Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Amerika Ulaya Zatumbukiza Mikono Yake ndani ya Damu ya Sudan na Watu Wake Mbele ya Watawala kutoka Upande wa Kijeshi na Kiraia, Bali Hata kwa Usaidizi Wao, Mwenyezi Mungu Awaangamize; Wanahadaiwa Vipi?

(Imetafsiriwa)

Leo tarehe 25/10/2021 wananchi wa Sudan wameamkia kuibuka kwa vuguvugu kutoka kwa jeshi lililowakamata baadhi ya mawaziri pamoja na idadi kadhaa ya washiriki katika serikali ya mpito ya kiraia na kisha kukamatwa kwa Waziri Mkuu Hamdok mwenyewe... Baadaye, Al-Burhan alitoa hotuba kwenye televisheni ambapo alitangaza hali ya hatari, kuvunjwa kwa Baraza Kuu na Baraza la Mawaziri la mpito na kuachiliwa huru kwa wakurugenzi wa majimbo na kisha mawaziri wadogo wa wizara, na akatoa wito kwa wakurugenzi wakuu wa kusimamia masuala ya wizara... Alitangaza kuwa hakufutilia mbali waraka wa katiba, bali alifutilia mbali ibara muhimu kama ilivyoelezwa kwenye hotuba yake, na kwamba anataka kurekebisha mwenendo wa mapinduzi na sio kuyatelekeza na mapinduzi!

Enyi Waislamu: Ardhi za Waislamu zimekuwa jukwaa la makafiri wa kikoloni, ambao ni hatari zaidi kwa Uislamu na watu wake, kushindania ardhi zao, kisha wanajitafutia zana kutoka kwa vijana wa Waislamu wanaoshikilia mikono yao kwa kuwaunga mkono, kana kwamba hawadiriki. Badala yake, kwa kweli hawadiriki. Amerika na vibaraka wake katika uongozi wa jeshi: Al-Burhan na wasaidizi wake, na Ulaya, hasa Uingereza, katika wizara ya Hamdok na ndugu zake, wanang'ang'na juu ya ni nani atakayepata udhibiti na utawala juu ya Sudan na watu wake kunyonya mali yake na kunyakua eneo na rasilimali zake. Hatukusudii kughafilika kwa watu wake, bali tunakusudia utambuzi wa wale wanaozidhibiti shingo zao, sawa ikiwa ni Burhan au Hamdok, bila ya kuona haya mbele ya Mwenyezi Mungu (swt), wala mbele ya Mtume Wake (saw) wala mbele ya waja wake, bali ni kukimbilia kwenye yale yanayowatengenezea njia hizaya katika maisha ya dunia na Akhera, na hiyo ndiyo fedheha kubwa kabisa.

Pande hizo mbili huchimba mashimo kwa kila mmoja kutumbukia! Pande hizo mbili zilikubaliana juu ya waraka wa katiba mnamo Agosti 21, 2019 kwa muda wa miezi 39, kwa Burhan na wasaidizi wake kutawala kwa miezi 21, kisha Hamdok na wale walio pamoja naye watafuata kwa miezi 18 ijayo, na kisha raia watachukua Mei 2021. Hata hivyo, ilifanyiwa marekebisho baada ya Mkataba wa Juba tarehe 3/10/2020 kuwa takriban miezi 53 kutoka kwenye waraka huo wa kikatiba, hivyo raia wangeanza kutawala Novemba 2021, na ilijulikana kuwa jeshi halingeruhusu hili na kisha kulivuruga. Hawatawawezesha raia kutawala mnamo Novemba mwaka huu, na jambo hili halikujulikana kwa kila mtu mwenye ufahamu ambaye anafahamu mambo kwa thamani yake. Hapo awali tulitoa jibu mnamo Septemba 23, 2019 kuhusu makubaliano ya waraka wa kikatiba, ambapo tulisema:

[- Serikali nchini Sudan kwa mujibu wa Waraka wa Katiba inakaribia kuundwa na pande mbili zenye mamlaka tofauti na utiifu wa kigeni unaokinzana, na jambo hili litaakisiwa katika kazi yao ya kutatua matatizo ya watu na usalama wa maisha yao, na kila mmoja wao kuwa na wasiwasi na kutumikia mwelekeo wanaofuata. Na kisha mmoja wao anasubiri mwingine atengwe kwa njia za ndani na nje... Kuanzishwa kwa mabaraza kama hayo nchini Sudan kunajulikana kuwa yameanzishwa tu kuhusiana na vipindi vya mpito na migogoro... hadi jeshi litakapoweza kupanga mambo ya serikali, kuvunja baraza, na kuweka rais wa nchi kutoka miongoni mwa maafisa wa jeshi], kisha tukaongeza: [- Kuhusu kile kinachotarajiwa, Amerika na Uingereza hazitaishi kwa utulivu. Maslahi yao ni tofauti na zana zao za ndani zinafuata, kwa hivyo pande zote mbili zitafanya kazi kumaliza harakati za mwingine! Kwa kufuatilia matukio ya sasa, kuchunguza masuala yanayohusiana nayo na kuchunguza taarifa za nje na ndani, hasa za maafisa wa Amerika na Ulaya, tunaweza kujua njia haswa ambazo pande zote mbili zitatumia kumnyanyasa mpinzani wake na kisha kumuondoa mamlakani.]

Hivi ndivyo ilivyotokea, kwa hivyo jeshi lilichochea mambo ambayo yalifungua njia kwa kile Burhan alichotangaza leo cha hali ya hatari nchini humo na taabu, shida na mateso zaidi kwa watu wa Sudan katika kutumikia mabwana wake makafiri wa kikoloni!

Enyi Waislamu: Si ajabu kwa maadui wa Uislamu kushindana ili kuidhoofisha nchi hii na watu, lakini jambo la kusikitisha ni kwamba haya yanafanywa na vibaraka wenye mafungamano na Uislamu na Waislamu, na Waislamu wananyamaza kimya huku wakiona na kusikia! Kisha wanalalamika juu ya ugumu wa maisha na uhaba wa chakula na vinywaji, kana kwamba hawajui Maneno Yake, Aliye Juu:

 (وَمَنْ أَعْرَضَ عَنْ ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنْكاً وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَى * قَالَ رَبِّ لِمَ حَشَرْتَنِي أَعْمَى وَقَدْ كُنْتُ بَصِيراً * قَالَ كَذَلِكَ أَتَتْكَ آيَاتُنَا فَنَسِيتَهَا وَكَذَلِكَ الْيَوْمَ تُنْسَى)

“Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu * Aseme: Ewe Mola wangu Mlezi! Mbona umenifufua kipofu, nami nilikuwa nikiona? * (Mwenyezi Mungu) atasema: Ndivyo vivyo hivyo. Zilikufikia ishara zetu, nawe ukazisahau; na kadhaalika leo unasahauliwa.” [TMQ Taha: 124-126].

Enyi Watu Wenye Nguvu na Uzuizi: Je, hakuna mtu miongoni mwenu mwenye busara? Hakuna kisingizio cha kuomba msamaha. Je, mnadhani Amerika na Uingereza wanazurura huku na kule katika ardhi zenu, na zana zao ni watu wanaoishi miongoni mwenu, bali ni viongozi wanaowaongoza kwenye udhalilishaji na udunishwaji, na bado mnatoa visingizio ili msimame dhidi yao?! Hawa ni makafiri wakoloni:

 (لَا يَرْقُبُونَ فِي مُؤْمِنٍ إِلّاً وَلَا ذِمَّةً وَأُولَئِكَ هُمُ الْمُعْتَدُونَ)

“Hawatazami kwa Muumini udugu wala ahadi; basi hao ndio warukao mipaka.” [TMQ At-Tawbah: 10]

(هُمُ الْعَدُوُّ فَاحْذَرْهُمْ قَاتَلَهُمُ اللَّهُ أَنَّى يُؤْفَكُونَ)

“Hao ni maadui; tahadhari nao. Mwenyezi Mungu awaangamizilie mbali! Vipi wanapotoka na haki?” [TMQ Al-Munafiqun: 4]. Na wale walio watiifu kwao miongoni mwa watawala katika nchi za Waislamu, haijuzu kuwategemea, na wao ni madhalimu na wapotovu.

(وَلَا تَرْكَنُوا إِلَى الَّذِينَ ظَلَمُوا فَتَمَسَّكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُمْ مِنْ دُونِ اللَّهِ مِنْ أَوْلِيَاءَ ثُمَّ لَا تُنْصَرُونَ)

“Wala msiwategemee wanao dhulumu, usije ukakuguseni Moto. Wala nyinyi hamna walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, wala tena hamtasaidiwa.” [TMQ Hud: 113]. Vipi hamuwezi kuchangamka?! Vipi heshima isikuchukueni kwa nguvu na ushindi mkawaondoa hao madhalimu, maadui wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake?! Vipi heshima ya Uislamu isikusukumeni ili muwakumbuke Maansari katika siku ya pili ya Aqabah walioinusuru dini ya Mwenyezi Mungu na waja wa Mwenyezi Mungu na wabebaji wa ulinganizi Wake?!

Hizb ut Tahrir inakulinganieni kuiunga mkono ili kusimamisha hukm ya Mwenyezi Mungu na kuwaondoa madhalimu wanaotawala nchi na watu kwa manufaa ya makafiri wa kikoloni. Njooni enyi watu wenye nguvu na uwezo, mumnusuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake ili kuiondosha hukmu ya kitaghut na kusimamisha hukmu ya Mwenyezi Mungu, ili mupate heshima hapa duniani na akhera, na huo ndio ushindi mkubwa. Njooni enyi watu wenye nguvu na uwezo, mumkumbuke Saad bin Muadh, ambaye kifo chake kilikitikisa Arshi ya Mwingi wa Rehema kwa heshima ya imani yake na nusra yake kwa dini ya Mwenyezi Mungu (swt). Imepokewa na Al-Bukhari kutoka kwa Jabir, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, nilimsikia Mtume (saw) akisema:

«اهْتَزَّ العَرْشُ لِمَوتِ سَعْدِ بْنِ مُعَاذٍ...» “Arshi (Kiti cha enzi cha Mwenyezi Mungu) ilitikisika kwa kifo cha Saad bin Muadh.”

Hizb ut-Tahrir inakualinganieni kuiunga mkono na kutowaogopa maadui wa Mwenyezi Mungu, na kumbukeni kauli ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, na Kauli yake ya kweli:

(إِنْ تَنْصُرُوا اللَّهَ يَنْصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ) “Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.” [TMQ Muhammad: 7]

(يَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَيُدْخِلْكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ وَمَسَاكِنَ طَيِّبَةً فِي جَنَّاتِ عَدْنٍ ذَلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ * وَأُخْرَى تُحِبُّونَهَا نَصْرٌ مِنَ اللَّهِ وَفَتْحٌ قَرِيبٌ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ)

“Atakusameheni dhambi zenu, na atakutieni katika Mabustani yapitiwayo na mito kati yake, na maskani nzuri nzuri katika Bustani za milele. Huko ndio kufuzu kukubwa.” [TMQ As-Saff: 12].

Enyi Waislamu! Enyi Watu Wenye Nguvu na Uwezo: Hizb ut-Tahrir inawaomba nusra yenu basi inusuruni na muikirimu.

 (يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ)

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [TMQ Al-Anfal: 24].

H. 18 Rabi' I 1443
M. : Jumatatu, 25 Oktoba 2021

Hizb-ut-Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu