Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya Habari 3/4/2020

Vichwa vya habari:

Virusi vya Korona: Virusi vya Korona ni Janga Mbaya Zaidi la Kiulimwengu tangu Vita vya Pili vya Dunia, asema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Wema wa Wapakistani katika Kupambana na Covid-19 

Virusi vya Korona: Hasira Zaongezeka juu ya Jaribio la Wazi la China Kuficha kuhusu Virusi vya Korona

Maelezo:

Virusi vya Korona: Virusi vya Korona ni Mzozo Mbaya zaidi wa Kidunia tangu Vita vya Pili vya Dunia, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Janga la virusi vya korona ndio janga mbaya zaidi la kiulimwengu tangu Vita vya Pili vya Dunia, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa - Antonio Guterres alisema siku ya Jumanne, akieleza namna janga hilo litakavyochochea mizozo duniani kote. Guterres alisema kwamba uzito wa janga hili limesababishwa na "ugonjwa ambao umekuwa ni tisho kwa kila mtu duniani na …athari ya kiuchumi ambayo itapelekea mgando wa uchumi kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa kabla." "Mkusanyiko wa mambo hayo mawili pamoja ni hatari na vinachangia hali ya kutokuwa na utulivu, machafuko na mizozo ambayo ni mambo yanayo tufanya tuamini kwamba hili ni janga kubwa kuwahi kupambana nalo tangu Vita vya Pili vya dunia”, aliwaambia waandishi wa habari. Umoja wa Mataifa – ulio na makao yake jijini New York ulianzishwa mwishoni mwa vita mnamo 1945 na una nchi wanachama 193. "Jibu la nguvu na makini... linawezekana kupitia mshikamano kama watu watakuwa kitu kimoja na kama tukiweka kando michezo ya kisiasa na kufahamu kuwa mwanadamu ndio wako hatarini," Guterres aliongeza. Kufikia sasa zaidi ya watu 40,000 wamefariki kwa kusambaa kwa ugonjwa huu kote duniani, na kusababisha madhara makubwa ya kiuchumi. "Bado hatujakuwa na mfuko wa kiulimwengu wa kuzisaidia nchi zinazo endelea ili kuweka dhurufu za kuuangamiza ugonjwa na kuondoa athari zake kubwa," Guterres alionya, akiashiria ukosefu wa ajira, kuanguka kwa biashara ndogo ndogo, na hatari ya watu kuingia katika shughuli za kiuchumi zisizo rasmi. "Tunakwenda taratibu sana kwenye muelekeo mzuri, lakini tunahitajika kuongeza kasi, na tunahitajika kufanya bidii zaidi ikiwa tunataka kuvishinda virusi hivi." Siku ya Jumanne, Umoja wa Mataifa ulianzisha hazina maalumu ili kuzisaidia nchi zinazo endelea baada ya wiki iliyopita kuomba michango kwa ajili ya mataifa masikini yaliyo kumbwa na mizozo. Mbali na misaada iliyo zoeleka kutoka kwa nchi tajiri "Tunahitaji kuwa na taasisi za kifedha zenye ubunifu ili nchi zinazo endelea ziweze kupambana na janga hili", Guterres alisema. Alionya kwamba athari za virusi vya Korona zitarudi tena kutoka nchi masikini, hasa Afrika, na kushambulia tena nchi tajiri, na hivyo mamilioni huenda wakafariki. [Chanzo: Khaleej Times]

Tangu kuundwa kwa Umoja wa mnamo 1945, uwashirikiano wa kiulimwengu daima umekuwa haba, hasa inapo kuja katika kutatua kadhia kubwa za kiulimwengu kama kusambaa kwa silaha za nyuklia, mabadiliko ya hali ya hewa na majanga. Muitikio duni dhidi ya virusi vya Korona, ni ishara ya wazi kwamba nidhamu jumla (Umoja wa Mataifa) iliyo undwa baada ya vita imefeli, na kwamba nidhamu mpya yatarajiwa kuchomoza.

Wema wa Wapikistani katika Kupambana na Virusi vya Korona 

Nje ya maduka katika mji wa Karachi, kuna tukio kubwa la kihistoria lilitokea wiki mbili zilizopita. Badala ya kuwahi majumbani baada ya kufanya ununuzi ili kuepuka maambukizi ya Korona, Wapakistani wengi wamekuwa wakikaa nje kwa ajili ya kutoa misaada ya chakula, pesa au misaada mengine kwa watu wasiokuwa na makaazi mitaani. Wema huu wa watoaji huambatana na ombi kwa anaye pokea msaada huo: “Omba janga hili [la maradhi ya virusi vya Korona] liishe haraka”. Kama ilivyo kwa mataifa mengine, Pakistan imeweka juhudi za dhati katika kupambana na janga hili la kidunia la virusi vya Korona, ikiwa ni pamoja na kufunga shule, kuzuia mikusanyiko na kufunga maduka yote ambayo hayauzi vyakula na madawa. Lakini ni tofauti na baadhi ya mataifa ambayo nayo yameweka vizuizi kama hivyo, athari za kufunga shughuli zote imepelekea uchumi kuwa mbaya zaidi – na athari kubwa zaidi. Hivi karibuni Waziri Mkuu wa Pakistani Imran Khan alihutubia taifa kuhusu virusi vya Korona, alisema “asilimia 25 ya Wapakistani hawana uwezo wa kupata milo miwili kwa siku.” Huku nchi hii ikiweka hatua kali za kutotoka nje na kuwalazimisha watu kubaki majumba mwao, watu wengi kama wale wanaotegemea shughuli za kupata kipato kwa siku – kuanzia wauza vyakula hadi washona viatu – mpaka hivi sasa hawajapata hata rupia moja kwa wiki hii, na wanaathirika kwa njaa. Huku wakiwa wamezungukwa na janga la Korona, Wapakistani wanaungana pamoja kupambana katika njia ya kuigwa. Hasa wengi wao wanatoa zaka, kujitolea misaada ya khiyari, kuwapa wale ambao hutegemea shughuli za kila siku kujipatia kipato, wasiokuwa na bima za afya au wasiokuwa na msaada wowote wa kifedha.  Huku wengi kote duniani wakiwa wanaangazia usafi wa kimwili wakati huu wa mkurupuko wa virusi vya Korona, Dkt Imtiaz Ahmed Khan, mwana Baolojia kutoka Chuo Kikuu cha Hamdard katika mji wa Karachi, amefananisha zaka na usafishaji wa kiroho, akinukuu msemo maarufu wa Pakistani, “Paisa haath ki meil hai” (pesa ni kama uchafu katika mikono ya mtu). “zaka inaondoa uchafu katika mali,” Dr Khan aliongezea. “Nitawajibika ikiwa jirani yangu yeyote atalala akiwa ana njaa. Vipi niweke ziada ya akiba ya chakula wakati jirani yangu anahitajia?” Ripoti kutoka kwa shiriki la Stanford Social Innovation Review, inasema Pakistan inachangia zaidi ya asilimia 1 ya pato lake la ndani katika msaada, ikiorodheshwa mwa nchi ambazo ni "tajiri zaidi kama Uingereza ambayo inachangia asilimia 1.3 na Canada asilimia 1.2 zaidi ya mara mbili ya kile India inachotoa katika pato lake la ndani.” Uchunguzi uliofanywa nchi nzima umeonyesha kwamba asilimia 98 ya Wapakistani wamekuwa wakitoa msaada pamoja na kujitolea muda wao – idadi inayo zidi kiwango cha wale watu wanaotakiwa kisheria kutoa zaka. “Kama nchi, tunaweza tukawa hatuna kikubwa, lakini tuna mioyo mikubwa”, alisema M Sohail Khan, Mpakistani anaeishi Loughborough, Uingereza. “Tembelea kijiji chochote na watakupa makazi; kuwajali wengine ndio utamaduni wetu. Tumeona mateso. Tuna huruma sana. Inahitajika kusambaza elimu kuwahamasisha watu kwamba kujiweka mbali na mikusanyiko ya kijamii haimaanishi kuwatelekeza majirani zako.” Kadiri virusi vya Korona vinavyo sambaa, Wapakistani wamekuwa wakitoa zaidi ya zaka inayo hitajika kwa kiwango cha asilimia 2.5, wakati huo huo wale ambao hawana uwezo wa kutoa zaka wamekuwa wakijitolea kwa namna mbali mbali. [Chanzo:  BBC]

Kuna kheri ya kweli katika Ummah wa Muhammad (saw). Mtu anaweza kutafakari, ni vipi Dola ya Khilafah itaweza kutumia kwa busara rasilimali sio tu kuwakomboa Waislamu katika umasikini wa kulazimishiwa, bali pia kuonyesha mfano usio pingika wa namna ya kuutokomeza umasikini wa kiulimwengu, jambo ambalo Wagharibi wamebakia kupiga domo tupu.

Virusi vya Korona: Hasira Zaongezeka juu ya Jaribio la Wazi la China Kuficha kuhusu Virusi vya Korona

Kulingana na ripoti za mwisho wa wiki hii, serikali ya Uingereza imekuwa ikisema upo uwezekano China ikawa imedanganya kuhusu kiwango cha mlipuko wao wenyewe kwa sababu zaidi ya 40. Muda mzuri wa nchi nyingi kujiandaa kupambana na virusi hivyo ulishapita na wakati walipoanza, zinaonekana kutegemea takwimu na taarifa za udanganyifu. Serikali ya China inaonyesha kujiingiza katika mtindo wa Urusi wa kampeni ya kutotoa taarifa. Waziri wake wa Mambo ya Nje ameandika katika mtandao wa twitter kwamba upo uwezekano "Jeshi la Amerika limeleta virusi hivyo katika mji wa Wuhan". Kupitia mdomo wake wa mtandaoni, the Global Times, limeripoti kwamba Italia inapaswa kulaumiwa, bila kutaja ushahidi wowote wa madai hayo ya kutowajibika. China sasa inakabiliwa na janga la mahusiano ya umma ambalo linaweza kuendelea kukua. Mataifa ya Kimagharibi yameweka zuio la kutotoka nje, chumi zao zimeganda au zinaanguka, na nchi ambayo inadhaniwa kuwa ndio chanzo cha tatizo imekuwa ikidanganya, kuficha na kusambaza taarifa zinazo onyesha kutokuhusika na tatizo. Hili haliwezi kusaidia kwani hata ile misaada ya kitabibu iliyotumwa na China kwenda katika nchi za Kimagharibi kusaidia katika vita vya kupambana na janga hili imekataliwa kwa kuwa ni ya viwango duni na ni hatari kwa matumizi. Uingereza, kunaripotiwa kuongezeka kwa hasira kuhusu serikali ya China kuongeza shinikizo katika uhusiano wa kibiashara. Hasira za chini kwa chini zinaweza kupelekea kufikiria upya uamuzi wa serikali wenye utata wa kuruhusu kampuni ya mawasiliano ya Huawei an, albeit dori ya kutengeneza mtandao wa 5G wa Uingereza. Nchini Amerika, utawala wa Trump haukupoteza muda, ukaitumia China kama chambo katika mgogoro unao hatarisha kuchaguliwa kwake tena katika uchaguzi ujao. Timu ya Donald Trump inaweza kukwepa uwajibikaji wake lakini maafisa wake wamekuwa washupavu linapokuja suala la virusi vya Korona  wamekuwa wakiviita virusi hivyo kwa jina la Wuhan au virusi vya  China ambako timu hiyo inaona ndiko vilikoanza. Wakati idadi ya vifo inaendelea kuongezeka, itabaki kuwa ni mkakati wa kuelekea katika uchaguzi wa Novemba. Dunia inahitaji nchi hizi kubwa mbili kufanya kazi pamoja ili kupambana na janga hili. Kuna ishara ndogo ya hilo kutokea kwa muda huu. [Chanzo: Sky News]

China pamoja na Magharibi zinapaswa kulaumiwa kwa kusambaa kwa kasi janga hili la virusi vya Korona. Jambo sawa baina yao wote ni hatua za mwendo wa kobe zilizo chukuliwa katika kupambana na virusi hivi katika jamii zao. Zaidi ya hayo, virusi vya Korona vimeonyesha udhaifu mkubwa wa mfumo wa fedha wa kiulimwengu katika kushughulikia janga hili lililopo.

 #Covid19    #Korona    كورونا#

 

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatano, 15 Aprili 2020 12:01

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu