Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Ziara ya Kamala kwa Afrika Inalenga Unyonyaji na Kuua Mfumo wa Kijamii

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo tarehe 26 Machi 2023, Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris aliwasili Accra Ghana kuanza ziara yake ya nchi tatu barani Afrika. Baadaye alitembelea Tanzania na Zambia. Akiwa ni kiongozi mkubwa wa 18 wa Marekani kuzuru Afrika mwaka huu, alitua Dar es Salaam, Tanzania tarehe 29/03/2023 kwa ziara ya siku tatu.

Maoni:

Katika ziara yake nchini Tanzania, Makamu wa Rais Kamala Harris aliweka wazi kuwa ziara yake italenga pamoja na mambo mengine kuimarisha demokrasia na matakwa ya demokrasia, hasa “ya watu” wa Afrika na hususan Tanzania. Kutokana na kauli hii Marekani inatuma ujumbe kuhusu dhamira yake ya kuunga mkono mawazo maovu ya kidemokrasia ikiwa ni pamoja na ushoga na mapenzi ya jinsia moja (LGBTQ) nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Kabla ya kuja Tanzania, Makamu wa Rais Kamala alizungumza kuhusu haki za mashoga na mapenzi ya jinsia moja (LGBTQ) alipokuwa katika ziara yake ya nchini Ghana, ambako mchakato unaendelea wa kupitisha sheria kali dhidi ya vitendo vya ushoga na mapenzi ya jinsia moja (LGBTQ). Katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo, (Kamala) alisema kwa kujiamini:

“Ninahisia kali sana kuhusu umuhimu wa kuunga mkono uhuru na kusaidia kupigania usawa baina ya watu wote, na kwamba watu wote waamiliwe kwa usawa”

“Pia nitasema kwamba, kadhia hii (ya mashoga) tunaizingatia na kuichukulia kuwa  ni kadhia ya haki za binadamu, na hilo halitabadilika.”

Nchini Tanzania Kamala iliidhinisha msaada wa dolari za Marekani bilioni 1 kwa ajili ya programu za kuwawezesha wanawake. Kwa hivyo, bila shaka ni kwamba miongoni mwa malengo mengine ya ziara ya Harris barani Afrika ni kuimarisha dhamira ya kuharibu mfumo wa kijamii kwa kuharibu maadili ya familia na kuhamasisha ajenda ya ushoga na mapenzi ya jinsia moja (LGBTQ).

Pia, ziara ya Kamala imekuja miezi mitatu tu baada ya Mkutano wa Viongozi wa Marekani na Afrika, uliofanyika Disemba 2022, wakati ambao pia Rais Samia alifanya ziara rasmi ya kikazi kwa Rais Xi Jinping wa China Novemba 2022. Bila shaka, China imewekeza sana nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla katika kipindi cha miongo miwili iliyopita, ziara hii ni sehemu ya mkakati wa Marekani wa kukabiliana na ongezeko la ushawishi wa China nchini Tanzania na bara zima kwa ujumla.

Zaidi ya hayo, ziara ya Kamala ililenga kuimarisha ukoloni na unyonyaji wa rasilimali za Tanzania hususan madini. Kwa sasa Amerika iko kwenye ujenzi wa kituo cha uchakataji wa madini ambayo hutumiwa kutengeneza betri za gari za umeme. Kamala alisema: “Hii itatoa nikeli ya kiwango cha kutengeneza betri kwa Marekani na masoko ya kimataifa punde tu ifikapo 2026. Mradi huu ni wa mfano na muhimu, unaotumia teknolojia ya ubunifu na ya utoaji wa hewa chafu kwa kiwango kidogo… Muhimu zaidi ni kuwa, malighafi zitachakatwa hivi karibuni hapa Tanzania na Watanzania. Mradi huu utasaidia kukabiliana na mgogoro wa hali ya hewa, kujenga ugavi imara wa kimataifa, na kuunda viwanda vipya na nafasi za kazi na ajira… Kuna fursa kubwa ya ukuaji hapa” (Whitehouse, Hotuba ya pamoja ya Makamu wa Rais Harris na Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania kwa vyombo vya habari, Machi 30, 2023).

Kwa kifupi, ziara ya Kamala nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla itanufaisha tu na kuendeleza ajenda ya kibepari ya Marekani na kusukuma Tanzania na Afrika kwenye mikopo isiyoisha, udumavu wa kimaendeleo, unyonyaji na utegemezi, huku katika mtazamo wa kijamii ikilenga kuharibu familia na kueneza uovu usioelezeka wa ushoga na mapenzi ya jinsia moja (LQBTQ).

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Said Bitomwa

Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Tanzania

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu