- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Uhakiki wa Habari 20/12/2023
Marekani Yazindua Rasmi Operesheni ya Kijeshi katika Bahari Nyekundu
Marekani imetangaza rasmi uzinduzi wa operesheni mpya ya kijeshi katika Bahari Nyekundu inayolenga kujibu mashambulizi ya Mahouthi wa Yemen kwa meli za kibiashara ambayo yalianza kwa kujibu shambulizi la umbile la Kiyahudi huko Gaza. Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin alitangaza mpango huo, unaoitwa Operesheni ya Ustawi wa Ulinzi, alipokuwa safarini kuelekea eneo hilo na akasema nchi zingine zinazoshiriki ni pamoja na Uingereza, Bahrain, Canada, Ufaransa, Italia, Uholanzi, Norway, Ushelisheli, na Uhispania. Mashambulio ya Houthi yamelazimisha baadhi ya meli kubwa zaidi za kiulimwengu kusitisha safari kupitia Bahari Nyekundu, ambapo inahatarisha athari kubwa kwa uchumi wa dunia. Mahouthi, waliojulikana kama Ansar Allah, wameapa kulenga meli zote zinazoelekea na kutoka 'Israel' na wakasema njia pekee ya "kuregesha utulivu" kwa eneo hilo ni kupitia usitishaji mapigano wa kudumu huko Gaza. Mahouthi hawajaonyesha ishara ya kuachana na hili na kutangaza mnamo Jumatatu kuwa wamefanya mashambulizi mawili ya droni kwenye meli za kibiashara. Bloomberg iliripoti kwamba Saudi Arabia na Imarati zimegawanyika juu ya jinsi Marekani inapaswa kujibu. Imarati inataka hatua za kijeshi na kwa Marekani kuwaorodhesha upya Mahouthi kama "shirika la kigeni kigaidi," ambapo itafanya utekelezaji wa mpango wa amani wa Yemen kutowezekana.
Rais el-Sisi Atangazwa Mshindi katika Uchaguzi wa Misri
Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sisi amepata muhula wa tatu kama kiongozi wa taifa lenye watu wengi la Mashariki ya Kati baada ya kuhesabiwa kura katika uchaguzi uliofanyika kati ya Disemba 10 na 12 kukamilika. Sisi alishinda asilimia 89.6 ya kura, Mamlaka ya Uchaguzi ya Kitaifa ilisema. Licha ya shida za Misri, ukandamizaji wa muongo mmoja wa wapinzani umeondoa upinzani wowote mkubwa kwa Sisi. Sisi alikuwa akigombea dhidi ya wagombea wengine watatu, hakuna hata mmoja wao aliyekuwa mashuhuri. Mgombea mashuhuri zaidi alisitisha ugombezi wake akilalamika kwamba kampeni yake ilikuwa imeingiliwa na wafuasi wake kadhaa kukamatwa. Sisi alirefusha muhula wa mamlaka ya rais kutoka miaka minne hadi sita na kurekebisha katiba ili kuongeza kikomo kwa mihula mfululizo katika afisi kutoka miwili hadi mitatu. Chini ya utawala wake, Misri imewafunga maelfu ya wafungwa wa kisiasa, na huku kamati ya msamaha wa rais ikiwaachilia huru karibu 1,000 katika mwaka mmoja, makundi ya kutetea haki yanasema kwamba watu wengi mara tatu hadi nne ya hao walikamatwa kwa kipindi hicho hicho.