Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  2 Muharram 1442 Na: 02 / 1442 H
M.  Ijumaa, 21 Agosti 2020

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Makubaliano ya Imarati na Mayahudi… Khiyana juu ya Msitari wa Unafiki Unaoonekana
(Imetafsiriwa)

Katika taarifa ya pamoja mnamo 13 Agosti 2020, Imarati, Amerika na umbile la Kiyahudi zilitangaza makubaliano baina ya Raisi wa Amerika Donald Trump, Waziri Mkuu wa umbile la Kiyahudi Netanyahu, na Mfalme Mtarajiwa wa Abu Dhabi Mohammed bin Zayed ya kufanya mahusiano kamili ya pande mbili kati ya umbile la Kiyahudi na Imarati. Mwenyezi Mungu Mtukufu asema kuhusu haya:

 (يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ لاَ تَتَّخِذُواْ الْيَهُودَ وَالنَّصَارَى أَوْلِيَاء بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاء بَعْضٍ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ إِنَّ اللَّهَ لاَ يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ * فَتَرَى الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ يُسَارِعُونَ فِيهِمْ يَقُولُونَ نَخْشَى أَن تُصِيبَنَا دَائِرَةٌ فَعَسَى اللَّهُ أَن يَأْتِيَ بِالْفَتْحِ أَوْ أَمْرٍ مِّنْ عِندِهِ فَيُصْبِحُواْ عَلَى مَا أَسَرُّواْ فِي أَنفُسِهِمْ نَادِمِينَ)

“Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu. Utawaona wale wenye maradhi nyoyoni mwao wanakimbilia kwao wakisema: Tunakhofu yasitusibu mabadiliko. Huenda Mwenyezi Mungu akaleta ushindi au jambo jingine litokalo kwake wakawa wenye kujuta kwa waliyo yaficha katika nafsi zao.” [Al-Ma’ida: 51-52].

Ummah wa Kiislamu haukushangazwa na khiyana hii iliyo tangazwa na Imarati, na vipi utashangazwa wakati ambapo umeonja kutoka kwa watawala hawa vibaraka Ruwaibidha, aina kadha wa kadha za khiyana, uhaini, utovu wa dini na ukosefu wa ari, mengi mno kiasi cha kukadiriwa na makumi ya vizazi?! Hakika, watawala wa Dola za Ghuba, hususan, wamefanya kila juhudi katika miaka ya hivi karibuni kuufanya ulimwengu ujue nia yao ya kuufuata mpango wa Amerika wa kusawazisha mahusiano na umbile la Kiyahudi. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

 (وَمِنَ الْأَعْرَابِ مَن يَتَّخِذُ مَا يُنفِقُ مَغْرَماً وَيَتَرَبَّصُ بِكُمُ الدَّوَائِرَ عَلَيْهِمْ دَائِرَةُ السَّوْءِ وَاللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ)

“Na katika Mabedui hao wapo wanao fikiri kuwa wanayo yatoa ni gharama ya bure, na wanakungojeleeni mambo yakugeukieni. Mageuko maovu yatakuwa juu yao! Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia Mwenye kujua.” [At-Tawba: 98].

Ujasiri huu uliolaaniwa juu ya Ardhi Iliyo Barikiwa (Palestina) unaweza tu kukomeshwa na Ummah wa Kiislamu kupitia hatua uliochukua katika kuukomboa Msikiti wa Al-Aqsa kutokana na uchafu wa Makruseda, ni hatua hiyo hiyo ndio Ummah unasifia ushujaa wake, na ni hatua hiyo hiyo ambayo kwayo Ummah unaendelea kuwapa watoto wao majina ya Umar, Khalid na Salahuddin… Kila wakati Ummah wa Kiislamu ulipotaka kuikomboa Bait ul-Maqdis (Jesrusalem), uliiendea na majeshi ya Khilafah. Lakini yako wapi majeshi ya Khilafah leo?

Enyi Waislamu:

Tunajua kwamba namna Wamagharibi watakavyourudia "Mchezo: Mtawala wa Kiislamu anayetangaza kuiteka kwake Palestina", imani yenu kuwa umbile la Kiyahudi linakaribia kutoweka mikononi mwa Ummah wa Kiislamu haitabadilika. Bali, tunajua kwamba msimamo wenu halisi ni ule ambao Khalifah Abdul Hamid, Mwenyezi Mungu amrehemu, aliandika kwa kusema: "…maadamu niko hai, mkono wangu kukatwa na kiwembe sio uchungu zaidi ya kushuhudia Palestina ikitenganishwa kutoka katika dola ya Khilafah na hili halitatokea."

Hapa tunalirudia swali: Yako wapi majeshi ya Khilafah leo?!

Jibu lake ni kuwa majeshi ya Khilafah yatazaliwa mara tu baada ya tangazo la ahadi ya utiifu (Bay'ah) kwa Khalifah, hii ni kwa sababu Ba'yah huanzishwa pekee na wale wanaoweza kumpa Khalifah jeshi ambalo kwalo atalinda Dar al-Islam (Makaazi ya Uislamu) na kufungua nchi, kwa njia ambayo Maanswari walisema katika bay'ah ya pili ya Aqabah, ambapo dola ya kwanza ya Kiislamu ilisimamishwa. Albara bin Ma’roor alimwambia Mtume (saw):

"والذي بعثك بالحق لنمنعنك مما نمنع منه أزرنا، فبايعنا يا رسول الله، فنحن والله أهل الحرب"

“Naapa kwa Yule aliyekutumiliza kwa haki, tutakulinda kama tunavyolinda watoto wetu, hivyo basi chukua ahadi yetu ya utiifu ewe Mtume wa Mwenyezi, Naap kwa Mwenyezi Mungu sisi ni watu wa vita.”

Hivyo basi, leo na wakati huu tunaamsha ari ya Uislamu katika watu wanaomiliki nguvu na uwezo, kufanya kazi na Hizb ut Tahrir ili kutoa Bay'ah kwa imam wa Waislamu "khalifah", ili pamoja naye, wakiondoe kisu kilicho kitwa mgongoni mwa Ummah wa Kiislamu, nacho ni watawala makhaini, kisha pamoja naye, wakiondoe kisu kilicho kitwa moyoni mwa Ummah wa Kiislamu, nacho ni umbile la Kiyahudi, mnyakuzi wa Ardhi Iliyo Barikiwa. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تَنصُرُوا اللَّهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ)

“Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.” [Muhammad: 7].

Mh. Salah Eddine Adada
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizbuttahrir.today
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu