Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
H. 28 Safar 1442 | Na: 1442 H / 006 |
M. Alhamisi, 15 Oktoba 2020 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Serikali ya Kyrgyz Inashirikiana na Serikali ya Uzbek katika Vita Dhidi ya Uislamu na Waislamu
(Imetafsiriwa)
Kulingana na habari zilizochapishwa na tovuti ya Habari za Asia ya Kati mnamo 13/10/2020 chini ya kichwa: "Kyrgyzstan yamkabidhi Muislamu mwingine kwa Uzbekistan), mnamo Septemba 15, 2020 M, serikali ya Kyrgyz ulimfukuza kaka wa Kiislamu Karimov Shuhrat Torsunovich (КАРИМОВ ШУХРТ) na kumkabidhi kwa mamlaka za serikali ya Uzbek. Kaka huyu Muislamu anasubiri mateso makali ambayo serikali nchini Uzbekistan unajulikana kwayo. Karimov Shuhrat alizaliwa mnamo Oktoba 1, 1967 M katika Wilaya ya Qoʻrgʻontepa, jimbo la Andijan.
Ama kaka yake, Karimov Shaukat Tursunovich, ambaye alizaliwa mnamo 1964, alifungwa na serikali ya Uzbek kwa mashtaka ya kidini mnamo Februari 1999. Walimtesa sana wakati wa uchunguzi. Jamaa zake walikwenda kwa mashirika ya haki za binadamu, mashtaka ya umma, na mahakama, kuwauliza haki, lakini juhudi zao ziliambulia patupu. Mahakama ilimhukumu kifungo cha miaka 9, ingawa mashtaka dhidi yake hayakuthibitishwa! Na pindi kifungo chake kilipomalizika mnamo 2008 M, waliongeza miaka 3 kwake, na baada ya hapo, waliongeza tena miaka mingine 3!
Na kwa hivyo, baada ya kifungo cha miaka 13, kuongezwa na kuteswa vibaya, Shawkat aliuawa shahidi mnamo 2012 M katika magereza ya Uzbekistan, Tunamhesabu hivyo, na hatumtakasi mtu yeyote mbele ya Mwenyezi Mungu, na kurudisha maiti kwa familia yake!
Ama mamake Karimov Shawkat, Bi Sa`dat Khan Karimova, baada ya misiba hii na kutengana huku kwa kuhuzunisha kwa mtoto wake, aliugua sana, ikifuatiwa na mshtuko wa moyo, na moyo wake wenye huzuni ukasimama kupuma na kufariki miezi sita baada ya kifo cha mtoto wake.
Kwa Karimov, aliwekwa pia (baada ya kaka yake) chini ya usimamizi wa idara ya usalama, ambayo ilimlazimisha kuondoka Uzbekistan kwenda Kyrgyzstan mnamo 2003; Katika mwaka huo huo alimuoa Bi Babarbuyeva Rahat Abi Bakr Sidikovna.
Shahrt hakuwezi kurudi tena kwa familia yake nchini Uzbekistan, kwani kaka yake Shawkat alimpenyezea habari wakati huo kwamba, "Usije Uzbekistan, kwa sababu ikiwa utakuja hapa wanakusudia kukutesa sana."
Mnamo Septemba 2019, Shuhrat alikamatwa katika uwanja wa ndege huko Bishkek, mji mkuu wa Kyrgyzstan, na Idara ya Usalama wa Kitaifa, alipokuwa njia akielekea Uturuki kupata matibabu. Baada ya taratibu za uchunguzi, kesi yake ilipelekwa mahakamani, na mnamo Juni 3, 2020, Jaji Aipek Ernesoglu alimhukumu kifungo cha miaka mitano gerezani, kisha akaachiliwa kutoka kwa chumba cha mahakama mara moja kwa sababu ya msamaha wa jumla. Lakini, alikamatwa tena kwa ombi la Mwendesha Mashtaka ya Umma kabla ya kuondoka kwenye chumba cha mahakama ya Pervomaysky. Walimweka kizuizini katika kituo cha kizuizini huko Bishkek, kwa kisingizio kwamba Uzbekistan inadai afukuzwe, na kwamba mamlaka za Kyrgyz zinapaswa kufikiria kumpeleka au la.
Na mnamo Septemba 7, 2020 M, Shuhrat alihukumiwa, na ingawa ulimwengu unajua unyama wa serikali ya Uzbek kwa wafungwa wa kisiasa, mahakama ya Kyrgyzstan iliamua kwamba Shuhrat anastahiki kufukuzwa kwenda Uzbekistan. Ukiukaji dhidi ya Shawkat mahakamani pia ulikuwa mwingi. Kwa mfano, ingawa wakili wake hakuwepo, mahakama ilileta wakili wa zamu na kumsomea uamuzi bila ya uwepo wa wakili wake.
Mnamo Septemba 15, 2020 M, mamlaka nchini Kyrgyzstan ilimhamisha Shuhrat kwenda Uzbekistan, hata kabla ya uamuzi uliotolewa mnamo Septemba 7, 2020 kuanza kutekelezwa.
Kulingana na yale yaliyosemwa katika barua ambayo mke wa Shuhrat alimwandikia Rais wa Kyrgyz Surenbai Jinbekov, ambapo alielezea kwamba haki za mumewe zilikiukwa, na alitaka rais wa Kyrgyz aiweke kesi hii chini ya udhibiti wake na ampe mumewe uraia wa Kyrgyz. Hususan kwa kuwa uraia nchini Kyrgyzstan hupewa mtu yeyote anayetoka nje ya nchi ikiwa ni wa asili ya Kyrgyz, na ambaye mama yake anajulikana kuwa Mkyrgyz. Leo, baada ya misiba mfululizo, na mithili ya mama yake marehemu, mke wa Shuhrat, ambaye ni mama wa watoto wake wanne, aliugua ugonjwa wa moyo. Ama nyoyo za watawala wa Kyrgyzstan na Uzbekistan, zingali kama mawe, bali ni ngumu zaidi.
Kwa hivyo tunaweza kuona kutokana na dhuluma hii yote iliyoratibiwa! Kwamba serikali ya Kyrgyz inashirikiana na serikali ya Uzbek katika vita dhidi ya Uislamu na Waislamu. Serikali ya zamani wa Kyrgyz iliwasalimisha wahamiaji wengi wa Kiislamu kwa mamlaka za serikali ya Uzbek.
Hakika serikali za kidhalimu, pamoja na matendo yao, hujaribu kuzima nuru ya Mwenyezi Mungu (swt), na Mwenyezi Mungu anakataa isipokuwa nuru yake itimizwe hata kama makafiri wanachukia. Na Mwenyezi Mungu akipenda, dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume ambayo itasimama hivi karibuni, itawalipizia kisasi wale waliodhulumiwa na watawala madhalimu, na hakika kesho tutaiona hivi karibu.
Ama sisi katika Hizb ut-Tahrir, tunaziomba nyoyo za Waislamu, juu yao watu wenye nguvu na ulinzi, wautazame Ummah wao na wakumbuke siku nzito ambayo hakuna kutoroka kutoka kwa mateso, siku ambayo Mwenyezi Mungu (swt), atawauliza kwa kile Alichowakabidhi. Tunatoa wito kwa nyoyo za watu wenye nguvu na ulinzi kuacha kuunga mkono madhalimu na kurudisha utawala kwa Ummah kwa Kiislamu na kusimamisha Khilafah Rashida iliyoahidiwa. Ikiwa hawatafanya hivyo, basi sisi Ummah wa Kiislamu tutakuwa wapinzani wao Siku ya Kiyama, na Mwenyezi Mungu (swt) atawabadilisha na wale ambao ni bora kuliko wao. Tunamwamini Mwenyezi Mungu (swt). Mwenyezi Mungu (swt) asema:
]وَمَن يَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّهِ فَهُوَ حَسْبُهُ إِنَّ اللَّهَ بَالِغُ أَمْرِهِ قَدْ جَعَلَ اللَّهُ لِكُلِّ شَيْءٍ قَدْراً]
“Na anaye mtegemea Mwenyezi Mungu Yeye humtosha. Hakika Mwenyezi Mungu anatimiza amri yake. Mwenyezi Mungu kajaalia kila kitu na kipimo chake.” [At-Talaq: 3].
Mh. Salah Eddine Adada
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari
Ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizbuttahrir.today |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info |