Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Je, Kura ya Kutokuwa na Imani ni Mchakato wa Kisiasa au wa Kimahakama?

(Imetafsiriwa)

Habari:

Wabunge nchini Kenya wameanza mchakato wa kumwondoa naibu rais wa nchi hii afisini. Wale wanaounga mkono juhudi hizo wanamshutumu Rigathi Gachagua kwa kuhusika katika maandamano ya Juni ya kupinga serikali - ambayo yaligeuka kuwa mabaya - pamoja na kuhusika katika ufisadi, kuhujumu serikali na kuendeleza siasa za mgawanyiko wa kikabila. Naibu rais amepuuzilia mbali madai hayo.

Maoni:

Jumla ya wabunge 291 walitia saini hoja hiyo – ikivuka kwa mbali kiwango cha thuluthi moja kinachohitajika ili kupigiwa kura. Msukumu wa kura ya kumtimua ulianzishwa na Mwengi Mutuse, mbunge kutoka muungano wa Ruto mwenyewe. Naibu Rais anatuhumiwa kujilimbikizia mali inayokadiriwa kufikia shilingi bilioni 5.2 (€35.96 milioni) ndani ya miaka miwili, licha ya mshahara wa mwaka wa Euro 83,520 pekee. Anakabiliwa na hoja 11 za kushtakiwa, ikiwa ni pamoja na madai kuwa alipingana na Ruto hadharani na kufananisha serikali na kampuni, akipendekeza waliopigia kura muungano huo walikuwa wastahiki wa kwanza wa kazi za umma na miradi ya maendeleo. Naibu huyo anadai kutengwa na Ruto katika miezi ya hivi majuzi na anakanusha madai kuwa alihusika na maandamano ya kuipinga serikali miezi kadhaa iliyopita.

Maonyesho ya kisiasa hayatakoma kamwe chini ya mfumo wa kijanja wa kisiasa wa Demokrasia. Kama ilivyo katika mkondo mwingine wa kisiasa, Seneta wa Makueni Dan Maanzo amewasilisha ombi la kumshutumu Rais William Ruto katika Seneti ili kujadili mienendo ya Raisi wa Nchi. Seneta huyo amemshutumu Rais kwa kukosa kuwalinda Wakenya kwa mauaji ya polisi, utekaji nyara, mateso na watu kupotezwa kwa nguvu. Viongozi wa kisiasa hujitoa muhanga kwa ajili ya kupata maslahi ya kisiasa, kiuchumi na kijamii kupitia mamlaka ya mazungumzo ya kikanda na kikabila ambayo hutumiwa kama zana za mapato na mafanikio ya kisiasa.

Kulingana na itikadi ya kisekula ambayo inaamini katika kutenganisha dini na siasa. Hakuna Serikali katika ulimwengu wa kisasa iliyo na njia ya kiakhlaki ya kuiendesha wala mwanasiasa kutokuwa na ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka na ulachu. Kinachojulikana kama uwajibishaji katika Demokrasia umeundwa kwa ajili ya kipote cha mabepari kuvikamata vyombo vya tawala. Kwa kuwa Demokrasia inachipuza kutokana usekula, mtawala kwa hiyo hazuiliwi kutoka na udhalimu kwa kumcha Mungu au kuwahesabiwa na Mungu. Kwa kukosekana kipengee hiki cha msingi cha uwajibikaji yaani ucha Mungu (taqwa) kiongozi katika mfumo wa kidemokrasia anaweza kudhulumu ikiwa hatazuiliwa na zana za serikali.

Kinyume na Mfumo wa Utawala wa Kiislamu, ambapo Khalifa anakuwa hana kinga dhidi ya Sharia ya Kiislamu na anaweza kuitwa na mahakama ya sheria ikiwa lolote kati ya matendo yake, ya kibinafsi au ya kiserikali, yataonekana kuwa ya kutiliwa shaka. Ni muhimu kutaja kuwa Khalifa si mtakatifu bali ni binadamu ambaye ni una uwezo wa kukosea. Hii ndiyo sababu mifumo kama hiyo ya uwajibikaji ya kina ipo ndani ya mfumo wa utawala wa Kiislamu. Ingawa Khalifa si mtu mtakatifu, ni lazima awe Muislamu na ‘adl (mwadilifu) na hawezi kuwa fasiq (mhalifu).

Zaidi ya hayo, chini ya Khilafah, Ummah unalazimika kuona kuwa kumhesabu mtawala sio tu kuwa ni haki yao bali kama wajibu wao mtukufu, wakikosa kutekeleza watakuwa ni wana madhambi. Hii ina maana kwamba vipengee vyote vya serikali vinafanya kazi katika kufikia malengo ya Kiislamu si malengo ya kimada wala kiki ya kisiasa.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu