Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Enzi Mpya ya Mahusiano kati ya Amerika na Uturuki na Yule Anayeitwa "Mshirika wa Kistratejia"

(Imetafsiriwa)

Habari:

Bunge la Seneti la Amerika limemuidhinisha Antony Blinken, mteule wa Rais Joe Biden wa nafasi ya Waziri wa Kigeni Katibu. Blinken ni mtu mashuhuri sana nchini Uturuki vilevile. Chini ya Barack Obama, alishiriki haswa katika mazungumzo na Syria, ISIS na Majeshi ya Kidemokrasia ya Syria (SDF), na alizuru Uturuki baada ya jaribio la mapinduzi la Julai 15. Blinken alikuwa amejitokeza mbele wiki iliyopita, baada ya kuiita Uturuki "yule anayeitwa mshirika wa kistratejia".

Kwa mujibu wa amri zilizotolewa chini ya saini ya Rais Recep Tayyip Erdogan, Feridun Hadi Sinirlioglu aliteuliwa kama Mshauri Mkuu wa Rais na kupewa jina la balozi, na aliteuliwa kama Mwakilishi Maalum wa Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Uturuki kwa Umoja wa Mataifa (UN).

Maoni:

Serikali mpya nchini Amerika, iliyoundwa baada ya uchaguzi wa Biden kama Rais, inaonekana kuathiri moja kwa moja uhusiano wa Amerika na Uturuki katika enzi mpya. Kwa sababu habari mbili tofauti hapo juu zinaunga mkono hili. Waziri mpya wa Mambo ya nje wa Amerika Antony Blinken alijibu maswali ya maseneta na akasema wazi yafuatayo juu ya Uturuki katika hotuba yake wakati wa kikao cha uteuzi mnamo Januari 19: "Wazo la yule anayeitwa - mshirika wetu kistratejia - kihakika kuwa sambamba na mmoja wa washindani wetu wakubwa wa kimkakati nchini Urusi halikubaliki." Kwa kweli, taarifa hii ya Blinken inahusu mifumo ya ulinzi wa anga ya S-400 ambayo Uturuki ilinunua kutoka Urusi, lakini ujumbe huu unamaanisha zaidi ya suala la S-400. Kwa sababu ukweli kwamba Uturuki ilinunua mifumo ya ulinzi wa anga ya S-400 kutoka Urusi, ilitokea chini ya ufahamu na idhini ya Amerika. Haitakuwa sawa kulichukulia hili kuwa ni upendeleo wa Trump kwa Uturuki, huu ni upendeleo wa Amerika. Amerika imeitumia vilivyo Urusi na Uturuki katika mchakato wa amani wa Syria. Kwa upande mwingine, haikusema chochote kwa Urusi na Uturuki juu ya uuzaji wa S-400. Sasa kwa kuwa mambo yanaendelea nchini Syria kwa niaba ya Amerika, haitahitaji tena Urusi na Uturuki kama hapo awali. Katika hali ambapo itawahitaji, itaweka mbele karata ya S-400 dhidi ya Uturuki. Itaweka shinikizo kwa Uturuki kutumia lugha ya kisiasa zaidi na kukuza msimamo wa kisiasa juu ya suala la PYD-YPG. Kwa sababu Blinken inasaidia 'mkakati mpya wa Amerika "ambapo PKK inayeyuka ndani ya YPG, kwa maana nyengine, katika njia ambayo kifurushi chake kinabadilishwa na msingi wa uhalali wa kimataifa unaimarishwa'.

Tunapozingatia sera ya usalama ya Uturuki ya miaka 2-3 katika mapambano ya silaha na PKK, mkakati wa Uturuki dhidi ya PKK na sera itakayofuata kwa ajili ya PYD-YPG itakuwa tofauti katika kipindi kijacho. Kwa sababu Uturuki ina hatua ambazo zinarejelea ukweli kwamba itaenda katika mwelekeo huu. Uteuzi wa Feridun Sinirlioglu kama Mshauri Mkuu wa Rais ni mojawapo ya ishara hizi.

Feridun Sinirlioglu ni nani? Feridun Sinirlioglu ni mtu ambaye aliwahi kuhudumu kama balozi katika nchi nyingi, alifanya kazi kama afisa kwa miaka mingi, alishauriana na taasisi kama Afisi ya Waziri Mkuu na Urais, la muhimu, ni mtu ambaye alikuwa Balozi wa Tel Aviv wa Uturuki kati ya 2002, mwaka wa kwanza Chama cha AK kilipoingia madarakani, na 2007, na muhimu zaidi, ni mtu ambaye alikuwa Katibu wa Mashauri ya Kigeni katika zama za Obama na Waziri wa Mambo ya nje kwa kipindi kifupi… Kwa maana nyengine, yeye ni mmoja wa watendaji maafisa nadra wa Amerika waliokuzwa na afisi ya kigeni ya Uturuki. Kwa uchaguzi wa Biden, Feridun Sinirlioglu ni muhimu kwa Rais Erdogan kwa sababu ya uhusiano ambao utafanya kazi kupitia taasisi badala ya uhusiano wa Amerika na Uturuki ambao utafanya kazi kati ya viongozi na watu. Kwa kuwa Rais ana mamlaka kamili katika mfumo wa urais, Erdogan atashauriana na Sinirlioglu juu ya mahusiano yake mapya na Amerika.

Kwa hivyo ni aina gani ya mabadiliko ambayo Sinirlioglu inaweza kuleta kwa sera ya kigeni ya Uturuki katika mahusiano kati ya Amerika na Uturuki? Kwa sababu Uturuki haiko huru katika sera za kigeni, hakutakuwa na mabadiliko kati ya hali ya zamani na mpya isipokuwa tofauti ya mtindo. Lakini, sera mpya za kigeni zinaonekana kuathiri hatua za Uturuki katika sera za ndani dhidi ya AKP na haswa Muungano wa Watu. Kwa sababu kuna mshabaha mwingi kati ya Waziri mpya wa Mambo ya nje wa Amerika Antony Blinken na mshauri mpya wa sera ya mambo ya nje wa Erdogan Sinirlioglu katika mahusiano ya Uturuki na 'Israel' na mtazamo wa Uturuki wa PYD-YPG.

Kwa mfano, mahusiano ya Uturuki na 'Israel' ni mojawapo ya haya ... Mtazamo juu ya PYD-YPG pia ni mojawapo ya haya… Sinirlioglu alitoa taarifa kuhusu PYD mnamo 2015, wakati alipokuwa Waziri wa Mambo ya nje. Alisema kuwa PYD ni chama kama HDP. Feridun Sinirlioglu, ambaye alizungumza na Verda Ozer kutoka Gazeti la Hurriyet katika kipindi hicho, alitoa taarifa juu ya Syria, operesheni ya kuvuka mpaka, kupigana dhidi ya ISIS na PKK. Sinirlioglu alisema, "Tunapaswa kutofautisha kati ya PYD na YPG. YPG ni sawa na PKK, ambayo iko kwenye orodha ya mashirika ya kigaidi ya Uturuki na Amerika. PYD, hata hivyo, ni chama, kama HDP nchini Uturuki. YPG ni tawi lake lenye silaha. Lakini PYD haishiki silaha mikononi mwake". Tunapoizingatia taarifa hii kutokana na mtazamo wa leo, unaweza kuiona kama taarifa ya kijasiri sana, lakini tunapoizingatia ya 2015, ilikuwa ni taarifa ambayo Erdogan na Chama cha AK waliiunga mkono na kuitabanni. Haijulikani wazi ni kwa muda gani Chama cha AK na Erdogan wanaweza kuendelea na sera yao ya uchaguzi ya 2023, ambayo wanaichukulia HDP kama shirika la kigaidi, chini ya dhurufu hizi.

Kwa kifupi, sera hiyo Uturuki inashikilia kwa njia inayoitegemea Amerika kuhusu sera ya kigeni, hadi sasa haijatoa mchango wowote kwa maslahi ya Waislamu na ndivyo itakavyokuwa. Tumeiona huko Syria, tumeiona huko Palestina, Libya na Misri. Sera hii ya kigeni, ambayo inaitegemea Amerika, inakifanya Chama cha AK na Erdogan kwenda mayobo, mazungumzo na mabadiliko tasa ya kisiasa katika siasa za ndani. Kwa amri ya kitumwa ambayo imeweka kamba yake mikononi mwa bwana wake, siasa zinaweza kufanywa tu kwa sana. Leo wanakuruhusu uongee, lakini kesho wanakufanya umeze maneno yako.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Mahmut KAR
Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Uturuki

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu