Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Machafuko ya Kisiasa nchini Tanzania ni Uso wa Unafiki wa Demokrasia

Habari:

Mnamo 10/03/2020, mahakama nchini Tanzania iliwapata na hatia na kuamua kwamba baadhi ya viongozi wakuu wa upinzani wa Chadema walipe faini au watumikie kifungo gerezani kwa mashtaka yanayohusiana na maandamano yaliyopigwa marufuku, uhaini na mashtaka mengine. Uamuzi huu ungeliwatupa gerezan lau wangelishindwa kulipa faini ya shilingi milioni 350 ($152,000) kama adhabu.

Maoni:

Kufuatia maamuzi ya mahakama licha ya tofauti zetu za kimfumo na mfumo wa kirasilimali na nidhamu yake ya kidemokrasia, bado sisi kama binadamu, tunawasikitikia viongozi wa upinzani kutokana na uamuzi huu usiokubalika na unaokandamiza wa mahakama. 

Kuhusiana na hukumu ya mahakama, Kamati ya Mahusiano ya Kigeni ya Seneti nchini Amerika, ilitoa taarifa yake ya kiunafiki ikielezea kwamba mashtaka hayo ni ghushi na kwamba yanazoretesha nafasi ya kisiasa na uhuru nchini Tanzania pamoja na juhudi za serikali kuufanya upinzani kuwa ni wahalifu na kudhoofisha uwezekano wa uchaguzi wa kidemokrasia baadaye mwakani.

Ni wazi kwamba Amerika kuisikitikia Chadema ni bandia kutokana na machafuko ya kisiasa nchini Tanzania na ni jaribio la kutaka kuishawishi, kwa kuwa ni chama kinachoegemea Ulaya, kwani imejaribu kufanya hivyo katika miaka ya karibuni na kufeli.

Suala hili linafichua wazi uongo wa demokrasia pale ambapo inapodai kwamba uhuru wa kukusanyika na kuandamana ni halali, lakini tu kwa maslahi ya watawala au chama tawala. Pia, licha ya kuwepo vitendo halali ndani ya nidhamu ya kisiasa ya vyama vingi, maamuzi yanaonekana kuimomonyoa nidhamu.

Pia kuna angalizo muhimu katika tukio hili, namna mahakama za kirasilimali zinavyokuwa na upendeleo katika utendajikazi wake, ilhali ni rahisi kwa wanasiasa wa kidemokrasia kwa kesi zao kusikizwa na kumalizika ndani ya mwaka mmoja, baadhi ya viongozi Waislamu (washukiwa) wamenyiwa dhamana, baada ya kufungwa pasi na kuhukumiwa kwa takribani miaka saba sasa, ilhali ni wazi kwamba shutuma dhidi yao ni za uongo kwa sababu ya imani yao ya Uislamu.

Tungelipenda kuwakumbusha Waislamu na wasiokuwa Waislamu mambo mawili: kushiriki katika siasa za kidemokrasia hakuna chochote kitakachopatikana isipokuwa kumwaga machozi na damu, kwa kuufanya mfumo muovu wa kirasilimali kudumu kwa ajili ya wachache kwa kutumia machungu ya wengi. Pia, nidhamu ya Kiislamu ya mahakama chini ya dola ya Khilafah itakuwa rahisi, adilifu na haitoruhusu aina yoyote ya ukandamizaji kwa Waislamu na wasiokuwa Waislamu. Mtu hatoadhibiwa, hatofungwa pasi na kuwepo ushahidi wa wazi kwamba yeye ndiye mkosaji.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Said Bitomwa
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Tanzania

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 26 Machi 2020 06:23

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu