Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
H. 7 Rabi' II 1443 | Na: 1443/015 |
M. Ijumaa, 12 Novemba 2021 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir Watembelea Ubalozi wa Uswidi jijini Beirut Kutaka Kusitishwa kwa Uhamisho wa Odiljon Jalilov hadi Uzbekistan
(Imetafsiriwa)
Mnamo siku ya Ijumaa, tarehe 12/11/2021, Ujumbe wa Hizb ut Tahrir ukiongozwa na Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir, Mh. Salah Eddine Adada, akifuatana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir nchini Lebanon Mh. Saleh Salam, ulitembelea Ubalozi wa Ufalme wa Uswidi jijini Beirut na kukutana na Msaidizi katika Ubalozi huo kuonesha uzito wa uamuzi wa kumfukuza Odiljon Jalilov kutoka Sweden na kumpeleka Uzbekistan; kwani uamuzi huo wa kumfukuza Jalilov unawakilisha tishio halisi kwa maisha yake. Ujumbe huo ulieleza kwamba Uzbekistan ina historia ndefu na yenye sifa mbaya ya ukandamizaji dhidi ya wapinzani wa kisiasa, na haswa mateso ya wanachama wa Hizb ut Tahrir hadi kufa. Ujumbe huo uliwasilisha sampuli ya picha zinazoonyesha ishara za mateso ya kutisha kwa wale waliouawa chini ya mateso nchini Uzbekistan.
Ujumbe huo pia ulitoa Taarifa kwa Vyombo vya Habari iliyotolewa na Hizb ut Tahrir nchini Uswidi inayoonyesha vyombo vya habari vya Uswidi na Ulaya na mashirika ya kutetea haki za binadamu uzito wa kile ambacho Ndugu Odiljon Jalilov atakabiliana nacho endapo uhamisho wake kwenda Uzbekistan utatekelezwa. Ujumbe huo pia uliwasilisha makala ya magazeti ya kimataifa yanayothibitisha ukweli wa ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na serikali ya Uzbekistan dhidi ya wanachama wa Hizb ut Tahrir na familia zao.
Tungependa kutaja kwamba kupuuza maombi yote ya kibinadamu na mamlaka za Uswidi na kusisitiza kufukuzwa na kukabidhiwa kwa ndugu yetu, Odiljon Jalilov, kwa utawala dhalimu wa Uzbekistan kunawakilisha tishio la kweli kwa maisha yake ambayo mamlaka za Uswidi zitawajibika.
Mh. Salah Eddine Adada
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizbuttahrir.today |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info |