Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ulimwengu Huru – Ambapo Ubaguzi wa Rangi ni Janga Lililo Enea

Habari:

Maandamano makali juu ya kifo cha George Floyd yamelipuka kwa siku tano mtawalia mnamo Jumamosi katika miji kote nchini Amerika, kuanzia Philadelphia hadi Los Angeles ambapo magari ya polisi yaliteketezwa moto na ripoti za majeraha kuripotiwa pande zote mbili.

Maandamano hayo, yalioanza jijini Minneapolis baada ya kifo cha Floyd mnamo Jumatatu ambapo afisa mmoja wa polisi alilifinyilia goti lake shingoni mwake (Floyd) hadi akashindwa kupumua, na kugeuka kuwa ni kadhia ya kitaifa huku waandamanaji wakishutumu miaka mingi ya unyama wa polisi dhidi ya Waamerika wenye asili ya Kiafrika. (Chanzo: gazeti la Independent 31/05/2020)

Maoni:

Huku ulimwengu ukizongwa katika hofu na machukivu kwa mauwaji ya raia mwengine wa Amerika mwenye asili ya Kiafrika, George Floyd, swali tunaloliuliza ni je, mahusiano ya rangi yanaelekea wapi kutoka hapa?

Huku unyanyasaji jumla usiokubalika unaofanywa na maafisa wa dola na majimbo nchini Amerika ukiwa ni hadithi iliyo kita mizizi ndani ya historia ovu na chungu, baadhi wanaamini kuwa nguvu ya mitandao ya kijamii inatoa mwangaza wa matumaini na kwamba uwazi zaidi na uchangamfu wa umma yatapelekea haki kutekelezwa. Zaidi ya hayo, wazo kuwa mfumo wa haki ambao ni sekta ya taaluma ya kifahari unavipa nguvu vitengo vya polisi ambazo ni sekta za taaluma za kiufundi, unaotulizia makini upelelezi wa mauwaji ya hivi karibuni ya Ahmaud Arbery na George Floyd, unatoa dhana kwa baadhi kuwa uwezekano wa kutokea kwa mapungufu katika haki utapungua.    

Siku tano zilizopita zinaelezea hadithi nyengine. Tumeona maandamano yakisambaa kuanzia Minneapolis hadi zaidi ya miji thalathini kote Amerika, yakiifananisha na maeneo ya vita. Huku watu wakitembea mabarabarani kuangazia, kwa mara nyengine tena, unyama wa kitaasisi, polisi, japo haujaripotiwa na vyombo vikuu vya habari, umechochea ghasia na majibu ya kuchukiza kupitia matumizi ya nguvu zisizo stahiki na za kupita kiasi, bali hili linathibitisha tena yale ambayo watu weusi nchini Amerika wanayapitia. 

Gavana wa Minnesota, Tim Walz, ameshindwa kushawishi, akifanya machache ili kuunganisha jimbo lake au kusimama pamoja na waandamanaji na bila ya kushangazwa Raisi Trump anaendelea kuchochea zaidi taharuki kwa kuwaita waandamanaji hao "majambazi" na hata kutumia maneno maarufu ya mbaguzi waziwazi wa rangi wa miaka ya tisiini, Mkuu wa polisi wa Miami Walter Headley, "pindi uporaji unapo anza mashambulizi ya risasi yanaanza."

Huku umma ukiwataka wanasiasa kuchukua hatua zaidi kuliko maneno matupu kwa kadhia ya ubaguzi wa rangi nchini Amerika, watu weusi wanalijua vizuri mno janga na umbile la maadili haya ya kitaasisi yaliyo oza. Dkt. Cornel West aliangazia hili katika mahojiano yake na Anderson Cooper katika runinga ya CNN, ambapo alitaja, 'Tumezijaribu nyuso nyeusi katika nyadhifa za juu,' na kusonga mbele na kuangazia namna gani wawakilishi kutoka katika jamii za walio wachache wanajisalimisha pakubwa katika nidhamu fisidifu ambapo pasi na budi wanakuwa ni sehemu yake. Shutma hizi za sasa kwa taasisi za dola zinaandamana na matarajio ya kimakosa kwa watu mithili ya Mkuu wa Sheria Keith Ellison, ingawa ukweli unao kodoa macho ni kuwa hakuna matarajio ya mabadiliko yoyote ya kimsingi.

Hii ni kwa sababu taasisi rasmi na zisizo rasmi ambazo zimeuunda na sasa zinaudhibiti mujtamaa wa Kiamerika zinafanya uondoaji wa mitazamo ya ubaguzi wa rangi inayo bebwa na, bila shaka, idadi kubwa ya Waamerika, kuwa vigumu kwa usiku mmoja.

Hatimaye, ni nidhamu iliyo jengwa juu ya Urasilimali iliyo chochea tofauti za hali ya juu na kudunisha utukufu wa uhai wa mwanadamu, kupitia kutokuwa na tofauti kwake katika unyanyasaji na janga la uhaba katika mataifa yaliyo endelea ya kimagharibi pamoja na kusini mwa ulimwengu. Kuenea kwa ubaguzi unaowakumba Waafrika-Waamerika katika makao na ajira pamoja na dhana ya watu kupewa madaraka kutokana na uwezo wao yamewaacha milioni 40 (asilimia 13 ya idadi ya watu) ndani ya umasikini mkubwa.

Uislamu unaangazia juu ya ugavi wa mali na kuondoa umakinifu na ukwamiaji wa rasilimali kupitia aina yoyote ya mapendeleo au usimamizi mbaya wa serikali. Nidhamu ya kiuchumi ya Kiislamu, ambayo imejengwa juu ya Qur'an na Sunnah ina asisi nidhamu ya kisheria iliyo na uwajibikaji na uwazi ambayo huitikia mahitaji ya raia sio tu kwa msingi wa mahitajio yao pekee bali pia majukumu yao. وَلاَ تُؤْتُواْ السُّفَهَاء أَمْوَالَكُمُ الَّتِي جَعَلَ اللّهُ لَكُمْ قِيَاماً وَارْزُقُوهُمْ فِيهَا وَاكْسُوهُمْ﴿ “Wala msiwape wasio na akili mali yenu ambayo Mwenyezi Mungu ameyajaalia yawe ni kiamu yenu. Walisheni katika hayo na muwavike,” [An Nisaa: 5]

Hivyo basi, Uislamu unaasisi haki baina ya watu wa jamii, dini na jinsia zote. Kiujumla inakubalika kwamba, katika Uislamu, fungamano baina ya raia na dola limejengwa juu ya fahamu ya udugu na haliathiriwi na aina yoyote ya ukabila, utaifa au ubaguzi wa rangi. Aina hizi ya 'isms' ni zenye kuleta mgawanyiko na kupelekea matukio ya kusikitisha tuliyoyashuhudia nchi Amerika sio tu katika wiki hii moja iliyo pita pekee bali kwa karne nyingi. Uislamu huwatazama raia kwa upande wa kibinadamu na hivyo usawa unampa kila mtu haki ya chakula, makao na mavazi na la muhimu zaidi unathamini utukufu wa uhai wenyewe. 

وَمَنْ أَحْيَاهَا فَكَأَنَّمَا أَحْيَا النَّاسَ جَمِيعًا﴿

“Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote.” [Al Maidah: 32]

Hivi ndivyo Uislamu unavyo tufunza.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) atutoe kutoka kwenye giza la mifumo mibovu hadi kwenye nuru ya mfumo Wake mtukufu, ili tuweze kuona mwisho wa dhulma ya sheria za kibinadamu inayo tekelezwa na mwanadamu mwengine. Ameen

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Maleeha Hasan

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumamosi, 06 Juni 2020 21:30

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu