Ijumaa, 08 Jumada al-thani 1447 | 2025/11/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Jibu la Swali

Ruwaza ya Marekani ya Kutatua Kadhia ya Cyprus
(Imetafsiriwa)

Swali:

“Afisi ya rais wa Uturuki ilitangaza mnamo Jumatatu kwamba Rais wa Jamhuri ya Uturuki ya Cyprus Kaskazini, Tufan Erhürman, atatembelea Ankara Alhamisi ijayo, 13/11/2025... Burhanettin Duran, mkuu wa idara ya mawasiliano ya rais wa Uturuki, alisema kwamba ziara ya Erhürman Ankara inakuja kutokana na mwaliko wa Rais Erdoğan, na Duran aliongeza kwamba ziara hiyo itakuwa kituo cha kwanza cha kigeni cha Erhurman... Na mnamo tarehe 19 Oktoba Bodi Kuu ya Uchaguzi ya Uturuki ya Cyprus ilitangaza ushindi wa kiongozi wa Chama cha Republican cha Kituruki, Tufan Erhürman, katika uchaguzi wa rais.” (Shirika la Anadolu, 10/11/2025). Kwa hivyo ni nini kimesababisha maridhiano haya? Ikifahamika kwamba Erhurman, wakati wa kampeni yake ya uchaguzi, alikuwa akitoa wito wa kuunganisha kisiwa hicho, huku Erdogan akitoa wito wa dola mbili? Na je, Amerika iko nyuma ya maridhiano hayo? Na Mwenyezi Mungu akulipe kheri.

Jibu:

Ili kufafanua jibu la maswali hayo hapo juu, tunahakiki mambo yafuatayo:

Kwanza: Mgombea wa upinzani nchini Cyprus Kaskazini, Tufan Erhurman, alishinda kutoka raundi ya kwanza ya uchaguzi na kupata zaidi ya 62% ya kura ikilinganishwa na chini ya 36% kwa rais wa sasa Ersin Tatar. (RT, 19/10/2025). Jambo jipya katika chaguzi hizi ni kwamba mgombea wa upinzani, ambaye alijenga kampeni yake ya uchaguzi kwa kuunganisha kisiwa hicho na Cyprus ya Ugiriki, alishinda kutoka raundi ya kwanza na kwa tofauti kubwa, huku rais wa sasa anayetaka suluhisho la dola mbili—suluhisho ambalo Uturuki imekuwa ikilipigia debe kwa miongo kadhaa—alianguka. Ili kuelewa athari za ndani na kimataifa za matokeo haya, tuna hakiki yafuatayo:

1. Kutoka pembe ya uwepo wa Uturuki nchini Cyprus Kaskazini: Uturuki wakati wa makubaliano yake na Waingereza, ilitumia kutengwa kwa Waislamu wa Cyprus ya Kituruki na Wa-Cyprus ya Ugiriki na kuingilia kati kijeshi mwaka wa 1974 ili kuzuia kuingia kwa ushawishi wa Marekani kisiwani kupitia vibaraka wa Amerika, na ilifanikisha hilo wakati huo. Lakini miaka ya Erdoğan madarakani imehamisha Uturuki kutoka kambi ya Uingereza hadi kambi ya Marekani, na hivyo uwepo wa Waturuki kaskazini mwa kisiwa hicho umekuwa kijiti mkononi mwa Amerika. Kuhusu hali ya ndani, masekula waliendelea kuwa na nguvu zaidi kaskazini mwa kisiwa hicho, na maafisa wa serikali waliendelea kuwazuia wasichana hata kuvaa hijabu (Khimar) mashuleni. Uamuzi wa Waziri Mkuu uliporuhusu hilo mnamo Aprili 2025, Mahakama Kuu ya Katiba ilibatilisha uamuzi huo mnamo Septemba 2025 (Gazeti la Haberler, 25/9/2025), ambayo inaonyesha kupenya kwa kina kwa usekula nchini Cyprus Kaskazini.

2. Na kwa sababu Uturuki haikuhamisha uzoefu wowote wa kiuchumi uliofanikiwa hadi sehemu ya kaskazini ya kisiwa hicho, na hali katika sehemu ya kaskazini ilibaki kuwa ya kiuchumi kidogo, na hata ikageuka kuwa kimbilio la pesa zisizo safi, na kasino zikaenea... huku kwa upande mwingine, Cyprus ya Ugiriki ikawa mwanachama wa Muungano wa Ulaya mnamo 2004 na kujiunga na Eurozone mnamo 2008. Yote haya yaliongeza hamu ya wale waliotaka kuungana tena kwa kisiwa hicho na Cyprus ya Ugiriki, haswa kwa kuwa Uturuki imekuwa ikibisha mlango wa Muungano wa Ulaya kwa miongo kadhaa na haujafunguliwa kwa ajili yake!

Pili: Hali hii ya ndani, mafungamano haya na Uturuki, na msukosuko huu wa kisekula yalichangia matokeo haya ya uchaguzi ambapo mgombea Tufan Erhürman alishinda kwa wingi na kutoka raundi ya kwanza. Lakini hali hizi za ndani hazikuwa kichocheo kikuu kilicholeta ushindi huu, kwani mabadiliko katika ulimwengu wa kimataifa na ugunduzi wa gesi asilia katika Mediterania ya Mashariki yalitoa vivuli vyake. Ufafanuzi ni kama ifuatavyo:

1. Vita vya Urusi nchini Ukraine: Kama sehemu ya kujiandaa kwa matukio yote yanayowezekana ya maendeleo ya vita vya Urusi nchini Ukraine, na uwezekano wa Urusi kudhibiti Bahari Nyeusi, Amerika inaimarisha uwepo wake wa kijeshi katika kambi zake nchini Ugiriki, ikiwa ni pamoja na kuhamisha baadhi ya vifaa vya ardhini. Ili kukabiliana na hatari hizi za Urusi, mtazamo wa Amerika kuhusu Cyprus kama “meli maalum ya kubebea ndege” katika eneo hilo unafanywa upya, na hivyo Amerika inafufua ndoto zake za zamani za kuanzisha kambi za kijeshi kisiwani humo. Vita nchini Ukraine vinaongeza hitaji la Amerika la kambi kisiwani humo. Kutoka pembe ya vita vya Mashariki ya Kati, Amerika inaona uwepo wa kijeshi nchini Cyprus kama imara zaidi kuliko uwepo wake katika eneo la Kiarabu, ambalo mabadiliko yake na hisia zinazoongezeka za Kiislamu inaziogopa zinaweza kufukuza ushawishi wa Marekani.

2. Ugunduzi wa gesi asilia: Ugunduzi mkubwa wa gesi katika Mediterania ya Mashariki katika miongo miwili iliyopita unachochea hamu ya makampuni ya nishati ya Marekani ambayo tayari yanashiriki leo katika kutumia viwanja vya gesi katika eneo hilo, na kuisukuma Amerika kupanua ushawishi wake zaidi. Katika suala hili, Cyprus ni kiungo muhimu, iwe ni kutoka kwa njia za uzalishaji au mabomba. Kwa sababu hii, balozi wa Marekani nchini Cyprus hukutana na rais wa Cyprus kila mara na kujadili naye masuala ya ugunduzi wa mafuta na gesi tangu 2018, pamoja na ziara za bunge huko Nicosia. Kwa sababu ya gesi hii, migogoro mipya iliibuka kati ya dola za eneo hilo kuhusu mipaka ya kiuchumi ya baharini. Na wakati utawala wa Trump uliporudi tena mwanzoni mwa mwaka, kasi ya makampuni ya nishati ya Marekani ilirudi nayo, na utawala wa Trump ukaanza kukimbilia kudhibiti uzalishaji wa gesi asilia katika Mediterania ya Mashariki, na kuifanya kuwa chombo cha ziada kwa zana zilizopo za kuifunga Ulaya nayo katika masuala ya nishati baada ya kuinyima gesi ya Urusi.

3. Udhaifu wa Uingereza baada ya Brexit: Mtazamo wa Amerika kuhusu Uingereza ulibadilika baada ya udhaifu wake kuonekana kufuatia Brexit. Licha ya ahadi za Amerika za makubaliano makubwa ya kibiashara wakati Uingereza ilipoondoka Muungano wa Ulaya mwaka wa 2020—ahadi ambazo hazikutimia—utawala wa Trump badala yake uliweka ushuru wa forodha ambao ulianza kuzima viwanda vya Uingereza. Na mtazamo mpya wa Amerika unahitaji kurithi ushawishi wa Uingereza na kutumia zana zake, hasa Cyprus. Jarida la Marekani, ‘The National Interest’—linalojulikana kwa msimamo wake wa kihafidhina unaoegemea Trump—lilichapisha mnamo 8/11/2024 makala ya mwanasiasa wa mrengo wa kulia wa Marekani Michael Rubin, akiitaka Amerika kuiondoa Uingereza kutoka Cyprus na kuchukua kambi mbili za kijeshi za Uingereza Akrotiri na Dhekelia, ambazo zinaunda 3% ya eneo la kisiwa hicho.

4. Uwezekano mkubwa ni kwamba mabadiliko haya ya kimataifa na ugunduzi wa gesi yamezalisha mwelekeo mpya wa Marekani kuelekea kuungana tena kwa Cyprus. Utawala wa Trump, wakati wa muhula wake wa kwanza, uliondoa vikwazo vya silaha vilivyowekwa dhidi ya Cyprus tangu 1987: (Marekani ilitangaza mnamo Jumanne kwamba kwa kiasi na kwa mwaka mmoja iliondoa vikwazo vilivyowekwa kwa zaidi ya miaka thelathini vya kuuza vifaa vya kijeshi vya Cyprus... Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilisema katika taarifa kwamba Waziri wa Mambo ya Nje Mike Pompeo “alimfahamisha” Rais wa Jamhuri ya Cyprus, Nikos, “juu ya uamuzi wake wa kuondoa vikwazo vya usafirishaji nje, na uhamisho wa vifaa vya ulinzi visivyo hatari na huduma za ulinzi.” (Swiss info, 2/9/2020). Kuondolewa huku kunafanywa upya kila mwaka. Kisha utawala wa Biden ulikamilisha njia hii kwa kutia saini makubaliano muhimu ya ulinzi na Cyprus: “Cyprus na Marekani zilitia saini muundo wa makubaliano ya ushirikiano wa ulinzi yanayoelezea njia za kuboresha majibu ya nchi hizo mbili kwa migogoro ya kibinadamu ya kikanda na wasiwasi wa usalama.” (Youm7, 10/9/2024).

Tatu: Katika tukio la nadra sana lililotokea tu mnamo 1970 na 1996 pekee, Rais wa Marekani Biden alimpokea rais wa Cyprus jijini Washington. Hii ilikuwa katika mwisho wa muhula wa Biden na baada ya kutangazwa kwa ushindi wa Trump, na Amerika ikatangaza msimamo wake: (Rais wa Marekani, ambaye alimpokea Rais Nikos Christodoulides katika Ikulu ya White House, alisema katika taarifa zake kabla ya mkutano: “Ninabaki na matumaini kuhusu uwezekano wa kuunganisha Cyprus kwa msingi wa shirikisho la kanda mbili, jumuiya mbili. Marekani iko tayari kutoa usaidizi wowote tunaoweza ili kufikia lengo hili.” Kwa upande wake, Rais Nikos alithibitisha kwamba anategemea usaidizi wa Marekani kuhusu suala la Cyprus…” (Shirika la Habari la Cyprus, 30/10/2024). Kabla ya hapo: “Waziri wa ulinzi wa utawala wa Cyprus, Pálmas, alisema kwamba ujenzi wa kituo cha helikopta karibu na Larnaca unaendelea, na vyombo vya habari vya utawala wa Cyprus ya Ugiriki viliripoti kwamba kituo hicho kitatengewa Marekani.” (Gazeti la ‘Turkey Today’, 29/7/2024).

Nne: Kuhusu Uturuki, ilikuwa imetangaza kukataa kwake makubaliano ya ulinzi kati ya Cyprus ya Ugiriki na Amerika (tovuti ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki, 11 Septemba 2024). Lakini kama dola inayozunguka katika mzunguko wa Amerika, haiwezi kupinga jambo ambalo Amerika imeamua. Kwa hivyo Uturuki ilianza kufanya mikutano ya ngazi ya juu na maafisa wa Ugiriki, na hata kuwasiliana na maafisa nchini Cyprus ya Ugiriki ingawa Uturuki haiwatambui:

1. “Maafisa wa Cyprus walisema marais wa Uturuki na Cyprus walikutana kando ya mkutano wa kilele nchini Hungary leo, Alhamisi, katika mkutano wa nadra. Naibu msemaji wa serikali ya Cyprus Yannis alisema kwenye mtandao wa X kwamba Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan pia alikuwepo.” (Al-Ittihad News, 7/11/2024). Hii inaweza kuwa tu kwa ombi la Amerika la kuisukuma Uturuki kujiandaa kukubali suluhisho la Marekani.

2. Uturuki ilipozidisha mvutano na Ugiriki, ilifanya hivyo kulingana na matakwa ya utawala wa kwanza wa Trump. Biden alipokuja na kufuata sera ya kurudi kuongoza washirika wake wa Ulaya, Uturuki—Erdoğan aliwiana na msimamo huu wa Marekani kinyume na utawala uliopita.

3. Upinzani wa Uturuki kwa ushirikiano wa ulinzi wa Marekani na Cyprus ya Ugiriki mnamo 2024 haukuwa na athari halisi, kwani mkutano wa Erdoğan na rais wa Cyprus wa Ugiriki ulikuja muda mfupi baada ya upinzani huo! Huu ni ushahidi kwamba Uturuki ya Erdoğan inajirekebisha kulingana na mwelekeo wa Marekani.

Tano: Kuhusu kauli ya rais mteule wa Cyprus Kaskazini: “Erhürman alielezea ushindi wake kama “ushindi kwa wananchi wote wa Cyprus ya Kituruki, wa vyama vyote,” akithibitisha azma yake ya kusimamia sera za kigeni “kwa uratibu wa karibu na Uturuki” ili kuhifadhi umoja wa cheo na msimamo.” (Al Jazeera Net, 20/10/2025). Hii ni kuandaa mazingira ya kuungana tena kati ya pande hizo mbili kuelekea kutekeleza mpango wa Marekani wa shirikisho nchini Cyprus. Kwa sababu hii, mshirika wa Erdoğan na kiongozi wa wazalendo wa Kituruki, Devlet Bahçeli, alikasirika sana, akakataa matokeo, na akatoa wito kwa Bunge la Cyprus Kaskazini kukutana haraka kukataa matokeo na kutangaza kujiunga na Jamhuri ya Uturuki (RT, 19/10/2025). Lakini Erdoğan mwenyewe, “Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan alimpongeza mnamo Jumapili kiongozi wa Chama cha Republican cha Kituruki katika Jamhuri ya kituruki ya Cyprus Kaskazini, Tufan Erhürman, kwa ushindi wake katika uchaguzi wa rais.” (Shirika la Anadolu, 19/10/2025), na hata alijivunia ukomavu wa demokrasia nchini Cyprus Kaskazini. Misimamo thabiti inasikika kutoka kwa duara za Kituruki zilizo mbali na utawala, huku duara ya Erdoğan, iliyozama katika mzunguko wa Amerika, ikichukua misimamo kulingana na mwelekeo wa Amerika. Kwa sababu hii, Erdoğan aliacha kuiunganisha Cyprus au suluhisho la dola mbili na kuanza kuegemea shirikisho.

Sita: Kutokana na hayo, hali inayowezekana ni kwamba mazungumzo ya kuunganisha kisiwa cha Cyprus yataongeza kasi kulingana na suluhisho la Amerika kwa msingi wa shirikisho la kanda mbili, la jumuiya mbili, ambapo wananchi wa Cyprus ya Ugiriki watakuwa na nguvu huku Waislamu wa Cyprus ya Kituruki watakuwa na haki ndogo za kisiasa, zikikubaliana na vita vya Amerika dhidi ya Uislamu na ruwaza yake ya dori kubwa kwa Cyprus yenye tabia ya Kigiriki inayoendana na Amerika. Uturuki imejiweka katika mzunguko wa Amerika na haiwezi kupinga. Ikiwa hali za ndani, za Uturuki, na kimataifa zitabaki kama zilivyo leo, njia itakuwa wazi wakati huu kwa mazungumzo yenye mafanikio ndani ya muundo wa muungano wa shirikisho kulingana na ruwaza ya Amerika. Na ni jambo linalowezekana kwamba ziara ya Tufan Erhürman nchini Uturuki mnamo siku ya Alhamisi, 13/11/2025, ni hatua ya kwanza katika kutekeleza mpango wa Amerika wa shirikisho la kanda mbili, la jumuiya mbili, huku masuala ya ndani ya kila eneo yakisimamiwa kando, huku ulinzi na mambo ya nje ukiwa mikononi mwa serikali ya shirikisho—yaani, wananchi wa Cyprus ya Ugiriki. Na ikiwa mambo yataendelea kama Amerika inavyotaka, mpango wake utajumuisha kuhamisha Cyprus kutoka kwa vikosi vya kigeni (kambi mbili za Uingereza na vikosi vya Uturuki) ili Amerika pekee iwe na kambi Kaskazini mwa Cyprus!

Saba: Ni jambo la kusikitisha sana kwamba utawala wa makafiri wa kikoloni unaendelea kuinuka juu ya ardhi za Waislamu moja baada ya nyengine mbele ya masikio na macho ya watawala Waislamu bila wao hata kukemea udhibiti huu, achilia mbali kuchukua hatua inayourudisha kwenye ardhi zake, na hata kuufuatilia kama ulivyofuatiliwa wakati wa enzi ya Khilafah Rashida hadi Uislamu utakapoenea na haki yake kote ulimwenguni... Lakini watawala watiifu kwa makafiri wakoloni wanawezaje kusimama dhidi yao? Cyprus ni shahidi: Amerika hufanya chochote inachotaka ndani yake, ingawa ni kisiwa cha Kiislamu kilichotekwa na Waislamu wakati wa Khilafah ya bwana wetu ‘Uthman, Khalifah wa tatu Rashid, mnamo 28 H. Ilikuwa moja ya safari za kwanza za baharini za Waislamu, na Maswahaba wengi walishiriki, wakiwemo Abu Dharr, ‘Ubada ibn al-Samit na mkewe Umm Haram, Abu al-Darda’, na Shaddad ibn Aws (ra). Kaburi la Sahabiyah mtukufu Umm Haram linabaki kuwa alama maarufu nchini Cyprus. Cyprus ina nafasi katika historia ya Kiislamu; kwa hivyo, wakati Makruseda wa Ulaya walipoikalia kimabavu katika vita vyao vya kwanza vya msalaba dhidi ya ardhi za Waislamu, Waislamu hawakupumzika hadi walipoikomboa na kuirudisha katika ardhi za Kiislamu. Kisha ikawa sehemu ya Dola ya Khilafah ya Uthmani kama ilivyokuwa kwa ardhi zengine za Waislamu wakati Khilafah ilipokwenda kwao. Khilafah ilipoondolewa, Waingereza waliiunganisha Cyprus na koloni zao. Lakini kama vile Waislamu walivyoirudisha kutoka kwa Makruseda hadi kwenye Nyumba ya Uislamu, watairudisha tena kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, Mwenye Nguvu, Mwenye Kusifiwa. Hili ndilo suluhisho sahihi kwa Cyprus: kwamba irudi kwenye asili yake kama ardhi ya Kiislamu kama ilivyokuwa ndani ya Khilafah ya Uthmani, na lazima irudi kuwa sehemu ya Uturuki hadi Khilafah irudi tena, na bendera ya Uislamu itakapoinuka juu yao na juu ya ardhi zote za Waislamu. Na hili kwa hakika litatokea, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na huo ndio ushindi mkubwa. Hili ndilo suluhisho na ndio ukweli:

[فَمَاذَا بَعْدَ الْحَقِّ إِلَّا الضَّلَالُ فَأَنَّى تُصْرَفُونَ]

“Na kipo kitu gani baada ya haki, isipokuwa upotovu tu? Basi huwaje mkageuzwa?” [Yunus:32].

Na sio suluhisho lililopangwa na Amerika au hapo awali na Uingereza. Kwa maneno mengine, suluhisho si kwamba Kupro iwe majimbo mawili, iwe moja imeunganishwa na Uturuki na

Na sio suluhisho lililopangwa na Amerika au hapo awali na Uingereza. Kwa maana nyengine, suluhisho sio kwamba Cyprus iwe dola mbili, moja iwe imeunganishwa na Uturuki na nyengine kwa Ugiriki, au hazijaunganishwa, wala Cyprus iwe dola ya shirikisho inayoongozwa na Warumi, wala hata dola moja inayoongozwa na Warumi; kwani ardhi yoyote ya Kiislamu haiwezi kuachwa kwa makafiri kuwa na mamlaka juu yake:

[وَلَنْ يَجْعَلَ اللَّهُ لِلْكَافِرِينَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ سَبِيلًا]

“wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini. [An-Nisa:141]. Cyprus, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, itarudi kama ilivyokuwa—ardhi ya Kiislamu. Siku zinazunguka, na mikono mingi imepita juu ya Cyprus, lakini mwisho daima ni kwa wachaMungu:

[وَاللَّهُ غَالِبٌ عَلَى أَمْرِهِ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ]

“Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kushinda katika jambo lake, lakini watu wengi hawajui.” [Yusuf:21].

21 Jumada al-Awwal 1447 H

12 Novemba 2025 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu