Jumatano, 11 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/13
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Silsila ya Maswali Yaliyowasilishwa kwa

Amiri wa Hizb ut Tahrir

Sheikh Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah katika Ukurasa Wake wa Facebook

Jibu la Swali
Tofauti Kati ya Manabii na Mitume, Amani Iwe Juu Yao
Kwa: Om Qutibah Odah
(Imetafsiriwa)

Swali:

Assalam Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh

Katika kitabu, Shakhsiya ya Kiislamu, sehemu ya kwanza ya sura ya Manabii na Mitume, ukurasa wa 130, inasema:

“Kwa hivyo, Musa (as) alikuwa Nabii kwa sababu alipewa wahyi na Shari’ah na Mtume kwa sababu Shari’ah hii ilikuwa kwa ajili ya utume wake. Kwa upande mwingine, ingawa Harun (as) pia alikuwa ni Nabii kwa sababu alipewa wahyi na Shari ́ah, hakuwa Mtume kwa sababu Shari ́ah iliyoteremshwa kwake haikuwa kwa ajili ya utume wake, bali ilikuwa kwa ajili ya utume wa Musa (as)”.

Tutaunganisha vipi baina ya yale yaliyotajwa katika kitabu, Shakhsiya ya Kiislamu, na yale yaliyothubutu katika Kitabu (Qur’an) pindi Mwenyezi Mungu (swt) anaposema: فَأْتِيَاهُ فَقُولا إِنَّا رَسُولا رَبِّكَ]  “Basi mwendeeni, na mwambieni: Hakika sisi ni Mitume wa Mola wako Mlezi!” [Ta-Ha: 47] [فَأْتِيَا فِرْعَوْنَ فَقُولا إِنَّا رَسُولُ رَبِّ الْعَالَمِينَ] “Basi mfikieni Firauni na mwambieni: Hakika sisi ni Mitume wa Mola Mlezi wa walimwengu wote.” [Ash-Shu’ara: 16] Katika tafsiri zote yeye ni Mtume na Nabii.

Jibu:

Wa Alaikum Assalam Wa Rahmatullah Wa Barakatuh

Kwanza: Kumekuwa na ikhtilafu baina ya wanazuoni kuhusiana na tafauti baina ya Nabii na Mtume katika kauli kadhaa, zikiwemo:

1- Nabii ni yule anayeteremshiwa kazi (taklif) na wala haamrishwi kuifikisha. Akiamrishwa kuifikisha basi ni Mtume. Imeelezwa katika Fath Al-Bari na Ibn Hajar Al-Asqalani: [Fath Al-Bari cha Ibn Hajar (11/112)

Neno ‘Unabii’ na ‘Ujumbe’ ni tofauti kiasili. Unabii unatokana na naba’ (julisha), ambayo ni habari. Nabii katika desturi za kawaida ni yule aliyepewa habari na Mwenyezi Mungu kwa amri inayohitajia kazi, lakini akiamrishwa kuifikisha kwa wengine, basi yeye ni Mtume; vyenginevyo, yeye ni Nabii si Mtume. Na kwa kuzingatia hili, kila Mtume ni Nabii lakini sio kinyume chake. Nabii na Mtume wanashiriki jambo la jumla ambalo ni habari (naba'), na wametengana katika ujumbe, hivyo ukisema fulani na fulani ni Mtume, unamaanisha kuwa yeye ni Nabii na Mtume. Ukisema fulani na fulani ni Nabii, basi haimaanishi kuwa yeye ni Mtume...]

2- Mtume ni yule aliyetumwa kufikisha wahyi na kwake kuna Kitabu, na Nabii ni yule aliyetumwa kufikisha wahyi kwa ujumla. Al-Ainy ametaja yafuatayo katika “Al-Banaya Sharh Al-Hidaya”: [Al-Banaya Sharh Al-Hidaya (1/116) [...Basi tafauti baina ya Mtume na Nabii: Mtume: ni yule aliyetumwa kufikisha wahyi na kwake kuna Kitabu, na Nabii ni yule aliyetumwa kufikisha wahyi kwa ujumla, sawa ilikuwa pamoja na Kitabu au bila Kitabu, kama Yoshua, amani iwe juu yake, kwa hivyo Nabii ni mkuu kuliko Mtume. Hivi ndivyo alivyosema Sheikh Qawam al-Din al-Atrazi katika “Sharh” yake, na katika hilo alimfuata mtunzi wa “Al-Nihaayah” pale aliposema: Mtume: ni Nabii ambaye ana Kitabu pamoja naye, kama Musa (as), na Mtume: ni mwenye khabari za Mwenyezi Mungu, hata kama hana Kitabu, kama Yoshua, amani iwe juu yake. Mtume (saw) amesema: «عُلَمَاءُ أُمَّتِي كَأَنْبِيَاءِ بَنِي إِسْرَائِيلَ» “Wanachuoni wa Ummah wangu ni kama Manabii wa wana wa Israili,” wala hakusema: “Mitume wa Israili.” Sheikh Akmal al-Din, Mwenyezi Mungu amrehemu, akawafuata na akawapambanua hivi].

3- (Mtume ni yule aliyeteremshiwa Shariah na ameamrishwa kuifikisha, huku Nabii ni yule aliyeteremshiwa Shariah ya Mitume wengine na ameamrishwa kuifikisha. Mtume ni yule mwenye kuamrishwa kufikisha Shariah iliyoteremshwa kwake, na Nabii ni yule aliyeamrishwa kufikisha Shariah za wengine), na hii ndiyo rai tuliyoichagua na kuibainisha katika kitabu “Shakhsiya ya Kiislamu”, juzuu ya 1, ukurasa wa 35-38 nakala ya Word:

[Manabii na Mitume: Nabii na ‘Mtume’ (rasul) ni maneno mawili yanayotofautiana lakini yanashirikiana katika upande kwamba Sharia inateremshwa kwa wote wawili. Tofauti kati ya Mtume na Nabii ni kwamba wa kwanza amepewa wahyi kwa Shari’ah ambayo ameamrishwa kuieneza, huku wa pili, yaani Nabii, pia amepewa wahyi, lakini ameamrishwa kueneza Shari’ah ya Mitume. Kwa maana nyengine, Mtume ameamrishwa kueneza Shari’ah yeye mwenyewe, huku Nabii anaeneza Shari’ah ya Mitume. Qadi al-Baydawi katika ufafanuzi wa kauli ya Mwenyezi Mungu (swt),  [وَمَا أَرْسَلْنَا مِنْ قَبْلِكَ مِنْ رَسُولٍ وَلَا نَبِيّ]  “Na hatukumtuma kabla yako Mtume wala Nabii,” [Hajj: 52]; Mtume ametumwa na Mwenyezi Mungu (swt) akiwa na sharia iliyorudiwa tena au mpya ambayo anawalingania watu, huku Nabii ametumwa na Mwenyezi Mungu (swt) kuthibitisha sharia ya iliyopita.” Hivyo, Musa (as) alikuwa Nabii kwa sababu alipewa wahyi kwa Shari ́ah na ni Mtume kwa sababu Shari ́ah hii ilikuwa kwa ajili ya utume wake. Kwa upande mwingine, ingawa Harun (as) pia alikuwa Nabii kwa sababu alipewa wahyi na Shari’ah, hakuwa Mtume kwa sababu Shari’ah, iliyoteremshwa kwake, haikuwa kwa ajili ya utume wake; bali ilikuwa ni kwa ajili ya utume wa Musa (as). Kwa mantiki hiyo hiyo, Muhammad (saw) alikuwa Nabii na Mtume kwa sababu alipewa wahyi na Shari’ah, ambayo ilikuwa kwa ajili ya utume wake]. Mwisho wa nukuu.

Rai hii ndiyo sahihi zaidi ya maneno na ndiyo inayowezekana zaidi kuwa sahihi. Hadith za Mtume (saw) zinaeleza uhalisia wa Nabii na tofauti kati yake na Mtume. Kwa mfano, Hadith iliyopokewa na Bukhari na Muslim kutoka kwa Abu Hazim, alisema: Nilikaa na Abu Huraira miaka mitano, basi nikamsikia akisema kuwa Mtume amesema.

«كَانَتْ بَنُو إِسْرَائِيلَ تَسُوسُهُمْ الْأَنْبِيَاءُ كُلَّمَا هَلَكَ نَبِيٌّ خَلَفَهُ نَبِيٌّ، وَإِنَّهُ لَا نَبِيَّ بَعْدِي، وَسَيَكُونُ خُلَفَاءُ فَيَكْثُرُونَ. قَالُوا: فَمَا تَأْمُرُنَا؟ قَالَ: فُوا بِبَيْعَةِ الْأَوَّلِ فَالْأَوَّلِ؛ أَعْطُوهُمْ حَقَّهُمْ فَإِنَّ اللَّهَ سَائِلُهُمْ عَمَّا اسْتَرْعَاهُمْ»

“Walikuwa wana wa Isra’il siasa zao zikiendeshwa na Manabii, kila Nabii alipokufa alirithiwa na Nabii mwengine. Na hakika yake hakutakuwa na Nabii mwengine baada yangu, lakini watakuwepo makhalifa na watakuwa wengi.” Akaulizwa watuamrisha nini? Akasema, “Mpeni ahadi ya utiifu (Bay’ah) mmoja baada ya mmoja; na wapeni haki yao kwani Mwenyezi Mungu atawauliza yale aliyowapa uchungaji kwayo.”

Ni wazi kutokana na Hadith hii kwamba Manabii wa Wana wa Israil ndio waliokuwa wakiwatawala, na hilo lilikuwa ni kwa mujibu wa Shariah ya Musa (as) kama inavyojulikana na inavyoonyeshwa na Hadith yenyewe, kwani inafananisha maumbile ya kazi ya makhalifa kwa kazi ya Manabii wa wana wa Israili, yaani, katika masuala ya utawala wa watu. Kama vile Manabii wa Wana wa Israili walivyokuwa wakiwatawala watu kwa mujibu wa Shariah ya Musa (as), ndivyo walivyo makhalifa; pia wanatawala Waislamu kwa mujibu wa Shariah ya Muhammad (saw). Hii ina maana kwamba Manabii wa wana wa Israili hawakuja na Shariah mpya, bali walifuata Shariah ya Musa (as). Hadith hii inaashiria kuwa Nabii ndiye anayepokea wahyi na kuwafahamisha watu juu yake, lakini hawajulishi sharia mpya; bali anafikisha Shariah ya Mtume aliyetangulia. Na kutokana na hilo pia inafahamika kwamba Mtume ndiye anayeleta Shariah mpya ambayo Manabii wanaomfuata wanaweza kuifuata, kama ilivyo kwa Manabii wa Wana wa Israili kuhusiana na Musa (as). Hadith iliyotajwa hapo juu ni ushahidi wa uhalisia wa tofauti kati ya Nabii na Mtume.

Pili: Uhalisia wa Bwana wetu Harun (as):

1- Kama tulivyotaja katika andiko lililonukuliwa hapo juu kutoka katika kitabu, Shakhsiya ya Kiislamu, tulisema: [Hivyo, Musa (as) alikuwa Nabii kwa sababu alipewa wahyi kwa Shari'ah na Mtume kwa sababu Shari'ah hii ilikuwa kwa ajili ya utume wake. Kwa upande mwingine, ingawa Harun (as) pia alikuwa Nabii kwa sababu alipewa wahyi na Shari’ah, hakuwa Mtume kwa sababu Shari’ah, iliyoteremshwa kwake, haikuwa kwa ajili ya utume wake; bali ilikuwa ni kwa ajili ya utume wa Musa (as)]. Kwa hiyo kwa kuzingatia ufafanuzi unaoelekea kuwa sahihi zaidi kwetu wa Nabii na Mtume, tumeamua kwamba Harun (as), ni Nabii na sio Mtume kwa maana hii, kwa sababu Harun (as), alikuwa akimfuata Musa (as) katika Shariah, na maandiko ya Shariah yanashuhudia hilo kama inavyoonyeshwa hapo chini.

2- Kuhusiana na aya mbili tukufu ulizozitaja katika swali, hebu tuziangalie tafsiri yake kwa ufupi kutoka katika baadhi ya vitabu vya tafsiri:

a- [Tafsir al-Nasafi (2/297, iliyohesabiwa moja kwa moja na al-Shamilah)

[فَأْتِيَاهُ]  “Basi mwendeeni” yaani, kwa Firauni,[فَقُولا إِنَّا رَسُولاَ رَبّكَ]  “na mwambieni: Hakika sisi ni Mitume wa Mola wako Mlezi” kwako wewe. Basi, wakenda kwake na kumfikishia Ujumbe na wakamwambia wameamrishwa kufanya hivyo.

[قَالَ فَمَن رَّبُّكُمَا يا موسى]  “(Firauni) akasema: Basi Mola wenu Mlezi ni nani, ewe Musa?” Aliwahutubia, kisha akamwita mmoja wao, kwa sababu Musa ndiye mwenye asili ya utume, na Harun akamfuata...].

Imekuja pia katika [Tafsir al-Nasafi (2/ 464, iliyohesabiwa moja kwa moja na al-Shamilah)

[فَأْتِيَا فِرْعَوْنَ فَقُولا إِنَّا رَسُولُ رَبِّ الْعَالَمِينَ]  “Basi mfikieni Firauni na mwambieni: Hakika sisi ni Mitume wa Mola Mlezi wa walimwengu wote.” Mtume haikutumika muundo wa mbili (tathniya) kama ilivyo katika aya: [إِنَّا رَسُولاَ رَبّكَ]  “Hakika sisi ni Mitume wa Mola wako Mlezi”

Kwa sababu Mtume inaweza kumaanisha yule aliyetumwa na inaweza kumaanisha Ujumbe, hivyo wakati mwingine ni katika maana ya yule anayetumwa, kwa hivyo hakuna haja ya kuzifanya katika muundo wa tathniya (mbili). Hapa ni katika maana ya Ujumbe; kwa hiyo, ni sawa katika maelezo ya moja, mbili au wingi. Au kwa sababu wameungana na kuafikiana katika Shariah moja kana kwamba wao ni Mtume mmoja. Au nataka kila mmoja wetu [أَنْ أَرْسِلْ] “atume” maana ya kutuma, ili Mtume ajumuishe maana ya kutuma na iwe na maana ya usemi [مَعَنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ] “Pamoja nasi wana wa Israail”. Anamaanisha kuwaacha waende nasi Palestina na yalikuwa makaazi yao. Basi wakaja mlangoni kwake, ruhusa haikutolewa kwa muda wa mwaka mmoja, mpaka mlinzi wa mlango akasema: Kuna mtu hapa anayedai kuwa ni Mtume wa Mola Mlezi wa walimwengu wote. Akasema: Mruhusu ili tumcheke. Basi wakampa Ujumbe, na Firauni akamjua Musa...]

b- [Tafsir Al-Qurtubi (13/93) kauli ya Mwenyezi Mungu (swt): [فَأْتِيَا فِرْعَوْنَ فَقُولا إِنَّا رَسُولُ رَبِّ الْعَالَمِينَ] “Nendeni kwa Firi’aun na mkamwambie: ‘Tuna ujumbe wa Mola Mlezi wa walimwengu wote.” Abu Ubaidah akasema: Mtume anaweza kuwa katika maana zote mbili maana ya uwili na wingi. Waarabu husema: Huyu ni mjumbe wangu na msaada wangu, na hawa wawili ni Wajumbe wangu na nguzo yangu, na hawa (wengi) ni Wajumbe wangu na nguzo yangu. Miongoni mwa haya ni kauli ya Mwenyezi Mungu (swt): [فَإِنَّهُمْ عَدُوٌّ لِي] “Kwa kuwa wao ni maadui zangu”. Na ikasemwa: Maana yake ni kuwa kila mmoja wetu ni Mtume wa Mola Mlezi wa walimwengu wote].

c- Kwa kuzichunguza Aya hizi mbili na Aya nyenginezo ambamo Harun (as) ametajwa kwa neno al-irsal (kutumwa) na al-Risala (ujumbe), inadhihirika kuwa kumtaja kwa neno al-irsal ilikuwa daima. pamoja na Musa (as), yaani, kwa kumfuata, kwa mfano kauli yake Mwenyezi Mungu isemayo: [ثُمَّ أَرْسَلْنَا مُوسَى وَأَخَاهُ هَارُونَ بِآيَاتِنَا وَسُلْطَانٍ مُبِينٍ] “Kisha tukamtuma Musa na ndugu yake Harun pamoja na aya zilizo wazi” [Al-Mu’minun: 45]

[وَأَخِي هَارُونُ هُوَ أَفْصَحُ مِنِّي لِسَاناً فَأَرْسِلْهُ مَعِيَ رِدْءاً يُصَدِّقُنِي إِنِّي أَخَافُ أَنْ يُكَذِّبُونِ]  “Na ndugu yangu Harun ni fasihi zaidi ulimi wake kuliko mimi. Basi mtume ende nami kunisaidia, ili anisadikishe. Hakika mimi nina khofu watanikadhibisha.” [Al-Qasas: 34]

[وَإِذْ نَادَى رَبُّكَ مُوسَى أَنِ ائْتِ الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ * قَوْمَ فِرْعَوْنَ أَلَا يَتَّقُونَ * قَالَ رَبِّ إِنِّي أَخَافُ أَنْ يُكَذِّبُونِ * وَيَضِيقُ صَدْرِي وَلَا يَنْطَلِقُ لِسَانِي فَأَرْسِلْ إِلَى هَارُونَ * وَلَهُمْ عَلَيَّ ذَنْبٌ فَأَخَافُ أَنْ يَقْتُلُونِ * قَالَ كَلَّا فَاذْهَبَا بِآيَاتِنَا إِنَّا مَعَكُمْ مُسْتَمِعُونَ * فَأْتِيَا فِرْعَوْنَ فَقُولَا إِنَّا رَسُولُ رَبِّ الْعَالَمِينَ * أَنْ أَرْسِلْ مَعَنَا بَنِي إِسْرَائِيل]

Na Mola wako Mlezi, alipo mwita Musa, akamwambia: Fika kwa watu madhaalimu * Watu wa Firauni. Hawaogopi? * Akasema: Hakika mimi nachelea wasinikanushe * Na kifua changu kina dhiki, na ulimi wangu haukunjuki vyema. Basi mtumie ujumbe Harun * Na wao wana kisasi juu yangu, kwa hivyo naogopa wasije kuniuwa * Akasema: Siyo hivyo kabisa! Nendeni na miujiza yetu. Hakika Sisi tu pamoja nanyi, tunasikiliza  * Basi mfikieni Firauni na mwambieni: Hakika sisi ni Mitume wa Mola Mlezi wa walimwengu wote * Waachilie Wana wa Israili wende nasi.” [Ash-Shu’ara: 10-17]

[اذْهَبْ أَنْتَ وَأَخُوكَ بِآيَاتِي وَلَا تَنِيَا فِي ذِكْرِي * اذْهَبَا إِلَى فِرْعَوْنَ إِنَّهُ طَغَى * فَقُولَا لَهُ قَوْلاً لَيِّناً لَعَلَّهُ يَتَذَكَّرُ أَوْ يَخْشَى * قَالَا رَبَّنَا إِنَّنَا نَخَافُ أَنْ يَفْرُطَ عَلَيْنَا أَوْ أَنْ يَطْغَى * قَالَ لَا تَخَافَا إِنَّنِي مَعَكُمَا أَسْمَعُ وَأَرَى * فَأْتِيَاهُ فَقُولَا إِنَّا رَسُولَا رَبِّكَ فَأَرْسِلْ مَعَنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ وَلَا تُعَذِّبْهُمْ قَدْ جِئْنَاكَ بِآيَةٍ مِنْ رَبِّكَ وَالسَّلَامُ عَلَى مَنِ اتَّبَعَ الْهُدَى * إِنَّا قَدْ أُوحِيَ إِلَيْنَا أَنَّ الْعَذَابَ عَلَى مَنْ كَذَّبَ وَتَوَلَّى]

Nenda, wewe na ndugu yako, pamoja na ishara zangu, wala msichoke kunikumbuka * Nendeni kwa Firauni. Hakika yeye amepindukia mipaka * Mwambieni maneno laini, huenda akazingatia au akaogopa * Wakasema: Ewe Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tunaogopa asije akapindukia mipaka juu yetu au kufanya jeuri * Akasema: Msiogope! Hakika Mimi ni pamoja nanyi. Nasikia na ninaona * Basi mwendeeni, na mwambieni: Hakika sisi ni Mitume wa Mola wako Mlezi! Basi waache Wana wa Israili watoke nasi, wala usiwaadhibu. Sisi tumekuletea ishara itokayo kwa Mola wako Mlezi. Na amani itakuwa juu ya aliye fuata uwongofu * Hakika tumefunuliwa sisi kwamba hapana shaka adhabu itamsibu anaye kadhibisha na akapuuza.” [Ta-Ha: 42-48]. Ni wazi kutokana na nususi zote hizi kwamba Harun (as) hakuwa peke yake katika maelezo ya Ujumbe; bali, maelezo yalikuwa juu ya Musa na juu yake pamoja, amani iwe juu yao wote wawili, ikimaanisha kwamba Harun (as), hakuwa huru na wa kipekee katika maelezo ya Ujumbe.

d- Lakini pale Harun (as) anapotajwa ndani ya Qur’an Tukufu huru peke yake katika maelezo, aliitwa Nabii na sio Mtume, na huu ni wakati ambao Qur’an ilimthibitisha Musa (as) sifa ya Mtume na Nabii kwa pamoja, Mwenyezi Mungu (swt) asema:

Na mtaje Musa katika Kitabu. Hakika yeye alikuwa ni mwenye kuchaguliwa, na alikuwa Mtume, Nabii * Na tulimwita upande wa kulia wa mlima na tukamsogeza kunong'ona naye * Nasi kwa rehema zetu tukampa nduguye, Harun, awe Nabii. [Maryam: 51-53] Yeye (swt) amesema kuhusu Musa (as) kwamba yeye alikuwa: [رَسُولًۭا نَّبِيًّۭا]  “alikuwa Mtume na Nabii[Maryam: 51] Ama Harun (as), mara tu baada ya hilo, Qur’an haikuthibitisha maelezo ya Ujumbe, lakini ilitosheleza kumsifia kwa unabii: [أَخَاهُ هَارُونَ نَبِيّاً]nduguye, Harun, awe Nabii.” [Maryam: 53]. Hili linaunga mkono ufahamu wetu kwamba Musa (as) ni Nabii na Mtume, kwa sababu Shariah mpya ilitumwa kwake na akaamrishwa kuifikisha. Ama Harun (as) yeye ni Nabii wala si Mtume kwa sababu alimfuata Musa (as) na akaamrishwa kufikisha Ujumbe wa Musa (as), na Shariah yake bila ya kuwa na Shariah mpya inayojitegemea. Yafuatayo yameelezwa katika tafsiri ya aya hizi katika Ibn Kathir:

[Tafsir Ibn Katheer (5/237) ...Pindi Mwenyezi Mungu (swt) alipomtaja Ibrahim Al-Khalil na kumsifu, Al-Kaleem Alitaja, na kusema:

[وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ مُوسَى إِنَّهُ كَانَ مُخْلَصاً]  “Na mtaje Musa katika Kitabu. Hakika yeye alikuwa ni mwenye kuchaguliwa” [Maryam: 51].

[وَكَانَ رَسُولا نَبِيّاً]  “na alikuwa Mtume na Nabii [Maryam: 51] Sifa mbili ziliunganishwa kwa ajili yake, kwa sababu alikuwa miongoni mwa Mitume watukufu watano (Uli Al-Azam), nao ni: Nuh, Ibrahim, Musa, Isa na Muhammad, rehma na amani ziwashukie wao na Manabii wote waliosalia... Na kauli yake:

[وَوَهَبْنَا لَهُ مِنْ رَحْمَتِنَا أَخَاهُ هَارُونَ نَبِيّاً]  “Nasi kwa rehema zetu tukampa nduguye, Harun, awe Nabii. [Maryam: 53]. Ikimaanisha: Tulijibu dua na ombi lake kwa kaka yake, hivyo tukamfanya Nabii, kama alivyosema katika aya nyengine

[وَأَخِي هَارُونُ هُوَ أَفْصَحُ مِنِّي لِسَاناً فَأَرْسِلْهُ مَعِيَ رِدْءاً يُصَدِّقُنِي إِنِّي أَخَافُ أَنْ يُكَذِّبُونِ]  “Na ndugu yangu Harun ni fasihi zaidi ulimi wake kuliko mimi. Basi mtume ende nami kunisaidia, ili anisadikishe. Hakika mimi nina khofu watanikadhibisha. [Al-Qasas: 34]. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[قَدْ أُوتِيتَ سُؤْلَكَ يَا مُوسَى]  “Hakika Umepewa maombi yako, ewe Musa!” [Ta-Ha: 36] Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[فَأَرْسِلْ إِلَى هَارُونَ * وَلَهُمْ عَلَيَّ ذَنْبٌ فَأَخَافُ أَنْ يَقْتُلُونِ]  “Basi mtumie ujumbe Harun * Na wao wana kisasi juu yangu, kwa hivyo naogopa wasije kuniuwa.” [Ash-Shu’ara: 13-14].

Ndio maana baadhi ya waliotangulia walisema: Hakuna aliyepewa uombezi duniani kuliko uombezi wa Musa kwa Harun, kwamba yeye awe Nabii. Mwenyezi Mungu (swt) asema: [وَوَهَبْنَا لَهُ مِنْ رَحْمَتِنَا أَخَاهُ هَارُونَ نَبِيّاً]  “Nasi kwa rehema zetu tukampa nduguye, Harun, awe Nabii. [Maryam: 53] Ibn Jarir amesema: Ya'qub alituambia, Ibn Aliyah alituambia, kutoka kwa Daud, kutoka kwa Ikrimah, alisema: Ibn Abbas alisema: Kauli yake. [وَوَهَبْنَا لَهُ مِنْ رَحْمَتِنَا أَخَاهُ هَارُونَ نَبِيّاً]  “Nasi kwa rehema zetu tukampa nduguye, Harun, awe Nabii. [Maryam: 53] Akasema: Harun alikuwa mkubwa kuliko Musa, lakini alitaka kumpa unabii wake].

3-Kutokana na yaliyotajwa hapo juu, inadhihirika kuwa kwa mujibu wa ufafanuzi tunaouchukua wa Nabii na Mtume, Musa (as), ni Nabii kwa sababu iliteremshwa Shariah ili kuifikisha, na Mtume kwa sababu Shariah maalum iliteremshwa kwake. Ama Harun (as) ni Nabii kwa sababu aliteremshiwa Shariah, lakini yeye si Mtume kwa sababu Shariah iliyoteremshwa kwake kufikisha haikuwa makhsusi kwake; bali ilikuwa ni Shariah makhsusi kwa kaka yake Musa (as).

Haya ndiyo tunayoyaona kuwa ndiyo rai iliyo sahihi katika jambo hili, nayo ndio rai yetu iliyotabanniwa, na Mwenyezi Mungu (swt) ni Mjuzi Zaidi na Mwingi wa hekima.

Ndugu Yenu,

Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

12 Shawwal 1444 H

2/5/2023 M

Link ya jibu hili kutoka ukurasa wa Amiri wa Facebook

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu