Jumatano, 11 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/13
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Serikali ya Mpito, Ambayo Inahusika katika Ajenda ya Mkoloni Kafiri

 Inataka Kutangaza Usawazishaji Mahusiano na Umbile la Kiyahudi

(Imetafsiriwa)

Katika taarifa kwenye akaunti yake kwenye wavuti, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan, Haider Badawi Sadiq, aliwataka Wasudan wapatane na (Israel), ikionyesha kwamba kuna mipango ya siri kati ya uongozi wa Khartoum na Tel Aviv, na msemaji huyo alimtaka kiongozi wa Baraza la Kuu na Waziri Mkuu kuheshimu watu wa Sudan, na kufichua kile kinachoendelea kwa siri kuhusu uhusiano kati ya nchi hizo mbili. (Gazeti la Al-Sharq Al-Awsat 19/20/20), na katika kukanusha kuthibitisha kile kinachoendelea kwa siri, Waziri mteule wa Mambo ya nje Omar Qamar al-Din alisema: (Wizara ya Mambo ya Nje ilipokea kwa mshangao taarifa za msemaji wa wizara hiyo, akisisitiza kuwa suala la uhusiano na (Israel) halikujadiliwa katika Wizara ya Mambo ya Nje. Kwa njia yoyote ile, Balozi Haider Badawi hakupewa jukumu la kutoa taarifa yoyote katika suala hili (gazeti la Al-Jarida 19/8/2020).

Kupitia ripoti hizi mbili, zinaweka wazi kuwa mazungumzo yanayozunguka chini ya meza kati ya serikali ya Sudan na umbile la Kiyahudi lililonyakua kibla cha kwanza kati ya vibla viwili, na Misikiti wa tatu Mtakatifu; Masra (eneo alilofanya Isra) Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Umbile hili limezama ndani ya damu tukufu ya Waislamu, na kukiuka utakatifu wa ndugu zetu Waislamu katika ardhi iliyonyakuliwa ya Isra na Mi'raj, ambalo lilithibitishwa na Waziri Mkuu wa umbile la Kiyahudi; Mmwagaji damu Netanyahu, kwenye ukurasa wake wa Twitter, ambapo aliandika hivi: ["(Israeli), na Sudan na eneo zima litapata faida kutokana na makubaliano ya amani na Sudan," kama Waziri wake wa Mambo ya Nje, Gabi Ashkenazi alivyokaribisha akisema: "Tangazo la Wizara ya Mambo ya nje ya Sudan linaonyesha mabadiliko ya kimsingi, baada ya miaka 53 tangu Kongamano la Khartoum wa LA mnamo 1967" (gazeti la Al-Sharq Al-Awsat (15240)].

Sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan tungependa kuweka wazi kwa watu wetu ukweli ufuatao:

Kwanza: Mtazamao wa Muislamu juu ya maswala, hafla, ukweli na maslahi unategemea msingi wa aqeedah ya Kiislamu; kwani hii dini yenye maadili kamili, Al-Haq (swt) anasema:

وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَمْراً أَنْ يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ وَمَنْ يَعْصِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالاً مُبِيناً﴿

“Haiwi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke kuwa na khiari katika jambo, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapo kata shauri katika jambo lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi hakika amepotea upotofu ulio wazi.” [Al-Ahzab: 36].

Na Swahaba mtukufu Rafi’ bin Khadij pindi Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alipokataza kukodisha ardhi kwa ajili ya ukulima:

«نَهَانَا رَسُولُ اللَّهِ ﷺ عَنْ أَمْرٍ كَانَ لَنَا نَافِعاً وَطَوَاعِيَةُ اللَّهِ وَرَسُولِهِ أَنْفَعُ لَنَا»

“Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ametukataza jambo ambalo kwetu lilikuwa na manufaa, lakini utiifu kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (saw) ndio wenye manufaa zaidi kwetu”.

Pili: Wajibu ulio katika shingo ya kila Muislamu ni kushikamana na kazi; ambayo kwayo ardhi ya Waislamu iliyonyakuliwa ya Palestina itakombolewa, na kila mahali, na kuwasaidia ndugu zake Waislamu dhaifu huko Palestina na kila mahali, Al-Haq (swt) anasema:

وَإِنِ اسْتَنْصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ﴿

“Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia” [Al-Anfal: 72]

Vipi basi mnawagura na kupatana na maadui wao na wenu?!

Tatu: Watawala vibaraka wa Sudan walianza kufuata njia ya kusawazisha mahusiano na umbile la Kiyahudi kwa kukutana na Al-Burhan na Netanyahu huko Entebbe mnamo 03/02/2020. Uhusiano wao na umbile la Kiyahudi kutoka chini ya meza hadi juu, ni mwendo wa kutekeleza mpango wa Amerika (Mpango wa Karne); Kuikabidhi Palestina yote kwa maadui wa Mwenyezi Mungu Mayahudi!!

Enyi Waislamu: Je! Mnaweza kuwaonyesha watawala hawa vibaraka msimamo unaompendeza Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (saw), msimamo ambao utawahakikishia kukaa mbali na lawama Siku ya Ufufuo Mkubwa, basi wapigeni watawala hawa kwa karatasi za khiyana zao nyeusi kwenye nyuso zao mbaya ili wajue; watumwa wa kafiri, kwamba sisi ni watumwa wa Mola wa mbingu na ardhi, tunajitenga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na khiyana zao, na tunaswali usiku na mchana, ili kurudisha mamlaka yetu yaliyonyakuliwa, na kumpa ahadi ya utiifu (Bay'ah) Khalifa wa Waislamu; atakaye safisha nchi kutokana na vibaraka wa Magharibi kafiri na khiyana zao, ili turegee kuwa Ummah bora uliotolewa kwa ajili ya watu? Na kamwe hilo halitawezekana bila ya majibu ya dhati ya watu wa nguvu na uthabiti kwa aqeedah yenu kwa mujibu wa njia ya Kisheria ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), basi na wajue kwamba wajibu wao ni mkubwa, hivyo nawasimame kwa ajili ya utiifu wa Mwenyezi Mungu (swt) na kwa ajili ya Pepo ambayo upana wake ni mbingu na ardhi iliyoandaliwa kwa ajili ya wachaMungu:

وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنْصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُمْ بِإِحْسَانٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي تَحْتَهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَداً ذَلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿

“Na wale walio tangulia, wa kwanza, katika Wahajiri na Ansari, na walio wafuata kwa wema, Mwenyezi Mungu ameridhika nao, na wao wameridhika naye; na amewaandalia Bustani zipitazo mito kati yake, wadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa.” [At-Tawba: 100].

H. 29 Dhu al-Hijjah 1441
M. : Jumatano, 19 Agosti 2020

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Sudan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu