Jumamosi, 19 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Enyi Majeshi katika Ardhi za Kiislamu!

Imetosha! Je, Munasubiri amri ya mtawala kuinusuru Gaza Hashem?
(Imetafsiriwa)

Kwa Majeshi katika Ardhi za Kiislamu: Je, hamna nyoyo za kuhisi, macho ya kushuhudia, na masikio ya kusikia? Je, hamuoni mito ya damu inayotiririka kutoka kwa watoto wa Waislamu huko Gaza? Je, hamuoni mauaji ya halaiki yakienea katika vijiji, miji na barabara? Je, hamuoni uharibifu wa nyumba, kulipuliwa kwa hospitali, na kuzuiwa kwa magari ya kubebea wagonjwa kuwasafirisha majeruhi, na kuwaacha kufa shahidi? Je, hamuoni ukatili wa Mayahudi duni unaoenea hadi kwa wanadamu, mawe, na miti? Udhalimu wa Mayahudi umefika Gaza na Ukingo wa Magharibi, na hata katika ardhi ya Palestina iliyokaliwa kwa mabavu 1948. Munasubiri nini? Bila shaka, munaona na kusikia kinachotokea. Je, hakuna mtu miongoni mwenu mwenye akili ya kuyaongoza majeshi ya Kiislamu, kushinda kwa ajili ya Uislamu na Waislamu kwa kulitokomeza umbile la Kiyahudi linalokalia kwa mabavu huko Palestina na kuirudisha yote kwenye ardhi za Uislamu? Je, ikiwa madhalimu wanampinga, je hapaswi kuwatawanye kwa nyuma? Je! hakuna mtu miongoni mwenu mwenye akili?

Yeyote anayesubiri amri ya watawala ni kama mtu anayenyoosha mikono yake kwenye maji, akitumaini kuwa yatamfikia mdomoni, na hilo halina hakika. Ni kama kungoja ngamia apite kwenye “tundu la sindano”. Watawala wanafuata amri za makafiri wakoloni walioanzisha dola ya Kiyahudi na kuwapa Ardhi Iliyobarikiwa. Kutarajia kheri au Jihad kutoka kwao ni kazi bure. Bali bora miongoni mwao ni yule anayehesabu mashahidi na waliojeruhiwa au kukimbilia dola za kikoloni za makafiri zinazoongozwa na Marekani kutafuta suluhisho, hata kama itamaanisha kujisalimisha kwa Mayahudi. Waliipongeza Mahakama ya Kimataifa ya Haki, labda angalau ingepata usitishaji vita, jambo ambalo haikufanya hivyo. Badala yake, ililitaka umbile la Kiyahudi liandikie mahakama hiyo ndani ya muda wa mwezi mmoja ikiwa limekomesha mauaji hayo! Uamuzi wao ulisema, (Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) iliamuru ("Israel" lazima pia izuie wanajeshi wake kufanya mauaji ya halaiki, kuzuia uchochezi wa kufanya mauaji ya halaiki, mashambulizi na uharibifu dhidi ya wakaazi wa Gaza; na lazima litekeleze " hatua za haraka na madhubuti” za kuhakikisha utoaji wa misaada ya kibinadamu na huduma za kimsingi zinazohitajika haraka huko Gaza.” Uamuzi huo pia ulitaka 'Israel' itoe ripoti kwa mahakama hiyo ndani ya mwezi mmoja kuhusu hatua zake za kutekeleza hatua hizo.'' (Al-Jazeera, 26/01/2024)). Ijapokuwa uamuzi wao ulikuwa dhaifu, lakini waliupongeza. Mnamo Januari 26, 2024, Al Jazeera iliripoti juu ya misimamo ya watawala katika nchi za Kiislamu iliupongeza uamuzi huo, na kuupokea ingawa ulikosa usitishaji vita vya uvamizi huo! Huu hapa ni mukhtasari wa majibu yaliyoripotiwa kwa makaribisho haya:

- Rais wa Uturuki alikaribisha uamuzi wa mahakama hiyo, na kuelezea kuwa ni azimio “lenye thamani”.

- Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Hussein Amir Abdollahian, alitoa wito kwa mamlaka za "Israel" kukabiliana na haki baada ya uamuzi wa mahakama.

- Jamhuri ya Kiarabu ya Misri ilithibitisha kwamba inatazamia kwa hamu uamuzi wa usitishaji vita mara moja wa mahakama na kusisitiza haja ya kuheshimu na kutekeleza maamuzi ya ICJ.

- Rais wa Algeria aliomba mkutano wa Baraza la Usalama kutoa "ufumbuzi wa kiutendaji" kwa maamuzi ya mahakama.

- Tunisia na Jordan ziliusifu uamuzi wa mahakama kama "wa kihistoria."

- Qatar, Kuwait, na Oman zilikaribisha uamuzi huo.

- Rais wa Pakistani aliukaribisha uamuzi wa mahakama kama uamuzi bora, akisisitiza kwamba jumuiya ya kimataifa na Baraza la Usalama lazima ziizuie "Israel" kufanya umwagaji zaidi wa damu huko Palestina.

- Ama kuhusu Mamlaka ya Palestina, Wizara ya Mambo ya Nje ya Palestina ilisema kwenye video moja, "Amri ya ICJ ni ukumbusho muhimu kwamba hakuna dola iliyo juu ya sheria," na haki hutekelezwa kwa kila mtu.

Ni kana kwamba uamuzi huu umekomesha uvamizi wa umbile la Kiyahudi huko Palestina, na hivyo kuukaribisha uamuzi huo! [قَاتَلَهُمُ اللهُ أَنَّى يُؤْفَكُونَ] “Mwenyezi Mungu awaangamizilie mbali! Vipi wanapotoka na haki?” [Al-Munafiqun:4].

Zaidi ya hayo, watawala hao wa Kiarabu waliharakisha kuitisha mkutano wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kujadili jinsi ya kushughulikia Gaza kutokana na kukaribisha kwao uamuzi wa mahakama hiyo. Wanavinjari kila suluhisho isipokuwa suluhisho lililonyooka lililowekwa na Mola Mlezi wa walimwengu wote, akifuatiwa na Mtume Wake (saw) na kuigwa na makhalifa walioongoka na walio baada yao hadi makafiri (kuffar) walipoiondoa Khilafah mwaka 1924. wakati huo, Palestina ikakabidhiwa Mayahudi.

Mwenyezi Mungu amrehemu Khalifa Abdul Hamid, ambaye alikataa pindi Herzl ilipotoa mamilioni ya dinari za dhahabu kwa Hazina ya Serikali kwa badali ya kuwaruhusu Mayahudi kuwa na makaazi huko Palestina, akisema, 'Palestina si mali yangu binafsi bali ni mali ya Umma wa Kiislamu. Watu wangu wameipigania nchi hii na kuimwagilia kwa damu yao. Mayahudi nawabaki na mamilioni yao, na endapo Khilafah itasambaratika, wanaweza kuichukua Palestina bila gharama yoyote.' Na hili ndilo lililotokea! Hawa hapa watawala wa Kiarabu wakati wa mkutano wao wa dharura, wakivinjari kila suluhu isipokuwa suluhu iliyonyooka, ambayo ni kuyakusanya majeshi kutoa nusrah (msaada) kwa Gaza Hashem na kuliondoa umbile vamizi la Kiyahudi linaloikalia kwa mabavu ardhi iliyobarikiwa ya Palestina! Mkutano wao haukwenda zaidi ya kuukaribisha uamuzi huo, wakisema kwamba ni 'fursa ya kuregesha sheria za kimataifa ambayo "Israel" imekuwa ikikiuka mara kwa mara, na ulazima wa kutumia vyema uamuzi huu kutoka upande wa Waarabu...' (Sky News Arabic , 28/01/2024).

Aidha, bado wanatafuta suluhu kutoka Marekani. Wapatanishi wa Kiarabu, Misri na Qatar, walikimbilia kwenye mkutano moja ulioitishwa na Marekani na Mayahudi ili kuvinjari kujisalimisha upya ili kuwaokoa mateka wa Kiyahudi wakati wa upinzani. Ujumbe wa "Israel", ukiongozwa na David Barnea, mkuu wa shirika la kijasusi la "Israel" Mossad, ulifika katika mji mkuu wa Ufaransa kufuatilia mazungumzo ya uwezekano wa mpango mpya wa kuwaachilia huru mateka zaidi walioshikiliwa huko Gaza. Ujumbe wa "Israel" umepangwa kukutana jijini Paris mnamo Jumapili jioni na wawakilishi kutoka Marekani, Qatar, na Misri, ambao wanaongoza juhudi za upatanishi wa pamoja ili kukamilisha na kuandaa makubaliano kati ya "Israel" na Hamas. Kwa mujibu wa maafisa wawili waandamizi wa Marekani, kuna dalili zinazoonekana za maendeleo kuhusu kile ambacho wapatanishi wa Marekani wanapendekeza, huku mfumo wa awali ukipendekeza "Israel" isitishe operesheni zake za kijeshi huko Gaza kwa miezi miwili ili kuachiliwa huru kwa duru mpya ya mateka, ambao idadi yao ni zaidi ya 100, wakiwemo wale wanaoshikiliwa na Hamas. (BBC, 28/01/2024) Marekani inawasukuma, na wao wanafuata nyuma!" [سَاءَ مَا يَحْكُمُون] “Hukumu mbaya hiyo wanayo hukumu.” [Al-Ankabut:4].

Hivi ndivyo watawala walivyo katika ardhi za Kiislamu. Basi chagueni njia yenu, enyi majeshi, mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, mkikimbilia moja ya matokeo mema mawili: Mafanikio ya dunia na ushindi wenye nusra unaonyanyua hadhi ya Ummah, na kufaulu Akhera yenye pepo pana mithili ya mbingu na ardhi, vilivyo andaliwa kwa ajili ya watu wema, ambayo kwayo mtainusuru Gaza, watetezi wake, na Palestina yote... Au mufuate njia ya watawala wenu, ambao hawatakunufaisheni hapa duniani wala kesho Akhera. Hali yenu itakuwa kama ya mtu anayeomba msaada wa moto kutoka kwenye barafu, bila ya mafanikio yoyote duniani na bila ya ulinzi kesho Akhera. Badala yake,

[لَهُمْ خِزْيٌ فِي الدُّنْيَا وَلَهُمْ فِي الْآخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ] “Hii ndiyo hizaya yao katika dunia; na katika Akhera watapata adhabu kubwa. [Al-Ma’ida:33]

Enyi Majeshi katika Ardhi za Kiislamu:

Wakumbukeni mababu zenu, mkumbukeni Salahudin aliyewashinda Makruseda baada ya kueneza ufisadi katika ardhi. Wakumbukeni Qutuz, Mabarbera, na majeshi ya Kiislamu yaliyowashinda Watatari. Kumbukeni kwamba haya yote yalitokea katika ardhi iliyobarikiwa ya Palestina. Kumbukeni haya yote na kuweni vizazi vyao. Fuateni nyayo zao, na muifanye Palestina, kwa mara ya tatu, kuwa kaburi la Mayahudi waliokufukuzeni kutoka katika nyumba zenu, pamoja na washirika wao waliojitokeza katika kukufukuzeni.

[إِنَّمَا يَنْهَاكُمُ اللهُ عَنِ الَّذِينَ قَاتَلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَأَخْرَجُوكُمْ مِنْ دِيَارِكُمْ وَظَاهَرُوا عَلَى إِخْرَاجِكُمْ أَنْ تَوَلَّوْهُمْ وَمَنْ يَتَوَلَّهُمْ فَأُولَئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ]

Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kufanya urafiki na wale walio kupigeni vita, na wakakutoeni makwenu, na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu. Na wanao wafanya hao marafiki basi hao ndio madhaalimu.” [Al-Mumtahina:9]. Haya kama Mwenye Nguvu na Mwenye Nguvu alivyosema,

[وَاقْتُلُوهُمْ حَيْثُ ثَقِفْتُمُوهُمْ وَأَخْرِجُوهُمْ مِنْ حَيْثُ أَخْرَجُوكُمْ] “Na wauweni popote mwakutapo, na muwatoe popote walipo kutoeni” [Al-Baqara:191].

Enyi Majeshi katika Ardhi za Kiislamu:

Je! hakuna mtu mwongofu miongoni mwenu? Kuwaongoza askari, hasa katika ardhi ya Kinana na Ash-Sham ambaye kwaye majeshi mengine yatamfuata, yakipiga takbira kwa Mwenyezi Mungu na Umma wote nyuma yao, wakiimba nusrah (ushindi) wa Mwenyezi Mungu (swt).

[إِنَّا لَنَنْصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ يَقُومُ الْأَشْهَادُ] “Hakika bila ya shaka Sisi tunawanusuru Mitume wetu na walio amini katika uhai wa duniani na siku watapo simama Mashahidi [Ghafir:51]. Imetosha! Enyi majeshi, na hakuna udhuru kwa mwenye kuomba msamaha, na hakuna uhalali kwa mwenye kulaani. Haitoshi kusaga meno yenu kwa hasira dhidi ya maadui zenu bila kuchukua hatua. Kama Mwenyezi Mungu Al-Hakim Al-Aziz alivyosema:

[قَاتِلُوهُمْ يُعَذِّبْهُمُ اللهُ بِأَيْدِيكُمْ وَيُخْزِهِمْ وَيَنْصُرْكُمْ عَلَيْهِمْ وَيَشْفِ صُدُورَ قَوْمٍ مُؤْمِنِينَ]

Piganeni nao, Mwenyezi Mungu awaadhibu kwa mikono yenu, na awahizi na akunusuruni muwashinde, na avipoze vifua vya kaumu ya Waumini [At-Tawba:14].

H. 18 Rajab 1445
M. : Jumatano, 31 Januari 2024

Hizb-ut-Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu