Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Habari na Maoni
Mgogoro wa Msitu wa Mau: Usimamizi Mbaya wa Rasilimali za Kiasili wa Serikali za Kisekula za Kirasilimali

Habari:

Serikali imeanzisha oparesheni ya kuwafurusha zaidi ya watu 40,000 kutoka katika msitu wa Mau ambao ni beseni kubwa la maji nchini Kenya ulio na ukubwa wa hektea 273,300 (ekari 675,000). Msitu huu ndio chanzo kikuu cha mito mingi inayomiminikia Ziwa Victoria ambalo ndio chanzo cha mto Nile, mto mrefu zaidi barani Afrika. Katika kile kinachowezekana kuwa janga la kibinadamu, mamia ya familia zinalala nje mwituni katika baridi kali baada ya nyumba zao kuchomwa, wazazi wametengana na watoto wao na tayari shule za msingi kumi na tano zimefungwa.

Maoni:

Kadhia ya msitu wa Mau tangu utawala wa Moi mpaka leo imegeuzwa kuwa chombo cha kisiasa na wanasiasa wamekuwa wakicheza mchezo wa kulaumiana juu ya kuhifadhi Eneo la Msitu wa Mau. Ufurushaji huu kwa mara nyengine tena umezua mdahalo mkali ndani ya uwanja wa kisiasa huku kundi la wanasiasa likiongozwa na Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Seneti Kipchumba Murkomen akionekana kupinga ufurushaji huo. Kwa upande mwengine, viongozi kutoka jamii ya Maasai wamejitokeza kuunga mkono oparesheni hiyo.

Mgogoro wa Mau umesababishwa na wanasiasa walafi ambao wamenyakua mamia ya hektea za ardhi yake. Kupitia miamala isiyo halali, wanasiasa hawa wafisadi huuza baadhi ya vipande vya ardhi ya msitu huu kwa watu masikini. Mnamo 1986, serikali ya Moi iliunda kile kinachojulikana kama shamba la majani chai la Nyayo Tea Zones; mradi wa serikali uliokusudiwa kuhifadhi msitu huo dhidi ya uharibifu zaidi au uangamizaji wake kupitia kuasisi ukanda wa usalama. Shirika hili la Maendeleo lilipaswa kuwepo kama shirika la kibiashara na huduma likizalisha majani chai na kuni kwa msingi wa kibiashara. Lakini, ni kupitia mradi huu ndio uliopelekea ugavi usio halali na unyakuzi wa msitu huu kutoka kwa wanasiasa hawa hawa. Katika ripoti ya ardhi iliyotolewa ya mnamo 2004 maarufu kama “Ripoti ya Ndung’u”, iliorodhesha ugavi wa msitu huo, ikiutaja kama usio halali na kupendekeza kufutiliwa mbali kwake. Mpaka sasa hakuna hatua ya kivitendo iliyochukuliwa.

Katika jamii inayokumbatia mfumo wa kirasilimali pamoja na njia zake ovu za umilikaji ardhi, mgogoro kama huu huibuka kila siku. Msingi wa mfumo huu unazunguka juu ya manufaa na tamaa ya ulimbikizaji mali kama kipimo chake, hivyo basi ufisadi na ufujaji ni mambo ya kawaida katika utawala wa urasilimali. Zaidi ya hayo, chini ya udhalimu wa mfumo huu muovu, umilikaji wa ardhi hukusudia ukiritimba na hatimaye kuuza kwa bei za ghali mno.

Ufurushaji katika msitu huu unaendelea kudhihirisha kasoro ya serikali ya kisekula inayojipiga vita yenyewe huku baadhi ya viongozi wake wakiunga mkono ufurushaji huu huku wengine wakiupinga! Hii yaonesha kuwa, serikali za kirasilimali huhudumu kwa mtazamo ya kinafiki katika kutatua kadhia. Ufurushaji wa kikatili uliofanywa na maafisa wa usalama umeonesha jinsi uongozi wa kisekula hauna mipango madhubuti katika utatuzi wa kadhia nyeti. Kwa kuwa urasilimali uko kwa ajili ya mabwenyenye na wala si kwa ajili ya watu wa kawaida, watu wanaogusika (masikini) ndio wanaofurushwa huku ‘wasiogusika’ (mabwenyenye) wakiachwa.

Kiujumla, usimamizi mbaya wa rasilimali pamoja na sera katili za ardhi za serikali ya kisekula ndizo zilizoleta janga hili. Uislamu umeunda sheria za ardhi ima ya umma, ya kibinafsi au ya serikali. Katika Uislamu, rasilimali asili kama mikondo ya maji ni mali za umma, ambazo kamwe haziwezi kumilikiwa na mtu binafsi au na maafisa wa serikali.

Natija yake, migogoro hii haitamalizika, mpaka kusimamishwe tena Khilafah katika njia ya Utume dola itakayotekeleza Uislamu kikamilifu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir na
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 09 Agosti 2020 06:54

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu