Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mayatima wa Gaza Wamwaga Machozi kwa ajili ya Wazazi Waliotoweka na Uchungu wa Njaa siku ya Idd

(Imetafsiriwa)

Habari:

Miezi 8 ya awamu mpya ya vitendo vya uvamizi, UNICEF inakadiria kuwa angalau watoto 17,000 mjini Gaza wako peke yao au kutenganishwa na familia zao. Tedros Adhanom Ghebreyesus, mkuu wa Shirika la Afya Duniani la Umoja wa Mataifa, alionya kwamba “idadi kubwa ya wakaazi wa Gaza sasa wanakabiliwa na janga la njaa na hali za uhaba wa chakula. “Licha ya ripoti za kuongezeka kwa utoaji wa chakula, kwa sasa hakuna ushahidi kwamba wale wanaokihitaji zaidi wanapokea kiasi cha kutosha na chakula bora”. Hadi sasa, zaidi ya vijana 8,000 wamegunduliwa na kutibiwa kwa utapiamlo mkali, wakiwemo watoto 1,600 walio na aina hatari zaidi ya ugonjwa huo.

Maoni:

Katika kipindi cha miezi 8 iliyopita wanawake na watoto wa Gaza wamekabiliwa na mtihani mkubwa zaidi tangu uvamizi wa umbile la Kiyahudi. Tunashuhudia alama za nyakati za mwisho. Ni jambo la dharura kwamba sisi, kama wanawake wa Kiislamu ambao hatuko moja kwa moja katika ardhi ya uvamizi, tutekeleze jukumu letu kwa Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake (saw). Uwajibikaji wetu ni mkubwa, na mtihani unaweza usiwe wa kimwili kwa njaa, mabomu na kupoteza watoto, lakini mtihani ni mmoja wa Iman na Aqeeda. Ufikiaji wa Jannah (Pepo) unaweza kufafanuliwa kwa jinsi tunavyojifungamanisha na maamrisho ya Mwenyezi Mungu (swt) kuitikia mwito wa dawah na kusimamisha Khilafah kama mamlaka ambayo itatumikia Quran na Sunnah, sio ajenda mkoloni ya utawala wa Magharibi. Wanawake na watoto wa Gaza watasamehewa kwa kile wasichoweza kufanya. Udhaifu wao na ukosefu wa rasilimali sio kosa lao kulibeba.

Hata hivyo, sisi kama Ummah tunaodai kuwa sehemu ya mwili wa kilimwengu wa Waislamu uliounganishwa na Shahada, hatuwezi kukataa kwamba janga hili linahitaji hatua na sio dua tu. Katika Quran Tukufu, Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:

[إِنَّ اللّهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالإِحْسَانِ وَإِيتَاء ذِي الْقُرْبَى وَيَنْهَى عَنِ الْفَحْشَاء وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ يَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ]

“Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha kufanya uadilifu, na hisani,na kuwapa jamaa; na anakataza uchafu, na uovu, na dhulma. Anakuwaidhini ili mpate kukumbuka.” [16:90].

Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) kwamba hii iwe ni Idd ya mwisho ambayo tunashuhudia ukandamizaji kama huo wa Ummah wetu kote duniani na kwamba ufueni, uadilifu na heshima ya Ummah vionekane chini ya kivuli cha Amiri wa Waislamu. Amin.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammad
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu