Jumatatu, 03 Safar 1447 | 2025/07/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Ewe Hamasa ya Uislamu ndani ya Umma wa Muhammad (saw)!
Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema: «لَيْسَ بِالْمُؤْمِنِ الَّذِي يَبِيتُ شَبْعَانَ وَجَارُهُ ‌جَائِعٌ إِلَى جَنْبِهِ» “Si Muumini anayelala ameshiba na hali jirani yake ana njaa.” (Imepokewa na Al-Hakim)

(Imetafsiriwa)

Miti na mawe yamelia kutokana na hofu iliyotusibu. Vifua vyetu vinatoa damu na maumivu, watoto wetu wanasisimka kutokana na njaa na kiu, wanawake wetu wanalia ili kuchochea wivu wa ulinzi wa waumini. Asiyeuawa kwa kupigwa mabomu hufa kwa njaa na kiu. Lakini maumivu ya usaliti ni mazito juu yetu kuliko milipuko ya mabomu, njaa, na kiu. Kaka na dada zenu mjini Gaza wanatangatanga bila malengo, bila makaazi, sauti zao zimenyamazishwa na udhaifu ulioletwa na njaa na kiu, baada ya kutoweka matumaini yote kwamba yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu atakuja kuwasaidia. Wanapiga kelele: Uko wapi Umma wa Uislamu? Iko wapi hamasa ya Dini? Uko wapi msaada wa Waumini?

Kinachovunja moyo ni “mitego ya kifo,” vile vituo vinavyoitwa kwa uwongo “vituo vya kibinadamu,” ambako watu wa Gaza huenda wakijua kwamba wanatembea kuelekea kwenye kifo, lakini njaa ya watoto wao na familia inawapeleka kwenye kifo kwa matumaini ya kupata angaa unga kidogo, hata kama unageuka kuwa mwekundu kwa damu yao!

Enyi Waislamu:

Je, munaweza kustahamili kuona watoto wa Gaza wakifa kifo cha polepole mbele ya macho ya wazazi wao, ambao hawawezi kufanya lolote isipokuwa kububujikwa na machozi na kumeza huzuni?

Je! nafsi zenu zinapata amani kwa kutazama matukio ya mauaji ya halaiki? Au sasa munaidhinisha usaliti wa watawala wenu, ambao walikabidhi hatima yenu na hatima ya Ummah wenu kwa Amerika na Mayahudi? Mnakubali kuuwawa kwetu, kuhamishwa kwetu, na kufuruswa kutoka kwa majumba yetu kwa mikono ya Amerika na Mayahudi?

Je, kuna usaliti wowote mkubwa kuliko kuifanya hatima ya watu wa Gaza kutegemea uamuzi wa Trump au Netanyahu?!

Je, kuna utelekezaji wowte mbaya zaidi kuliko kuwaacha watu na ndugu zenu kwa mauaji, njaa na kiu—ilhali mnao uwezo wa kuwanusuru?!

Je, kuna jinai kubwa zaidi kuliko majeshi kusalia kwenye kambi zao, ndege na virusha roketi vikiwa vimefungiwa kwenye sehemu zao, huku maadui wa Mwenyezi Mungu, waliolaaniwa wakiunajisi Msikiti wa Al-Aqsa na kumwaga damu zetu na kukiuks heshima yetu?

Ni udanganyifu wa unyonge uliopandwa ndani ya Umma na watawala wasaliti, mpaka majeshi ya Ummah, wanazuoni wake, na watu wake wakajisalimisha kwake. Je, jeshi la Misri kweli halina uwezo wa kupeleka tama la maji kwa watu wake na jamaa zake? Je, askari hodari wa jeshi la Jordan hawawezi kweli kufungua mpaka na kwenda kuukomboa Msikiti wa Al-Aqsa? Je, jeshi la Mujahid wa Pakistan kweli haliwezi kuteremsha mvua ya makombora juu ya umbile la watu waliolaaniwa, na kuwageuza kuwa uchafu wenye kutawanyika? Na vipi kuhusu majeshi ya Uturuki, Iraq, Hejaz, Algeria...n.k.? Je, hayana uwezo wa kuvunja mpaka na kuinusuru Palestina na mahali pa safari ya usiku ya Mtume (saw)?

Lo, ni huzuni kwa Umma wa Uislamu! Laiti ungeinuka na kuelekea Gaza na Ardhi Iliyobarikiwa kama vile makabila ya Sweida huko ash-Sham yalivyoinuka kuwalinda watoto wao na heshima yao, wale waliolaaniwa wangekimbia kwa hofu, wakihofia kisasi cha Umma wa Kiislamu kingewafikia.

Enyi Ummah wa Uislamu, enyi Ummah bora ulioletwa kwa ajili ya wanadamu:

Kuweni wakweli kwa Mwenyezi Mungu katika imani yenu. Kuweni wakweli kwa Mwenyezi Mungu katika nusra yenu. Kuweni wakweli kwa Mwenyezi Mungu katika msimamo wenu. Mnajua hakuna njia ya kusimamisha Dini yenu, kuwanusuru ndugu zenu, na kuikomboa Al-Aqsa yenu isipokuwa kwa kupindua viti vya watawala wenu waoga, wasaliti, kuvunja mipaka, na kuandamana hadi Msikiti wa Al-Aqsa.

Hivyo basi, hakuna kinachobakia kwa Umma wa Uislamu ila kuazimia jambo lake, kuhamisha majeshi yake, kupindua viti vya utawala vilivyosababisha njaa Gaza kwa ushirikiano na Mayahudi na Wamarekani. Hakuna kinachobakia isipokuwa kuitikia wito wa Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَا لَكُمْ إِذَا قِيلَ لَكُمُ انْفِرُوا فِي سَبِيلِ اللهِ اثَّاقَلْتُمْ إِلَى الْأَرْضِ أَرَضِيتُمْ بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا مِنَ الْآخِرَةِ فَمَا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فِي الْآخِرَةِ إِلَّا قَلِيلٌ * إِلَّا تَنْفِرُوا يُعَذِّبْكُمْ عَذَاباً أَلِيماً وَيَسْتَبْدِلْ قَوْماً غَيْرَكُمْ وَلَا تَضُرُّوهُ شَيْئاً وَاللهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ]

“Enyi mlio amini! Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya Akhera ni chache. (38) Kama hamwendi atakuadhibuni adhabu chungu, na atawaleta watu wengine, wala nyinyi hamtamdhuru chochote. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.” [Surat At-Tawbah 38–39].

Ewe Mwenyezi Mungu, tunakulalamikia kwa udhaifu wetu, mapungufu yetu, na udhalilifu wetu mbele ya watu. Ewe Mwingi wa kurehemu, Wewe ni Mola wa wanyonge, na Wewe ndiye Mola wetu. Unatuacha kwa nani? Kwa adui wa mbali anayetukemea, au kwa adui uliyemtia nguvu juu yetu? Ikiwa huna hasira na sisi, sisi hatujali. Msamaha wako ndio mkubwa zaidi kwetu. Tunajilinda kwa nuru ya Uso Wako, ambayo kwayo giza hutiwa nuru, na ambayo kwayo mambo ya dunia na Akhera yanasahihishwa, kutokana na kutushukia kwa hasira Yako au kutushukia ghadhabu Yako. Neema zote ni Zako mpaka Uridhike. Hakuna uwezo na nguvu ila Kwako.

H. 25 Muharram 1447
M. : Jumapili, 20 Julai 2025

Hizb-ut-Tahrir
Ardhi ya Baraka-Palestina

Yaliyomo ndani ya kifungu hichi: « Uhamisho au Ukombozi, enyi Umma wa Kiislamu?

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu