Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Habari na Maoni

Marekani Kujitoa Kijeshi Syria; Kuna nini nyuma yake?

Habari:

Trump Aondosha Majeshi ya Marekani kutoka Syria.

Maoni:

Tangazo la Trump kuondosha jeshi ndani ya Syria limezua patashika ya upinzani ndani ya bunge la Congress, na hata kutoka kwa watu muhimu ndani ya Chama cha Republican. Pia, Kamanda wa Marekani wa Afisi Kuu ya Majeshi, Jenerali.Joseph Votel na balozi wa Marekani wa muungano wa wanaopigana na Islamic State, Brett H. McGurk, walipinga vikali kuondoshwa kwa jeshi, ikisababisha kujiuzulu kwa Waziri wa Usalama Jim Mattis. Lakini wa mwanzo kabisa kuonesha wasiwasi mkubwa walikuwa ni wa Kurdi kutoka Syria.

Kwa hiyo maswali yanajitokeza, ni kwa nini Trump amekakamia maamuzi yake licha ya upinzani wote huu? Je ni kitendo cha kukurupuka cha Trump au ni sehemu ya mpango mpana?

Kwanza, ni lazima ieleweke kuwa kujitoa kwa jeshi haimaanishi kwa hali yoyote ile kuwa inaashiria kujitoa kwa Marekani au athari yake juu ya eneo. Na hususan lau jeshi litatoka itajumuisha tu sehemu ndogo ambayo haizidi elfu kadhaa ya wanajeshi kwa mujibu wa hali ya Syria. Lakini historia inatufunza kinyume chake. Uvamizi wa kijeshi wa kigeni au uwepo wa jeshi ni moja ya ala nyingi za dola za kikoloni katika kufikia malengo yao.

Hili lilisemwa wakati wa nyuma Machi 2018, Trump alisema kuwa atawaregesha wanajeshi nyumbani punde "watakaposhinda vita." Hakuweka siku maaalumu lakini alieleza malengo yake wakati huo pasi na upinzani wowote. Lakini hivi sasa yuko tayari kulitekeleza hili, kelele zinachipuza kama ambaye halikukuwepo suala hili. Kwa hiyo, upinzani dhidi ya maamuzi ya Trump lazima yatathminiwe kwa mtizamo kwamba tayari kuna mzozo baina ya baadhi ya pande husika ndani ya Marekani na Trump.

Licha ya tofauti hizi ambazo zimetokamana na njia na rasilimali, mpango wa Marekani juu ya Syria ulikuwepo wazi. Utawala wa Syria na nidhamu yake ya kisekula lazima ubakie ima Bashar al-Assad awepo au asiwepo, na upinzani ulio na mradi wa Kiislamu lazima upunguzwe kasi, udhibitiwe na umalizwe. Hili linafupisha kwa uhakika sera ya Marekani ndani ya miaka 7 iliyopita ndani ya Syria pamoja na washirika wake, Uturuki, Iran na Urusi.

Kutokana na sera hii, Utawala dhaifu wa Syria uliweza kudhibiti tena takribani kila eneo ndani ya Syria isipokuwa eneo la Idlib ambapo kumebakia chembechembe za upinzani hivi sasa na eneo la Kaskazini ambapo wa Kurdi wanamiliki eneo lao wanalojitawala. Mchezo unakaribia kuisha. Kikwazo pekee dhidi ya kuunganisha na kuufufua tena utawala wa Syria ni upinzani wa Syria na wa Kurdi walioko Kaskazini.

Ama kuhusu eneo la Kikurdi, Marekani imewajenga na kuwalinda dhidi ya Uturuki na imewatumia kikamilifu katika kupigana na kundi la Bagdadi na makundi ya Kiislamu. Marekani kujitoa kijeshi kutawaacha wakiwa hawana mtetezi dhidi ya tishio la Uturuki na upande mwingine tishio la Bashar al-Assad ambaye anataka kuiweka Syria yote chini ya udhibiti wa serikali yake.

Ndio sababu viongozi wa Kurdi walihisi joto na haraka wakazindua mazungumzo ya pande mbili na Damascus kuhusu makubaliano ya makaazi waliposikia kuhusu kujitoa kwa Marekani. Kwa hiyo wa Kurdi wamelazamishwa kiujanja kufanya mazungumzo na utawala wa Syria ambayo hatima yake ni kuunganishwa kwa Kaskazini ya Syria kuwa Syria "iliyoungana."

Pia, majibu muhimu lakini ya kujieleza yalitoka kwa Waziri wa Kigeni wa Uturuki Mevlut Cavusoglu. Alisema kuwa Uturuki na viongozi wa kiulimwengu watashauriana kuhusu kufanya kazi na Rais wa Syria Bashar al-Assad lau atashinda kura za kidemokrasia. Na Rais wa Sudan Omar al-Bashir akamzuru Bashar al-Assad na kumfikishia matumaini yake kuwa Syria hivi karibuni itarudi tena katika dori yake muhimu ya kieneo. Kwa kuitambua rasmi serikali hii ya kimauaji, inafichua na wakati huo huo inadhibitisha mpango unaofuata wa Marekani.

Mazungumzo kuhusu kurudi kwa Syria katika Muungano wa (Arab League) tayari yanaendelea. Hili lilielezewa na mtu katika makao makuu ya Muungano huo mjini Cairo siku ya Alhamisi pamoja na Sputnik.

Mapema, chanzo katika serikali ya rais wa Tunisia kilisema kuwa nchi nyingi za Kiarabu ikijumuisha Tunisia na Algeria, zinashirikiana katika juhudi za kuirudisha Syria katika shirika hilo. Kwa mujibu wa mzungumzaji, Tunisia, Iraq na Algeria ziko mbioni kuhakikisha kuwa Syria inashiriki tena katika kazi za Muungano huo.

Kujitoa kwa Marekani kulipongezwa na Wizara ya Kigeni ya Urusi kwa kusema kuwa hatua hiyo itatoa nafasi ya mchakato wa kisiasa ndani ya Syria.

Na mazungumzo ya pande mbili kati ya Trump na Erdogan kabla ya kutangaza kujitoa, kunadhibitisha kuwa kujitoa kwa Marekani sio kitendo cha kukurupuka bali ni mpango ndani ya mpango mpana muovu wa kuyamaliza mapinduzi ndani ya Syria pamoja na washirika wake.

﴿وَإِذْ يَمْكُرُ بِكَ الَّذِينَ كَفَرُوا لِيُثْبِتُوكَ أَوْ يَقْتُلُوكَ أَوْ يُخْرِجُوكَ وَيَمْكُرُونَ وَيَمْكُرُ اللَّهُ وَاللَّهُ خَيْرُ الْمَاكِرِينَ

“Na [kumbuka, Ewe Muhammad], walipo kupangia mpango walio kufuru wakufunge, au wakuuwe, au wakutoe [kutoka Makkah]. Wakapanga mipango yao, na Mwenyezi Mungu akapanga yake. Na Mwenyezi Mungu ndiye mbora wa mipango.  [Al-Anfal: 30]

Imeandikwa Kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Okay Pala
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Uholanzi

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 09 Agosti 2020 06:42

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu