Jumatatu, 23 Shawwal 1446 | 2025/04/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan

H.  23 Ramadan 1446 Na: Afg. H 1446 / 12
M.  Jumapili, 23 Machi 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
“Al-Wala wa-l-Bara” ni Hukmu Madhubuti ya Kiislamu na Kanuni Imara ya Kidini, na Haipaswi Kutolewa Kafara kwa ajili ya Maslahi ya Kitaifa
(Imetafsiriwa)

Adam Boehler, mwakilishi wa Kizayuni wa Trump katika masuala ya wafungwa, na Zalmay Khalilzad, mjumbe wa zamani wa Marekani katika masuala ya amani nchini Afghanistan, walikutana na Amir Khan Muttaqi, waziri wa mambo ya nje wa serikali inayotawala jijini Kabul. Kufuatia mkutano huu, serikali ilimwachilia huru mfungwa wa Kimarekani kama ishara ya nia njema. Amir Khan Muttaqi alitoa wito wa "mahusiano chanya ya kisiasa na kiuchumi na Marekani." Boehler alielezea hatua hii kama hatua kuelekea "kujenga uaminifu," na Khalilzad alisema kwamba "kuachiliwa huru kwa George Glezmann ni ishara ya nia njema ya Taliban."

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Afghanistan inauchukulia ushirikiano wa utawala wa Afghanistan na Marekani - ambayo kwa sasa iko katika vita vya moja kwa moja na Umma wa Kiislamu - kinyume na hukmu ya Kiislamu ya Al-Wala’ wa-l-Bara’, na inaulaani vikali. Kuhusiana na hili, nukta zifuatazo zinaletwa kwa ajili mazingatio ya Waislamu:

1. Kwa miongo kadhaa, Marekani imekuwa katika vita vya moja kwa moja vya kuendelea dhidi ya Umma wa Kiislamu. Tangu kuanza kwa mashambulizi ya kikatili ya dola ya Kiyahudi mjini Gaza, Marekani imetoa msaada kamili wa kijeshi, kiuchumi na kisiasa kwa dola hiyo. Kwa sasa, imeidhinisha dola ya Kiyahudi kuwafungulia Waislamu wa Gaza milango ya kuzimu ili kuwafukuza, na kwa kisingizio cha kuhakikisha usalama wake, mara kwa mara inalenga Syria na Lebanon vilevile. Aidha Marekani yenyewe imeanzisha mashambulizi makali ya anga katika ardhi ya Kiislamu ya Yemen na kusababisha kuuawa shahidi idadi kubwa ya Waislamu. Kwa hiyo, hairuhusiwi kwa Muislamu yeyote—awe mtu binafsi au dola—kujihusisha na mahusiano hayo na serikali zinazopigana vita kivitendo dhidi ya Uislamu.

2. Utawala wa Afghanistan unaodai kuwa ndio dola pekee ya Kiislamu katika ulimwengu wa Kiislamu na ulianzishwa kwa kuzingatia mihanga mitakatifu ya Mujahidina kutoka Afghanistan na kwengineko, unakiuka kanuni ya “uaminifu kwa waumini na kuwakana makafiri” (Al-Wala wal-Bara) katika muamala wake na serikali za kigeni. Kanuni hii ni hukmu ya thabiti ya Kiislamu na yenye kufungamanisha. Sera kama hiyo, kwa kweli, ni ukengeukaji kutoka kwa kanuni thabiti ya Kiislamu kwamba “vita na amani ya Waislamu ni moja,” na inawakilisha ubadilishaji wa Al-Wala’ wa-l-Bara’ kwa maslahi ya kitaifa—ikitoa kipaumbele kwa mambo yenye shaka juu ya yaliyo msingi, itikadi imara za Uislamu.

3. La kusikitisha zaidi ni kwamba raia wa Marekani anaachiliwa huru kwa msingi wa “nia njema,” huku makumi ya walinganiaji Waislamu wenye ikhlasi—waliofungwa kwa kutetea Khilafah kwa njia ya Utume na kujitahidi kupata umoja wa Ummah—wanabaki katika hali ngumu, wakitumikia vifungo virefu. Unafiki huu sio tu kwamba unagongana na hukmu za Kiislamu, bali pia ni ukiukaji wa wazi wa amri ya Mwenyezi Mungu (swt) na Sunna iliyothibiti ya Mtume (swa), ambaye alifundisha kwamba waumini wanapaswa kuwa imara dhidi ya makafiri na kuhurumiana baina yao.

Karne iliyopita imethibitisha mara kwa mara kwamba sera za kigeni zinazoegemea maslahi ya kitaifa zimeleta madhara makubwa zaidi kwa Umma wa Kiislamu, na kuwasukuma Waislamu katika mkanganyiko na mkwamo wa kisiasa. Kwa hiyo, serikali yoyote inayodai kuwa inawakilisha Uislamu lazima iegemeze sera yake ya kigeni kwenye Da’wah na Jihad, na hili si suala la ijtihad, lenye lengo la kutangaza dini na kusimamisha utawala wa Uislamu juu ya dini na mifumo mingine yote. Lengo hili linaweza kufikiwa tu pale Waislamu wanapoacha fikra za utaifa na sera za kimantiki (zinazoegemea maslahi), na kujitahidi kusimamisha Khilafah Rashida ya Pili kwa njia ya Utume—jambo ambalo ndilo suala la nyeti la Umma.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِ الْمُؤْمِنِينَ ۚ أَتُرِيدُونَ أَن تَجْعَلُوا لِلَّهِ عَلَيْكُمْ سُلْطَانًا مُّبِينًا]

“Enyi mlio amini! Msiwafanye makafiri kuwa ndio marafiki badala ya Waumini. Je, mnataka Mwenyezi Mungu awe na hoja iliyo wazi juu yenu?” [An-Nisa: 144]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Afghanistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-afghanistan.org/
E-Mail: info@hizb-afghanistan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu