya hali hii kwani haina maono, na badala yake inapendelea utumwa kwa wakoloni wa Magharibi kama njia ya kuwa madarakani. Mazoezi kama hayo ya pamoja ya Amerika ni ala mbaya mno ya kuyaweka majeshi ya jasiri na yenye nguvu ya Waislamu chini ya utiifu wa uongozi wa wanajeshi makafiri na washirikina ili kufikia malengo yao. Zaidi ya hayo, imeharamishwa kwa majeshi ya Waislamu kuhudhuria mazoezi ya pamoja kama hayo kama vile Mwenyezi Mungu (swt) anavyosema katika Quran al Karim:

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا عَدُوِّي وَعَدُوَّكُمْ أَوْلِيَاءَ تُلْقُونَ إِلَيْهِمْ بِالْمَوَدَّةِ وَقَدْ كَفَرُوا بِمَا جَاءَكُمْ مِنَ الْحَقِّ)

“Enyi mlio amini! Msiwafanye adui zangu na adui zenu kuwa marafiki mkiwapa mapenzi, na hali wao wamekwisha ikataa haki iliyo kujieni” [Surah Al-Mumtahinah: 1].

Badala ya kuligeuza jeshi letu kuwa chombo cha Makafiri-Washirikina, Khilafah inayokuja atatoa maono na kusudi halisi la vikosi vyetu vya kijeshi vya Kiislamu. Jeshi la Khilafah litahamasishwa papo hapo kuwaachilia huru Waislamu na wasio Waislamu waliodhulumiwa nchini India, ambayo ilikombolewa na babu zetu kupitia Jihad na sasa inakaliwa kwa njia haramu na Washirikina.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya ut Tahrir na
Muhammad Shiraz
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu