Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
H. 28 Muharram 1443 | Na: 1443 H / 025 |
M. Jumanne, 01 Machi 2022 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Khilafah ni Tunda Linaloweza Kufikiwa, Basi Harakisheni katika Kulichuma, Enyi Waislamu!
(Imetafsirirwa)
Mwezi wa Rajab huregea kila mwaka na huleta kumbukumbu nyingi zinazowafurahisha Waislamu, lakini mwezi wa Rajab unabeba kwa kizazi hiki cha Umma wa Kiislamu kumbukumbu maalum ambayo haiwezi kupuuzwa, ambayo ni kumbukumbu ya kuvunjwa Khilafah katika mwezi wa Rajab wa mwaka 1342 Hijria. Kuvunjwa kwa Khilafah lilikuwa ni janga lililofungua mlango wa msururu wa maafa yaliyoupata Umma wa Kiislamu katika kipindi cha karne iliyopita.
Kwa vile Umma wa Kiislamu bado unakabiliwa na matokeo ya moja kwa moja ya janga hili, ni lazima kukumbuka kumbukumbu hii hadi hali hii irekebishwe na Waislamu warudishe dola inayowalinda na maovu ya maadui, kuwahifadhi na machungu ya majanga, na kuwarudishia hadhi yao miongoni mataifa.
Kwa vile Kafiri mkoloni Magharibi ilifanikiwa katika njama zake za kuivunja Khilafah ili kuwatawala Waislamu na ardhi zao; iliufanyia Umma huu wa Kiislamu aina kali kabisa za dhulma na madhara, kiasi kwamba hali ya Ummah ni kana kwamba umewekwa kwenye kiti cha kuhojiwa katika chumba cha mateso! Kila aina ya madhara ya kimada yaliwekwa juu yake. Iliwaua watoto wake, ikavunjia heshima yake, ikapora mali yake, ikapora ardhi yake, ikaichana ardhi yake, na ikachochea fitna kati ya watu wake. Pia ilileta aina mbalimbali za madhara ya kimaadili juu yake. Ilizishambulia hukmu za Shariah ya Kiislamu, ikamtukana Mtume wake, tunaomba ulinzi kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na ikatukana utakatifu wake na usafi wake, na ikadunisha hadhi yake kufikia hadi ambapo mashetani watu miongoni mwa wahalifu na majambazi wakaichukua kama shabaha ya ulafi wao. Tunachokiona leo ni ushupavu dhidi ya watoto wa Kiislamu katika pembe zote za dunia, kuanzia utekaji nyara, utesaji, ukamataji, upotezaji, mauaji, njaa na kutelekezwa. Ni kwa sababu tu ndege hawa wasio na hatia na familia zilizo hatarini hazina mlinzi; Imamu ambaye atakuwa khalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na kwa njia yake, ambaye atawakusanya watu wa Ummah huu na mashujaa wake, na kuelekeza hasira zao kwa wahalifu waliowadhulumu, hivyo kuwasahaulisha minong'ono ya Shetani. Kutoka kwa Abu Hurairah, kutoka kwa Mtume (saw) amesema:
«إِنَّمَا الإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ»
“Hakika Imam ni ngao, watu hupigana nyuma yake na hujihami kwayo”
Uasi uliofuatana wa Umma wa Kiislamu umethibitisha kwamba unasubiri fursa na hauzikosi. Iwapo mtu ataonekana kujiamini katika uwezo wake na kutabanni maslahi yake, Ummah utamwamini na kuungana karibu naye na utashirikiana naye kujaribu kuregesha mamlaka yake yaliyochukuliwa kutoka kwao. Wale wanaozijua hali za Umma wa Kiislamu, hata miongoni mwa maadui zake, wanafahamu vyema kwamba Ummah baada ya kila jaribio la ukombozi, hata ukishindwa, utambuzi wa ukubwa wa chuki ya Magharibi na vibaraka wake dhidi yake, na kiwango cha haja yake ya kung'oa ushawishi wake kutoka kwa ardhi yake itakusanyika katika kumbukumbu yake. Kwa hiyo, uhalisia wa hali ya Ummah hivi leo ni kwamba unapambana na minyororo yake ili kujinasua kutoka kwayo, kusaga meno yake kwa hasira, na kuangalia machoni mwa muuwaji wake, na kumtishia matokeo mabaya. La muhimu zaidi ni kwamba Ummah umeitabanni Khilafah kama mfumo ulioletwa na Uislamu, na kila kinachopingana nayo ni haramu.
Umma wa Kiislamu leo uko katika mgongano wa wazi na Magharibi na hadhara yake. Katika nchi za Kiislamu Umma wa Kiislamu ulijaribu kugeuza meza juu ya hali ya ukoloni katika kile kilichoitwa Mapinduzi ya Kiarabu, na Magharibi haikuweza kukabiliana na uasi huu isipokuwa kwa chuma na moto, na kupata tu suluhisho la muda mfupi kwa ajili yake. Katika nchi za Magharibi, ambako Waislamu walihamia, jamii nzima za Waislamu kwa jumla na familia zao haswa ilikuwa vigumu kuwaoanisha katika hadhara ya Magharibi na ukafiri, upotovu na uasherati inayobeba. Wamagharibi walipoteza akili na kung'oka meno na wakachukua hatua iliyodhihirisha kufilisika na kukata tamaa kwake kutoka kwa Waislamu, jambo ambalo ni jaribio la kuwalazimisha Waislamu katika nchi zao na nchi za Magharibi itikadi na maisha ya kisekula kwa nguvu katika nchi zao na katika nchi za Magharibi, hata kupitisha kwa nguvu maamuzi yanayokinzana na rai jumla kwa uwazi. Rais wa Marekani aliwachochea watu wake na ulimwengu dhidi ya Waislamu, na rais wa Ufaransa akayabana maisha ya kibinafsi ya familia za Kiislamu nchini Ufaransa.
Serikali za Scandinavia zilichochea maamuzi ya kuwaondoa watoto wa Kiislamu na kuwaficha kutoka kwa familia zao. Watawala wa Familia ya Saud waliwafunga wanazuoni na kisha kufungua ardhi ya Misikiti Miwili Mitakatifu kwa nzige wasio na maadili wa wachezaji wa kike na wa kiume. Nchi za Ghuba ya Kiarabu ziliwaiga na kutangaza usawazishaji mahusiano na umbile la Kiyahudi lililonyakua Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina. Hii inaashiria kiwango cha kuchanganyikiwa na kufilisika kwa Wamagharibi katika kuuyeyusha Ummah ndani ya hadhara yake na kushindwa kwake kuunyenyekesha.
Harakati hii ya Ummah haimaanishi kwamba hauwezi kuhadaiwa na miradi iliyotiwa sumu, katika korido za siasa, na kwa njia za chukua na omba, na mitego ya mantiki ya Machiavelli, ambayo matokeo yake ni ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na hasara ya dunia na Akhera. Hautaokolewa kutokana na mitego hii au imani kwa vibaraka isipokuwa kwa kupitia wenye ikhlasi na uwezo wanaoweza kuushughulikia na ukawasikiliza wao na ushauri wao. Kwa wakati huu, wao ndio waundaji wa dhati wa rai jumla. Tunawageukia na kuwaonya kwa Mwenyezi Mungu (swt), wasisite kufichua njama, na wasiufanye Umma ufuate vibaraka na wasaliti, na wala wasiupotoshe Ummah kutojana na kadhia yake nyeti.
Hapa, Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir inatoa wito kwa wanahabari na vyombo vyote vya habari, hususan wale watiifu, wenye nia ya dhati ya kuunyanyua Ummah wa Kiislamu kutoka katika hali ya unyonge uliomo. Tunakualikeni muwe wenye kuinusuru haki na kuwa kinara wa kheri, hivyo basi shirikini katika kuangazia amali za kampeni hii ya kulingania kuregeshwa kwa Khilafah kwa njia ya Utume.
Ama kwa watu wenye nguvu na ulinzi, wao ndio wa mwisho kusimama baina ya Ummah na utambuzi wa kurudi kwa Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Ummah uko tayari kwa umoja, Khilafah, ujenzi na uhamasishaji. Unakosa tu wale watakaotoa eneo salama kwa Uislamu, ili liwe mahali pa kuzingatia ambapo kutoka hapo utaenea hadi ulimwengu mzima. Hili halitapatikana isipokuwa Nusra (msaada wa kimaada) upatikane na wale wenye uwezo wa kung'oa mamlaka kutoka mikononi mwa wasaliti na vibaraka na kuyarejesha kwa Umma wa Kiislamu.
Mwenyezi Mungu (swt) asema:
(وَالَّذِينَ آوَواْ وَّنَصَرُواْ أُوْلَئِكَ هُمُ الْمُؤْمِنُونَ حَقّاً)
“...na walio toa mahala pa kukaa na wakanusuru, hao ndio Waumini wa kweli.” [Al-Anfal: 74].
#الخلافة_101 #أقيموا_الخلافة
#ReturnTheKhilafah #YenidenHilafet
#TurudisheniKhilafah
Mhandisi Salah Eddine Adada
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizbuttahrir.today |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info |