Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Serikali ya Sri Lanka Yafichua Ujahili Wao na Chuki kwa Uislamu na Waislamu

Habari:

Mnamo 10 Machi 2021, Waziri wa Usalama wa Umma wa Sri Lanka, Rear Admiral (Mstaafu) Sarath Weerasekara aliwasilisha ripoti ya tume ya pamoja ya mashirika anuwai bungeni kuhusu matokeo ya mashambulizi ya kigaidi ya Jumapili ya Pasaka 2019. Ripoti hiyo ilinukuu maelezo kuhusu jinsi Zaharan Hashim alivyo shawishiwa kufanya unyama huo na watu na mashirika 'yaliyohusishwa' na uhalifu huo nchini Sri Lanka na ng'ambo. Waziri huyo alipendekeza hatua kadhaa kwa mtazamo wa kuzuia ukatili kama huo katika siku zijazo. (Ceylontoday)

Maoni:

Sri Lanka imethibitisha tena kuwa Demokrasia bila kujali ukubwa na nguvu zao wanaendelea kuonyesha chuki yao kwa Uislamu na Waislamu, sambamba na uchafuzi Amerika wa sura  ya Uislamu na Waislamu. Ripoti hiyo imejaa utepetevu na ujahili. Licha ya kuonyesha kuhusika kwa mashirika manne hadi matano ya ujasusi ya kigeni katika kumaliza uhalifu, uwasilishaji wa mukhtasari hausubutu kuzitaja nchi hizi au majina ya watu waliohusika katika uhalifu huo wa kinyama. Badala yake, ilichagua kwa urahisi kugeuza uhasama kwa raia wao wa Kiislamu kama mawakala wa uhalifu, ikitoa wito wa kupigwa marufuku hijab, kuondolewa kwa maandishi ya Qur'an katika vitabu vya shule, kupigwa marufuku mashirika ambayo yamekuwepo kwa miaka mingi yakijishughulisha na Dawah (ulinganizi wa Uislamu) na kukamatwa kiholela kwa watu wengi. Yote yalifupishwa kama kupambana na 'msimamo mkali'. Kwa hivyo, badala ya kuwaadhibu wahalifu, serikali ya Sri Lanka inajipa 'leseni ya kukandamiza'.

Waislamu nchini Sri Lanka na ulimwenguni wanapaswa kutambua wazi kwamba ima wao ni Wanademokrasia au Madikteta, chuki yao kwa Uislamu na Waislamu iko mbele. Mateso wanayowaletea Waislamu unatokana na hofu yao na chuki kwa kile ambacho Mwenyezi Mungu (swt) amewaamuru wanadamu kukifanya katika maisha yao katika ulimwengu huu, na ambacho kwacho Waislamu wanatarajiwa kutoa ushuhuda juu yake. Chuki yao kwa Uislamu ni kubwa sana mpaka hata wafu kati ya Waislamu wamekiukwa heshima yao, kama tulivyoona hivi karibuni katika kuchomwa kwa lazima kwa wagonjwa wa Kiislamu wa Covid19 nchini Sri Lanka, licha ya WHO kuruhusu kuzika wafu. Ni kitendawili cha kweli kwamba taifa la kisiwa linaonyesha chuki yake kwa Uislamu mkesha wa kuamkia Karne moja ya Kuvunjwa kwa Khilafah, Ngao ya Uislamu na Waislamu mnamo 28 Rajab 1342 Hijria. Waislamu lazima watambue kuwa mambo yao yanaweza kulindwa tu na Khalifa na wanapaswa kuunga mkono kusimamishwa kwake tena katika ulimwengu wa Kiislamu ambaye utatoa haki ya kweli na amani kwa ulimwengu.

«إِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ»

“Hakika Imam (Khalifa) ni ngao watu hupigana nyuma yake na hujihami kwayo.” [Muslim]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Riadh ibn Ibrahim

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu