Jumamosi, 19 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kadhia ya Palestina ni Kadhia ya Umma wa Kiislamu, sio Jumuiya ya Kimataifa

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mkuu wa Majeshi (COAS), Jenerali Syed Asim Munir, mnamo Ijumaa, tarehe 15 Novemba 2024, alihutubia sherehe maalum ya Mazungumzo ya Margalla 2024 yaliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Sera ya Islamabad (IPRI). COAS ilizungumza juu ya mada ‘Dori ya Pakistan katika Amani na Utulivu.’ Alisema kwamba Pakistan haitakuwa sehemu ya mzozo wowote wa kimataifa. Badala yake Pakistan itaendelea kucheza dori yake kwa amani na utulivu wa kimataifa. Pakistan daima imekuwa ikisisitiza kuanzishwa kwa dola huru ya Palestina. [Chanzo]

Maoni:

Hotuba hii ya Jenerali Asim Munir ilikuwa taarifa ya sera kuhusu masuala mbalimbali yakiwemo Palestina, Kashmir, ‘ugaidi’, itikadi kali za India, habari ghushi na mabadiliko ya tabianchi. Kauli hii ya sera ilikuja siku chache kabla ya maonyesho muhimu ya ulinzi, IDEAS 2024, ili kuonyesha uwezo wa kijeshi wa Pakistan.

Inaonekana kana kwamba Jenerali Asim Munir alihutubia matakwa ya Waislamu wa Pakistan ya kuhamasishwa kwa majeshi ili kukomesha ugaidi wa umbile la Kiyahudi, ambalo linapewa silaha na fedha na ulimwengu wa Magharibi unaoongozwa na Marekani. Tangu tarehe 7 Oktoba 2023, Waislamu wa Pakistan wametaka kwamba baba zao na watoto wao katika vikosi vya jeshi kuhamasishwa kukomboa Al-Masjid Al-Aqsa, Gaza na Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, bila kujali gharama tunayopaswa kubeba.

Utawala wa Munir-Sharif hapo awali ulidai kuwa hauwezi kufanya lolote kwa sababu ya kutokuwepo kwa Njia ya Mawasiliano (GLOC). Hata hivyo, watu wamekataa kisingizio hiki duni. Wanaona kwamba wakati wowote wakoloni wa Magharibi wanapohitaji askari wetu popote pale duniani, uongozi wa kijeshi huwatuma. Katika hotuba hiyo hiyo, Jenerali Asim Munir alisema, “jumla ya walinda amani 235,000 wa Pakistan wameshiriki katika misheni ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kudumisha amani duniani na Wapakistani 181 pia wamejitolea maisha yao katika suala hili.” Basi kwa nini watawala wasikusanye majeshi yetu ili kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina?

Sasa utawala wa Munir-Sharif umekuja na kisingizio chengine, na kusema kwamba Pakistan haitakuwa sehemu ya mzozo wowote wa kimataifa. Kadhia ya Palestina si mzozo wa kimataifa unaopaswa kutatuliwa na dola kubwa za sasa za wakoloni. Palestina ni ardhi ya Kiislamu ya Kharaji. Kadhia yake ni kadhia ya Umma wa Kiislamu na majeshi yake pekee. Kuhusu Kashmir, hata kama tulikubali kisingizio cha utawala, Kashmir inachukuliwa kuwa sehemu ya Pakistan. Kwa hivyo, kwa nini watawala wa Pakistan hawakukusanya vikosi vyetu vya jeshi kuikomboa Kashmir Iliyokaliwa, wakati Dola ya Kibaniani ilipovuka mstari mwekundu wa mwisho, kwa kunyakua Kashmir kwa nguvu mnamo 5 Agosti 2019?

Uhalisia ni kwamba utawala wa Muneer-Shabaz ni kibaraka wa wakoloni, mithili ya tawala zilizopita. Msingi wa sera zao ni maslahi ya wakoloni, bila kuzingatia usalama wa ardhi za Waislamu wala Dini yao. Hakuwezi kuwa na mkanganyiko kati ya Waislamu wa Pakistan na vikosi vyake vya jeshi. Ramani ya njia ya kuepuka udhalilifu ni kuwang'oa vibaraka wa wakoloni, kusimamishwa Khilafah kwa Njia ya Utume, na kuunganisha ardhi za Waislamu kuanzia Indonesia hadi Morocco. Hapo ndipo Khalifa Rashid atakusanya mamilioni ya askari wa Waislamu kukomboa ardhi zote zinazokaliwa kwa mabavu.

Kusimamishwa kwa Khilafah Rashida sio ndoto. Ni faradhi ya Shariah na ni bishara njema ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Mtume (saw) amesema,

«ثُمَّ تَكُونُ مُلْكًا جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ ثُمَّ سَكَتَ»

“…Kisha utakuweko utawala wa kutenza nguvu (ملكًا جبرية), utakuwepo katika muda apendao Mwenyezi Mungu uwepo, kisha atauondoa apendapo kuuondoa, kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume.” Kisha yeye (saw) akanyamaza.(Ahmed)

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Shahzad Shaikh - Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu