Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Uislamu ndio Wokovu Pekee kwa Watoto wa Tharparkar

(Imetafsiriwa)

Habari:

Ripoti ya kuogofya ya vifo vya watoto zaidi ya 36 katika wilaya ya Tharparkar, vilivyosababishwa na maradhi mbalimbali katika mwezi wa kwanza wa 2022, imesababisha kizungumkuti kwa serikali ya mkoa. (Tribune Pakistan)

Maoni:

Kwa mujibu wa rekodi ya Idara ya Afya ya Tharparkar, zaidi ya watoto 600 waliozaliwa walikufa katika mwaka uliotangulia, 2021. Vifo hivi vilitokana haswa na kutopatikana kwa huduma za afya na lishe duni. Kama tunavyojua sote kwamba maisha yanategemea maji, watu wa Thari hutumia sehemu kubwa ya siku yao kutafuta maji safi ya kunywa, na katika hili, usafi wao ni tofauti na usafi wa kawaida.

Kuna vyanzo tofauti wanavyotumia, kama kukusanya maji ya mvua na visima virefu vilivyochimbwa. Kwa sababu ya matumizi ya mara kwa mara ya maji ya ardhini yenye floridi ya juu, maradhi ya fluorosis yamekuwa janga eneo la Thar, na kusababisha fluorosis ya meno, ulemavu wa viungo, na matatizo ya tezi na figo. Hii inasababisha watu wazima wenye utapiamlo kuzalisha na kulea (kama watabakia hai) watoto wenye utapiamlo. Wilaya ya Tharparkar ina wakazi wanaokadiriwa kuwa milioni 1.6, waliosambaa zaidi ya kilomita 22,000 mraba. Uhaba wa maji ni tatizo kubwa la eneo hili. Na visima vilivyochimbwa vimepatikana kuwa chanzo pekee endelevu cha maji ya ardhini. Wamekuwa wakiishi kwa maji yaliyochafuliwa, chumvi na maji ya ardhini ambayo hayajatibiwa. Siku yao huanza kwa kubeba mitungi ya maji, ambayo hujaza kutoka kwa maji ya mvua yaliyohifadhiwa au matangi madogo ya asili, baada ya kutembea zaidi ya kilomita 3 kwenye joto kali.

Serikali tofauti tofauti kwa miaka mingi zimetumia kisiasa ukame, njaa na vifo vya watu wa Thari kwa manufaa yao wenyewe. Miradi ya maji ilitangazwa ambayo haikufikia kukamilika; kutokuwepo kwa vituo vya matibabu huongeza mafuta kwenye moto na kutafuta msaada wa matibabu kunaweza kuwagharimu watu wanaolazimika kutembea umbali mrefu na kutumia pesa nyingi. Mnamo 2021, Mahakama ya Upeo iligundua vifo vya watoto, na iliona kuwa hakuna madaktari, dawa au vituo vya afya vilivyopatikana katika hospitali za Tharparkar, ambayo inaonyesha kukatika kabisa mafungamano ya Serikali na watu.

Watu wa Ummah huu wanahisi uchungu kwa kaka na dada zao na tunaona watu binafsi na mashirika mengi yakifanya kazi kwa ajili ya watu wa Thari. Kambi za matibabu za kibinafsi zimewekwa na watu na msaada pia hutolewa lakini bila shaka hizi haziwezi kukidhi mahitaji. Kwa njia hii watu huishia kulipa gharama mara mbili, kwanza kwa Serikali kwa njia ya kodi na pili kwa kuwasaidia watu wa Thari moja kwa moja. Suala hili linahitaji mpango ufaao na haliwezi kusuluhishwa, Tharparkar ndio jangwa pekee lenye rutuba duniani na kwa mujibu wa uchunguzi wa kijiolojia wa hifadhi ya makaa ya mawe ya Pakistan inakadiriwa kuwa takriban tani bilioni 175, na kuifanya kuwa mojawapo ya hifadhi kubwa zaidi za makaa ya mawe ya lignite Dunia. Endapo hifadhi hizi zitatumiwa kwa uaminifu basi sio tu zinaweza kusaidia kutatua matatizo ya nishati ya Pakistan, vilevile zinaweza kupanga maisha ya utu kwa watu wa Thari. Hata kama hakukuwa na hifadhi ya makaa ya mawe, na kutengeneza mifereji ya maji kwa ajili ya kuwasaidia watu wa Thar haikuwezekana, jukumu la Serikali la kuokoa maisha na riziki za watu wake bado linabakia.

Katika Uislamu, Mtawala ni mmoja kwa Ummah mzima wa Kiislamu, bila kujali rangi au eneo la makaazi. Ni chini ya kivuli cha Khilafah pekee, ndipo tutaona afueni kwa Ummah katika nyanja zote za maisha. Mali za umma zitatumika kwa manufaa ya umma. Khalifah atateua magavana na hao magavana watawajibika kwa eneo lao. Khalifah mwenyewe atafuata mtindo wa Khalifah Umar Bin Al-Khattab aliyeongoka, ambaye kipindi chake cha utawala kilikuwa kirefu zaidi kati ya Makhalifa Waongofu wanne wa mwanzo. Alijulikana sana kwa hisia zake kali za uwajibikaji katika kushughulikia mambo ya Waislamu. Alifanya doria usiku ili kuhakikisha watu wanatunzwa vyema. Mwenyezi Mungu atujaalie mtawala muadilifu.

Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«مَا مِنْ عَبْدٍ يَسْتَرْعِيهِ اللَّهُ رَعِيَّةً يَمُوتُ يَوْمَ يَمُوتُ وَهُوَ غَاشٌّ لِرَعِيَّتِهِ إِلَّا حَرَّمَ اللَّهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ»

“Hakuna mja yeyote ambaye Mwenyezi Mungu anamfanya msimamizi wa raia kisha akafa ilhali anawaghushi raia wake, isipokuwa Mwenyezi Mungu amemuharamishia Pepo.” [Al-Bukhari na Muslim]. Riwaya nyengine ni: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«فَلَمْ يَحُطْهَا بِنُصْحِهِ لَمْ يَجِدْ رَائِحَةَ الجَنَّة» “Kisha asiangalie mambo yao kwa wema na ikhlasi, hatanusa harufu ya Pepo.” Riwaya ya Muslim ni: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«مَا مِنْ أميرٍ يلي أمور المُسْلِمينَ، ثُمَّ لا يَجْهَدُ لَهُمْ وَيَنْصَحُ لَهُمْ، إِلَاّ لَمْ يَدْخُلْ مَعَهُمُ الْجَنَّةَ»

“Hakuna kiongozi yeyote, anayetawala mambo ya Waislamu, asijizatiti kwa ajili yao na asiwatumikie kwa ikhlasi, isipokuwa hataingia pamoja nao Peponi.”

 Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ikhlaq Jehan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu