- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Wanawake lazima Wauone Udanganyifu wa Fikra ya Anuwai na Ushirikishwaji katika Siasa za Kiliberali
(Imetafsiriwa)
Habari:
Chaneli ya Kiislamu ilijadili ripoti mpya inayofichua miondoko ya chuki dhidi ya Uislamu, kutengwa kitaaluma inayoathiri wanawake wa Kiislamu kwenye vyombo vya habari. Athari hii imeenea hadi kwa masuala ya afya ya akili na imani katika mashirika.
Ilijadili jinsi mwonekano wa waandishi wa habari wa kike wa Kiislamu unavyoathiriwa haswa na uchokozi mdogo, maoni potofu, na tofauti za mishahara.
Kituo cha Ufuatiliaji wa Vyombo vya Habari, ambacho kilichapisha ripoti hiyo awali ikifichua kuenea kwa chuki dhidi ya Uislamu, tamaduni zenye sumu za vyumba vya habari, na athari za afya ya akili, haswa kufuatia uangaziaji wa vyombo vya habari wa vita vya "Israel" dhidi ya Gaza.
Kuripotia kuhusu mauaji ya halaiki kumeashiria nukta ya mabadiliko kwa wataalamu wengi, ambao wanazingatia matarajio yao ya kitaaluma ya baadaye ndani ya tasnia hiyo, nukuu moja inatoa mtazamo wa tatizo hapa;
"Wanawake wa Kiislamu wanaofanya kazi katika vyombo vya habari vya Uingereza hawaonekani wala hawasikiki. Wao ni muhimu katika simulizi hii, hata huku taasisi zikijaribu kuweka pembeni, kuwatenga, au kutumia uwepo wao,"
Matokeo ya utafiti yanapendekeza kwamba wakati ukongwe unatoa ushawishi fulani, vikwazo vya kitaasisi mara nyingi huwalazimisha wanawake wa Kiislamu kuendana na ajenda kuu za uhariri, aghlabu zenye chuki dhidi ya Uislamu.
Maoni:
Inafahamika sana na taasisi za kimataifa za vyombo vya habari kwamba miundo ya Magharibi ya uhuru wa kujieleza na fikra ya anuwai hutoa hifadhi kwa wanawake wa demografia zote.
Tumeona jinsi wanahabari mashuhuri wanavyozikimbia "serikali kandamizi" na kujiimarisha katika taasisi za "kidemokrasia", wakidai kwamba "mfumo wao wa kiikolojia wa Kiislamu" unahitaji kuwa huria zaidi.
Ripoti hii inatoa ushahidi wa wazi kwamba imani katika uhuru wa kujieleza na uwakilishi haina msingi kabisa na inapaswa kutupiliwa mbali. Tunaweza kuona jinsi hatua zile zile za ukandamizaji ambazo wanawake hukimbia zinapatikana sana katika mataifa ambayo yanajigamba kuwa maregeleo ya vyombo vya habari huria.
Uhalisia ni kwamba hakuna hata moja ya ardhi za Kiislamu yenye uwakilishi wowote wa jinsi ujuzi wa kifikra wa wanawake wa Kiislamu umelindwa, kwani wote wanafanywa watumwa na ajenda ya vyombo vya habari vya kimataifa dhidi ya ule ambao haswa ndio Uislamu.
Wanaadhibu kivitendo upinzani na jaribio lolote la kufichua simulizi ya udhibiti wa vibaraka wa mabwana kwamba sheria za Kiislamu zinanyamazisha na kupunguza ujuzi wa wanawake. Hii ni ili kujenga dhana kwamba miundo huria ya kidemokrasia ya Magharibi ndiyo chaguo pekee kwa maendeleo.
Elimu ya wanawake na mchango wao kwa wingi katika mazingira ya vyombo vya habari vya Dola ya Kiislamu imerekodiwa vyema kihistoria, ukweli kwamba nchi za Magharibi zinajaribu kuficha sura yao iliyopinda, iliyohaririwa pakubwa ya zamani. Hii hapa ni mifano michache tu;
• Fatima al-Fihri: Anasherehekewa kwa kuanzisha Chuo Kikuu cha Al-Qarawiyyin huko Fez, Morocco, ambacho kinatambuliwa na UNESCO kama taasisi kongwe zaidi, inayoendelea kufanya kazi duniani. Chuo kikuu hiki kilitoa masomo mbali mbali, yakiwemo yale yanayohusiana na mawasiliano na usambazaji wa elimu.
• Zaynab binti al-Kamal: Mwanachuoni huyu alijulikana kwa umahiri wake wa Hadith (maneno na matendo ya Mtume Muhammad) na kufundisha katika taasisi mashuhuri. Alikuwa mamlaka iliyoheshimiwa, na wanafunzi walisafiri kutoka mbali ili kusikiliza mihadhara yake. Kazi yake inaangazia umuhimu wa wasomi wa kike katika kuhifadhi na kusambaza elimu ya kidini.
• Umm al-Darda al-Sughra: Mtu mwingine mashuhuri ni, Umm al-Darda, alikuwa mwanafiqhi, mwanachuoni wa Hadith, na mtawa. Alijulikana kwa elimu na hekima yake, na aliwafundisha wanaume na wanawake. Ushawishi wake unaonyesha dori muhimu ambayo wanawake walicheza katika usomi wa kidini katika kipindi hicho.
• Wanawake Wengine Maarufu: Wanawake wengine wengi walichangia katika mazingira ya usomi ya wakati huo. Kwa mfano, Aisha binti Talha, Umm Salama, na Hafsa binti Sirin pia walikuwa wanazuoni mashuhuri katika nyanja mbalimbali. Wanawake hawa, pamoja na wengine, walitengeneza muundo wa kifikra na kithaqafa wa jamii za Kiislamu.
Quran ilithibitisha usemi wa wanawake na dhulma yoyote dhidi yao kwa wito wa wanaume na wanawake katika Uislamu kuelimishwa na kutafuta elimu katika Uislamu, huku mke wa Mtume (saw) Aisha (ra) akiwa miongoni mwa waliobobea zaidi, pamoja na wapokezi wa Hadith.
[يَرْفَعِ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَالَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ دَرَجَاتٍ وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ]
“Mwenyezi Mungu atawainua walio amini miongoni mwenu, na walio pewa ilimu daraja za juu. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda.” (Surah Al-Mujadila, 58:11)
Ni lazima turudi kwenye mamlaka ya Khilafah, tukiwakilisha na kulinda ujuzi wa kifikra wa wanawake wa Kiislamu ili kamwe tusitegemee hatua hizi za kirongo ili kupata haki zetu katika vyombo vya habari au maisha ya kijamii.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammad
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir