Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Jibu la Swali
Matukio Nchini Kyrgyzstan
(Imetafsiriwa)

Swali:

["Mapema mnamo siku ya Ijumaa, Bunge la Kyrgyz liliidhinisha kujiuzulu kwa Rais Sooronbay Jeenbekov, na kufutilia mbali hali ya hatari, ambayo ilitangazwa wiki moja iliyopita katika mji mkuu, Bishkek ..." (www.yenisafak.com/ar/,16 / 10/2020)]. Mji mkuu wa Kyrgyz umeshuhudia maandamano ya vurugu; waandamanaji walichukua udhibiti wa makao makuu ya serikali, wakidai kufutwa kazi kwa Rais Sooronbay Jeenbekov, ambaye ni mwaminifu kwa Urusi, na hili limefanikiwa kwao ... Kwa hivyo, ni upi uhalisia ulioko nyuma ya matukio haya nchini Kyrgyzstan? Je! Ushawishi wa Urusi uko njia unaondoka kutoka katika nchi hii ya Kiislamu? Je! Kuna dori yoyote ya Amerika katika mzozo huu? Jazak Allah Khair.

Jibu:

Ili kupata jibu wazi na kuelewa uhalisia wa matukio nchini Kyrgyzstan, yafuatayo lazima yafafanuliwe:

Kwanza: hali jumla nchini Kyrgyzstan:

1- Kyrgyzia au Kyrgyzstan, ni moja ya nchi za Kiislamu katika Asia ya Kati, mipaka yake imeunganishwa na China leo kutoka upande wa Mashariki wa Turkestan, pamoja na nchi zingine za Kiislamu za Asia ya Kati: Kazakhstan, Uzbekistan na Tajikistan. Kyrgyzstan imekuwa ikikaliwa na Urusi ya kiTsar tangu 1876 M. Kulikuwepo na mapinduzi mengi dhidi ya uvamizi wa Urusi huko. Walakini, Urusi iliweza kuyaavya. Kyrgyzstan ikawa jamhuri ndani ya Umoja wa Kisovyeti, ikimaanisha kwamba ilitawaliwa moja kwa moja kutoka Moscow kuanzia 1876 hadi 1991 wakati Umoja wa Kisovyeti ulipovunjwa na Kyrgyzstan kutangaza uhuru wake. Lakini tabaka la kisiasa ndani yake lilikuwa limezama katika uaminifu wao kwa Urusi, kwa hivyo Urusi, baada ya uhuru wake, ilikuwa na ushawishi mkubwa juu ya Kyrgyzstan ..

2-Kyrgyzstan ilitawaliwa tangu uhuru wake na viongozi wa Chama cha Kikomunisti baada ya kubadilisha barakoa zao na kuanzisha vyama vyenye majina mengi. Vilikuwa moja kwa moja chini ya maagizo ya Moscow, lakini kipindi cha udhaifu wa Urusi wakati wa miaka ya tisiini na kuregea nyuma kwake kuliipa Amerika mwanya wa kuwafikia wanasiasa hawa. Wakati wa mbio za wahafidhina wapya kipindi cha enzi ya George Bush Mwana, na tangazo la Amerika la vita dhidi ya Uislamu na uzinduzi wake wa vita vya Amerika dhidi ya Afghanistan na Iraq, Amerika iliweza kupenya Asia ya Kati na kuanza kusuka uhusiano na watawala wake na nguvu za kisiasa, na ndani ya muundo huu ilianzisha Kambi ya Jeshi ya Manas karibu na mji mkuu, Bishkek, kusaidia jeshi la Amerika katika vita vyake dhidi ya Afghanistan.

3- Kuzama kwa Amerika ndani ya sokomoko ya Iraq kati ya 2003 na 2009 kulisadifu kurudi kwa nguvu kwa serikali nchini Urusi baada ya Vladimir Putin kuchukua hatamu za uongozi jijini Moscow. Kwa hivyo, mnamo 2014 Amerika ililazimika kuvunja Kambi yake ya Jeshi ya Manas karibu na Bishkek, na badali yake Urusi iliimarisha kambi yake ya jeshi nchini Kyrgyzstan, ambayo iliianzisha mnamo 2003. Mnamo 2015 Kyrgyzstan ilifutilia mbali makubaliano yake na Amerika:

[“Waziri Mkuu wa Kyrgyz Tamir Sariyev aliamuru serikali yake ifutilie mbali makubaliano ya pande mbili na Amerika ya 1993. Serikali ilisema katika taarifa kwamba makubaliano haya hayatatumika kuanzia Agosti ijayo 20." (Al-Jazeera Net, 22/7/2015)]. Kwa hivyo, Urusi ingefanikiwa katika kuuondoa ushawishi wa Amerika kikamilifu kutoka Kyrgyzstan. Urusi ilikuwa imeijumuisha Kyrgyzstan katika Shirika la Mkataba wa Usalama wa Pamoja (CSTO) ambalo lilianzishwa juu ya magofu ya Umoja wa Kisovyeti tangu kuanzishwa kwake mnamo 1992, na Kyrgyzstan iliendelea kuwa mwanachama hata wakati wa kipindi ambacho Amerika ilikuwa na ushawishi jijini Bishkek. Iliiongeza pia kwa Jumuiya ya Uchumi ya Eurasia tangu kuanzishwa kwake takriban mwaka 2014.

4-Kwa mtazamo wa kindani, tabaka la kisiasa nchini Kyrgyzstan, kama ilivyo katika nchi nyingi ambazo zilipata uhuru kwa sababu ya kusambaratika kwa Umoja wa Kisovieti, linasifika kwa ufisadi mkubwa. Ushindaniaji mamlaka ndani yake kwa haraka hubadilika kuwa mapambano makali kwa washindani kupata utajiri wa Ummah, na fahamu zozote za utunzaji hazipo. Watu wameachwa wakizurura bila mlinzi wa kuwaangalia. Kwa sababu kina cha ufisadi ni kikubwa, watu nchini Kyrgyzstan mnamo 2005 walimwasi Rais Akayev, ambaye alitawala tangu uhuru. Kwa hivyo, alikimbilia Urusi. Mnamo 2010, watu walimwasi Rais Bakiyev kwa wimbi kubwa la hasira ambalo lilikatizwa na vitendo vya vurugu ambavyo viliathiri wahasiriwa wengi na kuishia kwa mapinduzi ya vikosi vya usalama dhidi ya rais, ambaye alikimbilia kusini mwa nchi, na kisha kuondoka hadi Kazakhstan, Atambayev aliwekwa kama rais wa mpito ...

5- Ingawa Urusi ilikuwa inachochea hali dhidi ya Uislamu na Waislamu katika Asia ya Kati, kwa zana zake, watawala ambao walikuwa wamefanikiwa katika enzi ya Soviet. Walakini, fikira za Kiisilamu zilienea tena nchini Kyrgyzstan kabla ya uhuru wake na baada ya hapo, na Hizb ut Tahrir ilikuwa ikilingania kwa uchangamfu utawala wa Uislamu na kusimamishwa kwa Khilafah ya Kiislamu, kazi yake ilikuwa ya kipekee, haswa katika mikoa ya kusini ambayo ni sehemu ya kijiografia ya Bonde la Ferghana, licha ya ukweli kwamba mamlaka nchini Kyrgyzstan, chini ya uelekezi wa Urusi ambayo inachuki na Uislamu, mithili ya dhalimu wa Uzbekistan na nchi zingine za Asia ya Kati, kwa hivyo waliikabili amali ya Hizb kwa ukandamizaji mkali. Lakini Uislamu nchini Kyrgyzstan bado una ushawishi mzuri katika maeneo mengi, licha ya shambulizi kali kutoka kwa Urusi na wafuasi wake.

Pili: Ghasia za hivi majuzi katika mji mkuu, Bishkek:

1- Rais Sooronbay Jeenbekov, ambaye amekuwa akitawala nchi hiyo tangu 2017, alikuwa amepanga kupata kura nyingi katika uchaguzi uliopita wa ubunge ambao utamuwezesha kurekebisha katiba, ili aweze kugombea tena baada ya kumalizika kipindi chake cha kikatiba, kwani katiba inatoa muhula mmoja tu wa urais wa miaka sita. Tangazo la ushindi wa kishindo kwa vyama vilivyo tiifu na karibu na rais katika uchaguzi wa ubunge lilikuwa mnamo tarehe 4/10/2020. Ni vyama vinne tu kati ya 16 vilivyo weza kuvuka kizingiti cha bunge (7% ya kura), ikimaanisha kwamba bunge jipya (wanachama 120) lilitakiwa, kulingana na mpango wa Jeenbekov, kuundwa na vyama vyenye utiifu kwake na karibu naye, [“… Na Tume Kuu ya Uchaguzi nchini Kyrgyzstan ilitangaza kuwa vyama4 kati ya 16 vya kisiasa vilivyoshiriki uchaguzi vilifanikiwa kuingia katika bunge jipya lenye viti 120, ambavyo vilipelekea wafuasi wa vyama 12 ambavyo havikuwakilishwa bungeni kutoka katika maandamano dhidi ya matokeo.” (Daily Sabah ya Kituruki 6/10/2020)]. Mpango huu ulidhoofisha haki za kisiasa za vyama vingine ambavyo havikufanikiwa ("na vyama 12 vilivyoshindwa vilitoa tamko la pamoja ambalo walisema hawayatambui matokeo hayo ya uchaguzi ..." (TRT Kiarabu, 6/10/2020).

2- Kwa hivyo, wafuasi wa vyama vya kisiasa wanaokataa matokeo ya uchaguzi walimiminika kuanzia asubuhi mapema hadi Alato Square na karibu na Afisi ya Waziri Mkuu, kisha umati huu wenye hasira uliyashambulia na kuyateka makao makuu ya serikali, na kihakika waliliteka jengo la bunge na kukamata afisi ya rais. Vilevile umati wa watu ulivamia magereza na wafungwa maalum waliachiliwa huru. Makao makuu ya Kamati ya Usalama wa Kitaifa yalishambuliwa katika mji mkuu, Bishkek, na Rais wa zamani Atambayev, ambaye alikuwa amekaa ndani ya seli ndani yake akitumikia kifungo cha miaka 11 kwa mashtaka ya ufisadi, aliachiliwa huru. Sadyr Japarov aliachiliwa huru, na korti kwa haraka ilimwondoa mshtakiwa shtaka la utekaji nyara mnamo 2013. Tuhma hii ambayo kwayo alifungwa gerezani, na sambamba na mji mkuu, maandamano makubwa maarufu yalizinduliwa katika vituo vya majimbo yakishutumu serikali na kumtaka rais kujiuzulu, na katika majimbo ya kusini anakotokea rais, na ambako mikutano mingine ya kumuunga mkono ilizinduliwa, lakini haikuwa katika kiwango cha yale wanaotaka aondolewe.

3- Wimbi kubwa la maandamano lilitosha kuitisha serikali, kwa hivyo Waziri Mkuu na Spika wa Bunge waliwasilisha kujiuzulu kwao, kama vile wakuu wa majimbo mingine. Rais Jeenbekov alitoweka na huduma za usalama zikatoweka naye barabarani. Rais alitoa taarifa zake kutoka mahali palipofichwa kupitia mtandao, na kutangaza kwamba ameziagiza huduma za usalama zisishambulie waandamanaji. Aliutuhumu upinzani kwa kufanya mapinduzi na kuchukua madaraka, na akatangaza kwamba alikuwa tayari kwa maelewano. Aliitaka Kamati Kuu ya Uchaguzi ichunguze kasoro hizo na kufuta matokeo ikiwa ni lazima, katika kuashiria ukali na nguvu ya maandamano dhidi yake, [“Jeenbekov alivitaka vyama vya kisiasa kuwa na subira, akiwahutubia vijana: "Mumeonyesha kuwa thamani ya Kyrgyzstan ni kubwa kuliko kung'ang'ania mamlaka, na hiyo ni kwa vitendo sio kwa maneno, lengo letu ni kuhakikisha amani na utulivu katika nchi yetu, nina imani kwamba tutaibuka kutoka katika mgogoro huu kwa juhudi za pamoja. " Aliongeza, "Nawashukuru vijana ambao hawajasita katika kutekeleza majukumu yao nchini." (AR Haberler.com 7/10/2020)]

4- Kisha Kamati Kuu ya Uchaguzi ilitangaza kufuta matokeo ya uchaguzi, na vyama vya upinzani viliunda Baraza la Uratibu la Vikosi vya Upinzani, ambalo lilimteua Sadyr Japarov kama Waziri Mkuu mpya wakati wa kikao cha dharura cha Bunge kilichofanyika katika hoteli moja katika mji mkuu, Bishkek, yeye ndiye aliyeachiliwa huru na upinzani kutoka gerezani. [“Sadyr Japarov aliteuliwa kama rais mpya serikalini baada ya kura wakati wa kikao cha dharura, badala ya waziri mkuu wa zamani, Kubatbek Boronov, ambaye aliwasilisha kujiuzulu kwake, na kuongeza kuwa bunge la sasa litaendelea kufanya kazi hadi uchaguzi wa bunge jipya. ” (RT, 7/10/2020)]… [“Leo, Jumatano, zaidi ya wabunge 80 kati ya 120 walihudhuria kikao kisicho cha kawaida cha Bunge wakati ambao walipiga kura kuidhinisha kuteuliwa kwa Japarov kwenye nafasi hiyo na serikali yake inayopendekezwa. Jeenbekov kisha alitia saini amri ya kuthibitisha kuteuliwa kwa Japarov kama waziri mkuu pamoja na serikali yake, kulingana na taarifa ya afisi ya rais ...”(Al-Mayadeen, 14/10/2020)].

5- ["... na mapema leo, Ijumaa, Bunge la Kyrgyz liliidhinisha kujiuzulu kwa Rais Sooronbay Jeenbekov, na kufuta hali ya hatari, ambayo ilitangazwa wiki moja iliyopita katika mji mkuu, Bishkek." Wale walioshiriki kikao hicho, wakati ambao kujiuzulu kwa rais na kufutwa kwa hali ya hatari, kuliidhinishwa kwa umoja, pamoja na Jeenbekov na Waziri Mkuu Sadyr Japarov, pamoja na Spika wa Bunge Kanat Isayev. Kabla ya kura hiyo, Jeenbekov alitoa hotuba yake ya mwisho kwa wabunge, ambapo alisema kwamba kutekwa kwake ni ili kuhakikisha amani nchini na kuzuia mgawanyiko wa jamii ...” (Yenisafak Arabic, 16/10/2020 ]] Na kwa hivyo, ["Waziri Mkuu wa Kyrgyzstan, Sadyr Japarov, aliimarisha mamlaka yake, baada ya mamlaka ya urais kuhamishiwa kwake baada ya kujiuzulu kwa Rais Sooronbay Jeenbekov, ambayo "aliwasilisha" jana, na kuahidi kuhifadhi sera ya kigeni ya nchi hiyo. Japarov alisema leo, Ijumaa, mbele ya bunge: "Ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwamba mabadiliko ya mamlaka yalikuwa ya amani… nitajitahidi kadiri ya uwezo wangu kuhifadhi sera za kigeni na miongozo mingine muhimu." (Sputnik, 16/10/2020)].

Tatu: Ushawishi wa Urusi nchini Kyrgyzstan:

1- Ushawishi wa Urusi nchini Kyrgyzstan uko imara na una matawi. Urusi ilijenga kambi ya jeshi nchini Kyrgyzstan wakati ambapo Amerika ilikuwa ikiunda kambi yake ya jeshi, kwa hivyo ushawishi wa Urusi haukukosekana kutoka Kyrgyzstan hata katika kipindi ambacho Amerika iliweza kuanzisha ushawishi wake kwake. Urusi iliunda kambi ya jeshi mnamo 2003. [“Kituo cha Anga cha Kant cha Urusi kilifunguliwa nchini Kyrgyzstan mnamo Oktoba 2003, kama sehemu ya anga ya Kikosi cha Usambazaji wa Haraka cha Shirika la Mkataba wa Usalama wa Pamoja. Kazi zake kuu ni kufunika angaa shughuli za ardhini za CSTO. Ina vifaa vya ndege, helikopta za Su-25SM na Mi-8MTV ...” (RT, 28/3/2019)]. Siku iyo hiyo, Alhamisi, Moscow na Bishkek zilitia saini, wakati wa ziara ya Rais wa Urusi Vladimir Putin katika mji mkuu wa Kyrgyz, itifaki ambayo inaleta marekebisho ya makubaliano kati ya nchi hizo mbili kuhusu kambi ya jeshi la Urusi nchini Kyrgyzstan. Msaidizi wa Rais wa Urusi Yuri Ushakov alisema:

["Makubaliano kadhaa yametiwa saini, ikiwemo kutiwa saini kwa hati ya kurekebisha makubaliano ya 2012 kuhusu hadhi na hali ya kambi ya jeshi la Urusi nchini Kyrgyzstan." Kwa upande wake, Rais wa Urusi Vladimir Putin alisema, "Kambi ya jeshi la Urusi nchini Kyrgyzstan ni jambo muhimu kwa usalama na utulivu katika Asia ya Kati na inachangia uwezo wa ulinzi wa Kyrgyzstan." Msingi huu ni pamoja na ndege za kushambulia za Sukhoi-25 na helikopta za Mi-8 ...” (Jarida la Al-Dustour, 28/3/2019)]. Kwa hivyo rais wa Kyrgyzstan, Jeenbekov ni mwaminifu kikamilifu kwa Urusi, na anaratibiana pamoja nayo katika Mkataba wa Usalama wa Pamoja, na anaitii katika kila kitu inachotaka, kama vile kuimarisha kambi hiyo ya jeshi.

2- Lakini Urusi inaogopa sana kwamba vyama vingine vya upinzani ambavyo vina mawasiliano na Amerika vitachukua nguvu jijini Bishkek na kuvunja ushawishi kipekee wa Urusi ndani yake. Licha ya ukweli kwamba Urusi inaanzisha uhusiano na vyama vingi vya upinzani nchini Kyrgyzstan ili kuhakikisha kuwa hazina uadui na Urusi na kwamba baadhi ya vyama hivi ni waaminifu kwa Urusi na sio nje ya uwanja wake wa ushawishi, lakini Urusi inafuatilia ung'ang'aniaji huu wa mamlaka katika jaribio la kuzuia kuingiliwa kwa vikosi vya nje ndani yake na inaudhibiti juu ya huduma za usalama ambazo zinaweza kuingilia katika wakati muhimu mno. ["Rais wa Urusi Vladimir Putin alisema leo, Jumatano, kwamba Moscow inawasiliana na pande zote kwenye mzozo na inatarajia kurudi kwenye mchakato wa kidemokrasia hivi karibuni," (Al-Jazeera Net, 7/10/2020)] ... na kinachoongeza hofu ya Urusi ni kwamba mzozo mzito kati ya vikosi vya waaminifu kwake wakati mwingine huibuka, kama ilivyoonekana mara kwa mara, haswa hivi karibuni baada ya Rais Sooronbay Jeenbekov, ambaye ametawala nchi hiyo tangu 2017, kujaribu kudhibiti matokeo ya uchaguzi, ili aweze kugombea tena baada ya kumalizika kwa kipindi chake cha kikatiba, na hapo mtafaruku utatokea, haswa ikiwa udanganyifu utafichuliwa katika uchaguzi, ambao utawezesha kutumiwa na wafuasi wa Amerika, hata kama ni wachache na hivyo kuifedhehesha Urusi ...

3- Msimamo wa asili wa Urusi ni dhidi ya maandamano dhidi ya marais watiifu kwake. Huu ndio msimamo wa Urusi, isipokuwa ikiwa inalazimika kushikilia msimamo tofauti na huu ili kuhifadhi maslahi yake, kwani hairuhusu hali hiyo kutoka nje ya udhibiti wake. ["Kremlin ilikadiria leo kuwa nchi hii inakabiliwa na hali ya machafuko." Msemaji wa Afisi ya rais wa Urusi, Dmitry Peskov, alisema kuwa Urusi ina wajibu wa kuzuia kuporomoka kikamilifu kwa hali ya Kyrgyzstan." (Al-Jazeera Net, 8/10/2020)] . Urusi, ambayo ina udhibiti wa huduma za usalama nchini Kyrgyzstan, hairuhusu vyama ambavyo vina mawasiliano na Amerika na wafuasi wao kuongoza mandhari jijini Bishkek, na imekuwa ikishikilia fimbo ya Rais Jeenbekov ambaye alitangaza kuwa atajiuzulu bila kujiuzulu hadi Urusi itakapoamua hivyo kulingana na maslahi yake. Ndio maana Urusi ilimtuma naibu mkuu wa idara ya rais huko Kremlin Dmitry Kozak, wiki hii, kufanya mazungumzo na Jeenbekov na Japarov, na kusoma mambo kwa karibu... ["Ubalozi wa Urusi ulisema, jana, Jumanne: "Dori muhimu ya rais wa nchi "katika kuhakikisha maendeleo ya baadaye ya Kyrgyzstan ilisisitizwa wakati wa ziara ya Kozak ..." (Al-Mayadeen, 14/10/2020)], na hii yote ni kuchukua hatua zinazohitajika ... Walakini, haiwezekani kwamba Urusi itaingilia kijeshi moja kwa moja, kwani inaamini kuwa wafuasi wake wanaweza kudhibiti mambo nchini Kyrgyzstan, na kwamba vikosi vya usalama viko chini ya mikono yake na viko kwa matumizi yake ikiwa inataka kubadilisha rais kwa mwingine katika wafuasi wake, haswa kwa kuwa vikosi vingi vya kisiasa ni wafuasi wake!

4- Sasa kwa kuwa maandamano yameongezeka, Urusi iliamua "kutuliza hali" kwamba Rais wa Kyrgyzstan anaidhinisha uteuzi wa Sadyr Japarov kama waziri mkuu, baada ya bunge kupiga kura ya kutaka kumrudisha mamlakani tarehe 14/10/2020 . Hii ilikuwa baada ya kuachiliwa huru kwake hivi karibuni kutoka gerezani mikononi mwa wafuasi wake, ambako alikuwa akitumikia kifungo kwa zaidi ya miaka 11. [“Leo, Jumatano, zaidi ya wabunge 80 kati ya 120 walihudhuria kikao kisicho cha kawaida cha Bunge wakati ambao walipiga kura kuidhinisha kuteuliwa kwa Japarov kwenye nafasi hiyo pamoja na serikali yake inayopendekezwa. Jeenbekov kisha alitia saini amri ya kuthibitisha kuteuliwa kwa Japarov kama waziri mkuu pamoja na serikali yake, kulingana na taarifa ya afisi ya rais ...” (Al-Mayadeen, 14/10/2020)]

5- ["... na mapema leo, Ijumaa, Bunge la Kyrgyz liliidhinisha kujiuzulu kwa Rais Sooronbay Jeenbekov, na kufuta hali ya hatari, ambayo ilitangazwa wiki moja iliyopita katika mji mkuu, Bishkek." Wale walioshiriki kikao hicho, wakati ambao kujiuzulu kwa rais na kufutwa kwa hali ya hatari, kulikubaliwa kwa umoja, walijumuisha Jeenbekov na Waziri Mkuu Sadyr Japarov, pamoja na Spika wa Bunge Kanat Isayev. Kabla ya kura hiyo, Jeenbekov alitoa hotuba yake ya mwisho kwa wabunge, ambapo alisema kuwa kutekwa kwake ni ili kuhakikisha amani nchini na kuzuia mgawanyiko wa jamii ...” (Yeni Safak Arabi: 16/10 / 2020)].

Na kwa hivyo, ["Waziri Mkuu wa Kyrgyzstan, Sadyr Japarov, aliimarisha mamlaka yake, baada ya mamlaka ya urais kuhamishiwa kwake baada ya kujiuzulu kwa Rais Sooronbay Jeenbekov, ambayo "aliwasilisha" jana, na kuahidi kuhifadhi sera ya kigeni ya nchi. Japarov alisema leo, Ijumaa, mbele ya bunge: "Ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwamba mabadiliko ya mamlaka yalikuwa ya amani… nitajitahidi kadiri ya uwezo wangu kuhifadhi sera ya kigeni na miongozo mingine muhimu." (Sputnik, 16/10/2020)].

Nne: Dori ya Amerika:

1- Kwa upande wa Amerika, msimamo wake ulikuwa wazi, ilitumia kile kilichotokea katika uchaguzi ili kuifedhehesha Urusi na mamlaka ya Kyrgyz. [“Amerika ilizihimiza pande zote nchini Kyrgyzstan kujizuia na kupata suluhisho la amani, ikielezea wasiwasi juu ya vitendo ambavyo vilivuruga uchaguzi na kusababisha maandamano makubwa. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Amerika aliambia AFP "Tunatoa wito kwa pande zote kupinga ghasia na kusuluhisha mzozo wa uchaguzi kwa njia za amani." Wizara ya Mambo ya Nje ya Amerika iliashiria kuwa misheni ya ufuatiliaji iliyoungwa mkono na Shirika la Usalama na Ushirikiano barani Ulaya "ilihitimisha kwa habari za kuaminika juu ya ununuzi wa kura ambao ulivuruga uchaguzi." (AlJazeera.net 7/10/2020)].

Hii inamaanisha kuwa hali mpya nchini Kyrgyzstan, ambazo zinasifika kwa sintofahamu ya kisiasa, zinaipatia Amerika mazingira mwafaka ya kuingia nchi hii, na bila shaka ina mawasiliano na vyama kadhaa vya upinzani. Ilituhumiwa mwanzoni mwa mwaka huu kwa kutumia dolari milioni 60 pesa taslimu kusaidia wagombea na vyama vya wabunge ili wafuasi wake wawe na ushawishi. Ikiongezea na pesa zingine zilizotumiwa na Wakfu wa George Soros kwa kusudi la kuvuruga utulivu katika nchi inayotawaliwa na ushawishi wa Urusi, na pesa hizo zote zilitumika bila ya serikali ya Jeenbekov kujua, kulingana na wavuti wa kampuni ya time, 10/1/2020

2- Amerika ina wafuasi katika upinzani wa Kyrgyz, lakini ni wachache na hawana ufanisi katika kuondoa ushawishi wa Urusi nchini Kyrgyzstan hadi leo, lakini wanafanya kazi ya kupatiliza kutoelewana kokote kati ya wafuasi wa Urusi wanaoshindania mamlaka, na wangekuwa karibu kufaulu lau Urusi haingemwamuru Jeenbekov kujiuzulu ili kutuliza hali hiyo. Urusi inafanya kazi katika kuteua watu wengine baada ya uchaguzi uliofanyika chini ya macho na masikio yake.

Tano: Hitimisho ni:

1- Ung'ang'aniaji mamlaka nchini Kyrgyzstan kimsingi ni mzozo wa kindani, na ni kwa sababu ya ukosefu wa ukomavu katika mawazo ya utawala wa viongozi wa kisiasa katika nchi hii ya Kiislamu. Na kwa sababu ya hili, mizozo na ghasia huibuka, ambayo kiasili ni ya kimbari, kikanda au kikabila, na ya vyama vya upinzani, na vile vile "uaminifu", hata ingawa ina majina jumla. Walakini, wataalamu hutofautisha mielekeo yake ili isibadilike kutoka kwa asili ya kimbari, kikanda au kikabila. Mgogoro huu, na katika kesi hii, haukusudiwi kuondoa ushawishi mkubwa wa Urusi kutoka katika jamhuri hii ndogo, bali Urusi inaogopa mawasiliano ya Amerika na vyama vingine vya upinzani kwa sababu ya machafuko yaliyotokea baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa bunge, inaogopa kwamba Amerika itapata nafasi kutia mguu wake tena baada ya Urusi kufanya juhudi zake kuiondoa kutoka Kyrgyzstan, na kwa hivyo itakuwa na ushawishi ambao kwao inaweza kufanya kazi dhidi ya Urusi ndani na pambizoni mwa Kyrgyzstan.

2- Hii itabaki kuwa hali ya Waislamu nchini Kyrgyzstan na kwingineko, ambapo watawala wa kutisha wanaowatawala, ambao huusukuma Ummah kuteremka kutoka chini hadi chini zaidi, na wanajali tu maslahi yao ya kibinafsi; wanauona uamuzi huo kama ngawira, hawana mtazamo wa kuangalia mambo ya Umma ambao huwateua au kukaa kimya juu ya uteuzi wao na kafiri anaye wakoloni. Hali hiyo itabaki kuwa hivyo, hadi Umma unyanyuke na kundi lenye nguvu zaidi ndani yake lisimama, na kuwafukuza watawala hawa na kumng'oa mkoloni kafiri kutoka katika nchi za Waislamu, na kuunda dola yake, dola ya Khilafah, kwa msingi wa Dini yake, na kumueka mtawala kuitawala kulingana na yale yaliyoteremshwa na Mwenyezi Mungu (swt), ambaye atakuwa ndiye msaada wake kwa maisha bora na kwa njia yake ya kwenda mbinguni, Mwenyezi Mungu akipenda.

]يَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَيُدْخِلْكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ وَمَسَاكِنَ طَيِّبَةً فِي جَنَّاتِ عَدْنٍ ذَلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ * وَأُخْرَى تُحِبُّونَهَا نَصْرٌ مِنَ اللَّهِ وَفَتْحٌ قَرِيبٌ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ]

“Atakusameheni dhambi zenu, na atakutieni katika Mabustani yapitiwayo na mito kati yake, na maskani nzuri nzuri katika Bustani za milele. Huko ndio kufuzu kukubwa *Na kinginecho mkipendacho, nacho ni nusura itokayo kwa Mwenyezi Mungu, na ushindi ulio karibu! Na wabashirieni Waumini!” [As-Saff: 12-13]

1 Rabii’ Al-Awwal 1442 H

18/10/2020 M

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumamosi, 28 Novemba 2020 23:06

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu