Jumatano, 15 Dhu al-Hijjah 1446 | 2025/06/11
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  10 Dhu al-Hijjah 1446 Na: H 1446 / 122
M.  Ijumaa, 06 Juni 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Pongezi kwa Idd Al-Adha Iliyobarikiwa 1446 H

(Imetafsiriwa)

Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, La Ilaha Illallah, Allahu Akbar, Allahu Akbar wa lillahi Al-Hamd

Hizb ut Tahrir inatoa pongezi na baraka nyingi zaidi kwa Umma wetu mpendwa wa Kiislamu, wenye subira na wenye kukubali malipo licha ya maafa na majanga yote unaopitia, maafa na majanga ambayo ni mzigo mzito hata kwa kundi lililo imara zaidi la wanadamu, hususan watu wetu wenye subira mjini Gaza na katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, katika Sikukuu ya Idd ul-Adha. Tunamuomba Mwenyezi Mungu azijaalie siku za Idd hii kuwa ni utulivu katika nyoyo zao na wanyanyuliwe daraja mbele ya Mola wa walimwengu wote. Iddi ni ambayo Al-Mustafa (saw) amesema, «إِنَّ أَعْظَمَ الْأَيَّامِ عِنْدَ اللهِ يَوْمُ النَّحْرِ» “Siku kubwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu ni siku ya kukichaja”

Vile vile nina furaha kutoa pongezi zangu, pamoja na pongezi za Mkuu wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na ndugu na dada wote wanaofanya kazi katika idara na vitengo vyake, kwa Amir wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa, Ata bin Khalil Abu al-Rashtah (Mwenyezi Mungu amhifadhi). Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) kwamba Umma hivi karibuni utatoa kiapo cha utiifu kwake, kiapo cha utiifu kwa Khilafah, ambacho kinahitimisha zama za utawala dhalimu ambao Ummah unaishi chini yake, na pamoja naye kuanza zama za ushindi, ukombozi, na tamkini katika kutimiza maneno ya Mwenyezi Mungu (swt):

[وَعَدَ اللهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُم فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْناً]

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao.” [An-Noor: 55]

Idd al-Adha inakuja mwaka huu wakati Umma wa Kiislamu unateseka zaidi kuliko hapo awali kutokana na moto wa maadui zake. Waislamu wanauawa katika makumi ya maelfu mbele ya macho ya dunia nzima, na ndani ya umbali wa pua na mdomo kwa majeshi ya Ummah yaliyowekwa kwenye kambi zao, huko Palestina, Sudan, Kashmir, Ash-Sham, Yemen na Lebanon kwa makombora, ndege, droni, vifaru na aina zote za silaha. Viungo vya mwili vimetapakaa, miili inachomwa moto, na wanawake, wajane na yatima wanalia kuomba msaada, lakini hakuna msaidizi au mwokozi! Hali haivumiliki.

Ummah kwa sasa una haja kubwa kwa majeshi yake na maafisa wake kukusanyika ili kuitikia wito wa wajibu, ili wapate heshima ya kuunusuru Uislamu na Waislamu, na wakusanyike kwenye Hawdh pamoja na As’ad wawili (maswahaba wa Mtume), Mwenyezi Mungu awe radhi nao, mbele ya Al-Mustafa (saw). Hakuna siku zinazopendwa zaidi na Mwenyezi Mungu kuliko siku hizi za kuwa siku za Nusra (ushindi), utukufu, na tamkini. Mtume (saw) akasema:

«مَا مِنْ أَيَّامٍ الْعَمَلُ الصَّالِحُ فِيهِنَّ أَحَبُّ إِلَى اللهِ مِنْ هَذِهِ الْأَيَّامِ الْعَشْرِ. فَقَالُوا: يَا رَسُولَ اللهِ، وَلَا الْجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللهِ؟ فَقَالَ رَسُولُ اللهِ ﷺ: وَلَا الْجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللهِ، إِلَّا رَجُلٌ خَرَجَ بِنَفْسِهِ وَمَالِهِ فَلَمْ يَرْجِعْ مِنْ ذَلِكَ بِشَيْءٍ»

Hakuna siku ambazo amali njema hupendeza zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko siku hizi kumi." Alipoulizwa kama hata jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu haipendezi, alijibu: "Hata jihad katika Njia ya Mwenyezi Mungu, isipokuwa mtu anapotoka kwa nafsi yake na mali yake na akapoteza uhai na mali.”

Enyi Waislamu: Ni Idd al-Adha, moja ya siku zilizobarikiwa za Mwenyezi Mungu. Basi muombeni Mwenyezi Mungu (swt) aziongoze nyoyo za kundi la waumini walio na nguvu na azma, ambao wataunusuru Ummah na kusimamisha Dini, ili kuwe na Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Na tegemeeni katika ushindi wa Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye uwezo,

[وَمَا النَّصْرُ إِلاَّ مِنْ عِندِ اللهِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ]

“Na msaada hautoki isipo kuwa kwa Mwenyezi Mungu, Aliye tukuka, Mwenye nguvu na Mwenye hikima” [Aal-i-Imran: 126]

Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, La Ilaha Illallah...

Allahu Akbar, Allahu Akbar, wa lillahi Alhamd

Mhandisi Salah Eddine Adada

Murugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizbuttahrir.today
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizbuttahrir.today

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu