Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya Habari 02/06/2021

Vichwa vya Habari:

  • Uingereza Yaipa Mafunzo PLO katika Ukingo wa Magharibi
  • Mazayuni Wahitaji Msaada wa Kijeshi

Maelezo:

Uingereza Yaipa Mafunzo PLO katika Ukingo wa Magharibi

Uingereza inatumia mamilioni ya pauni katika mradi wa kuisaidia Ukingo wa Magharibi uliokaliwa kimabavu na ‘Israeli’ ili kuimarisha “uwezo zaidi” wa vikosi vya usalama vya Palestina ambavyo vinaweza kuzuia uwezekano wowote wa kutokea machufuko au ghasia kwa Israel”. Kulingana na taarifa za siri ni kwamba mradi  huo unalenga—kujenga uwezo, uwajibikaji, uiamara na mradi jumuishi— kutoa usaidizi kwa vikosi vya ndani vya usalama vya mamlaka ya Palestina (PA), serikali ya muda katika eneo la Ukingo wa Magharibi  ilioundwa mwaka 1994 kama  sehemu ya mkataba wa Oslo. Iligharimu pauni milioni 3.3-mwaka uliopita. Israel iliandika hayo huku ikiendelea na mpango wa kuwafukuza Wapalestina katika eneo la Jerusalem na hatua ya kijeshi ya ‘Israeli’ katika eneo la Gaza, “Ukingo wa Magharibi unatarajiwa kuona maandamano makubwa. Moja ya sababu ni ushirikiano wa Israeli na Mamlaka ya Palestina, kwani pande zote mbili zinafanya kazi kwa bidii ili kutuliza hali.” PLO kwa muda mrefu imekuwa ni sehemu ya tatizo badala ya suluhu. Muungano huo umekubaliana mpango wa serikali mbili muda mrefu uliopita, bila kujali mwelekeo mbaya uliokuwa nao PLO imekuwa ni msaada mkubwa kwa Mazayuni badala ya kuwakilisha matakwa ya watu wa Palestina.

Mazayuni Wahitaji Msaada wa Kijeshi

Baada ya kampeni ya siku 11-ya kupiga mabomu Gaza ambayo iliua wapalestina 256, ikiwa ni pamoja na watoto 67, ‘Israeli’ inaomba kwa washirika wake ziada ya msaada wa kijeshi wa dolari bilioni 1 “za dharura”, juu ya dolari bilioni 3.8 ambazo Washington imekuwa ikiipa kila mwaka. Seneta Lindsey Graham (R-SC) alithibitisha kwamba  ‘Israeli’ ilifanya ombi hilo siku moja baada ya yeye kukutana na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu katika mji wa Jerusalem. “kutakuwa na ombi litakalotolewa na Israeli kwenda Pentagon siku ya Jumatano la msaada wa dolari bilioni 1 kwa ajili ya kuimarisha mtambo wa  Iron Dome batteries,” Graham  aliiambia Fox na Friends mnamo siku ya Jumanne. Umbile la Kizayuni ni umbo bandia ambalo baada ya mashabulizi kidogo tu limeshaishiwa silaha na kukimbilia Amerika kuomba kuongezewa. Katika mzozo wowote na nchi au jeshi jirani linaloizunguka Israel itashindwa vibaya. Ikipenda inaweza kuegemea msaada wa Amerika, inapaswa kutazama namna ambavyo Taliban iliyafanya majeshi ya Amerika nchini Afghanistan.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu