- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Maneno Hayatoshi Kuuadhibu Utawala wa Modi wenye Chuki na Uislamu
(Imetafsiriwa)
Habari:
Hivi majuzi, serikali ya Narendra Modi ilijikuta matatani baada ya baadhi ya wanachama wake kutoa matamshi ya dharau dhidi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Katika nia ya kujinasua kutoka kwa ghadhabu inayozidi kuongezeka katika ulimwengu wa Kiislamu, Modi alichukua hatua haraka kuwasimamisha kazi maafisa wa BJP wenye hatia lakini hii haikusaidia kuzuia kashfa dhidi ya serikali yake. [The Times]
Maoni:
Katika ulimwengu wa Kiislamu, kumekuwa na hasira ya kidiplomasia dhidi ya utawala wa Modi kwa matamshi machafu yaliyotolewa na maafisa wa BJP. Iran, Kuwait na Qatar ziliwasilisha malalamiko rasmi mbele ya maafisa wa India waliokusanyika, huku Saudi Arabia ikichapisha taarifa ya kulaani tukio hilo. Karipio kali zaidi lilitoka kwa Qatar, ambayo ilitangaza “kuruhusu matamshi kama hayo ya chuki kwa Uislamu kuendelea bila adhabu, ni hatari kubwa kwa ulinzi wa haki za binadamu.” [The Times]
Hata hivyo, zaidi ya maneno matupu, kulikuwa na pingamizi la kushindwa kwa pamoja kwa watawala wa ulimwengu wa Kiislamu kuchukua hatua kali. Hakukuwa na hatua ya kuwafukuza wafanyikazi wa kidiplomasia wa India na kufunga balozi zake au kuwafukuza wafuasi matajiri wa BJP wanaoishi katika nchi za Ghuba. Kando na wito wa kususia bidhaa za India kutoka kwa baadhi ya maeneo ya kidiplomasia, hakukuwa na kutajwa kwa kukata usambazaji wa kawi kwa India au kukata aina zote za mafungamano ya kibiashara, ambayo yote haya yangeilazimisha serikali ya kibaguzi ya Modi kubadili mkondo. Kukosekana kwa hatua za pamoja dhidi ya Modi kunadhihirisha tu udhaifu wa watawala wa ulimwengu wa Kiislamu kutetea maadili ya Kiislamu. Pia inafichua kwamba watawala hawa wanataka tu kuwaridhisha raia wao nyumbani, huku wakihakikisha mikataba ya kawi na biashara yenye faida kubwa inaendelea pamoja na utawala dhalimu wa Modi.
Hata hivyo hali ya kutojali ya viongozi wa ulimwengu wa Kiislamu haishangazi. Viongozi hao hao wametazama kwa ukimya kwa miaka mingi jinsi serikali ya Modi inayochukia Uislamu imechochea ghasia kimakusudi na kuunga mkono kikamilifu ukandamizaji wa wakaazi wake wa Kiislamu huko Kashmir na majimbo mengine ya India. Kwa hakika, wafuasi wa dhehebu la Kibaniani waliochochewa na ajenda ya Modi ya Hindutva mara kwa mara wamebomoa misikiti, kuua Waislamu wengi mchana kweupe, na kuwapora wanawake wa Kiislamu heshima yao. Matendo haya yote ya kinyama yameangukia kwenye uziwi. Imepokewa kutoka kwa Abdullah ibn Umar: “Nilimuona Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akiizunguka Al-Ka’bah na kusema:
«مَا أَطْيَبَكِ وَأَطْيَبَ رِيحَكِ، مَا أَعْظَمَكِ وَأَعْظَمَ حُرْمَتَكِ، وَالَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ لَحُرْمَةُ الْمُؤْمِنِ أَعْظَمُ عِنْدَ اللَّهِ حُرْمَةً مِنْكِ؛ مَالِهِ وَدَمِهِ وَأَنْ نَظُنَّ بِهِ إِلَّا خَيْراً»
“Jinsi gani ulivyo mzuri na jinsi manukato yako yalivyo mazuri! Jinsi ulivyo mkuu na jinsi utakatifu wako ulivyo mkuu! Naapa kwa yule ambaye nafsi ya Muhammad imo mkononi mwake, utakatifu wa Muumini ni mkubwa zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko utakatifu wako, katika mali yake, na maisha yake, na tusimdhanie chochote isipokuwa kheri.” [Sunan Ibn Majah] Hakuwezi kuwepo na mafungamano ya amani na dola ambayo inaua wakaazi wake Waislamu na kumvunjia heshima Mtume wa Uislamu.
Unyenyekeshaji wa Waislamu nchini India mikononi mwa utawala dhalimu wa Modi na mashambulizi ya kimataifa dhidi ya Uislamu yatakwisha tu pale uongozi usio na uwezo wa ulimwengu wa Kiislamu utakapofagiliwa mbali kwa kuregea kwa Khilafah Rashida.
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]
“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al Anfal: 24]
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Hizb ut Tahrir na
Abdul Majeed Bhatti