Jumamosi, 21 Rajab 1447 | 2026/01/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  16 Rajab 1447 Na: H 1447 / 042
M.  Jumatatu, 05 Januari 2026

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Katika Kumbukumbu ya Miaka 105 ya Kuvunjwa kwa Khilafah... Dunia Inajitayarisha Kurudi Kwake
(Imetafsiriwa)

Mtu anaweza kufikiri, huku akiangalia yanayojiri hivi karibuni katika ngazi ya kimataifa na katika ardhi za Kiislamu, kwamba uhalisia unazidi kuwa wa giza tororo kwa Umma wa Kiislamu, na kwamba matumaini ya kuamka kwake na kuregeshwa kwa heshima yake yanafifia au kupungua. Hata hivyo, kutafakari haya yanayojiri kunaonyesha kwamba yanafichua matumaini ambayo yanajajidishwa na kuzidi kuwa makubwa, na mbinu ya kuelekea mwamko siku baada ya siku.

Licha ya ukweli kwamba kampeni za Magharibi na ukafiri dhidi ya Uislamu na Waislamu zinaendelea moja baada ya nyengine, huku wakoloni wakidhihirisha meno yao na kujipanga kama mkono mmoja dhidi ya Waislamu katika sehemu kadhaa duniani, Ummah, ingawa umenyimwa mfumo wa kisiasa na Imam anayeuongoza, ikimaanisha Dola ya Khilafah na Khalifa bado umesimama kwa mshikamano na kukabiliana na kampeni hizi kwa uthabiti na changamoto iliyoongezeka ambayo imewakosesha uwezo Wamagharibi wakoloni makafiri, kiasi kwamba kwa muda kadhaa karibu waendelee kupindua ndoto zao za kikoloni katika ardhi za Ummah.

Hakika, uthabiti huu wa Ummah umekusanya hisia miongoni mwa Magharibi nzima kwamba hauwezi kupoteza kitambulisho chake au kuyeyuka ndani ya hadhara ya Kimagharibi. Magharibi imegundua kuwa maisha ya kisekula na hali za kikoloni katika ardhi za Waislamu zinaweza kuendelea tu kupitia ukandamizaji na kulazimishwa. Kisha Ummah hivi karibuni umeasi hapa na pale na kujaribu kujiondoa katika hali hizi zisizo za kawaida. Magharibi kisha ikaimarisha mshiko wake zaidi na zaidi, hadi kufikia hatua ya kuwahamasisha vibaraka wake na zana zake kushambulia miji yake kwa mabomu na makombora, na kuachilia vikosi vya mauaji ili kuwaua watoto na wanawake wake dhaifu zaidi mbele ya wanaume wake. Kwa hivyo tumeweza kusema kwamba Magharibi kafiri mkoloni “inashambulia rai jumla ya umma” katika nchi za Waislamu.

Mkusanyiko wa uthabiti huu na uasi unaoendelea wa Ummah wa Kiislamu yamesababisha hisia ya kukata tamaa kwa jumla ndani ya Magharibi, kiasi kwamba wanafikra wake na watu mashuhuri wa vyombo vya habari wamelazimika kushiriki katika uzushi kuhusu maadili yao wenyewe na kubatilisha madai yao ya uhuru. Wamekaribia kuwatenga Waislamu, miongoni mwa watu wote, kwa kutoa wito wa kuwanyima kutoa maoni yao ya kisiasa, au hata kutekeleza waziwazi mfumo wao wa stara wa maisha wa Kiislamu.

Sauti za Wamagharibi zinazotoa wito wa kufukuzwa kwa Waislamu kutoka Magharibi nzima zimeongezeka, na kwa kutia hatiani hata upingaji wa mauaji yanayofanywa dhidi ya Waislamu katika nchi zao.

Kutokana na hisia hii ya kukata tamaa katika Magharibi kuelekea Umma wa Kiislamu kulizua hisia za shaka na wasiwasi wa ubatili wa kisiasa. Hivyo, Magharibi ilianza kutilia shaka sera za kigeni za nchi zake na kuuona uwepo katika nchi za Waislamu kama ubatili wa kisiasa ambao huleta madhara na sio manufaa yoyote. Kutoka tumboni mwa wasiwasi huu kulizaliwa wito wa kurudi ndani, kama vile “Amerika Kwanza” na “Ifanye Amerika Tukufu Tena,” pamoja na kurekebisha sheria ili taasisi za hifadhi na uhamiaji, ambazo zilikuwa na lengo la kuvutia kile kinachoitwa mtaji wa binadamu, zibadilishwe kuwa kitu kinachofanana na vikosi vya polisi vya kisiasa vinavyomtesa kila mgeni na kufunga milango dhidi ya watu.

Hii inaonyesha hisia ya kufeli kwa hadhara, ikimaanisha kwamba Magharibi haijioni tena kama chombo cha hadhara kinachoweza kuyeyusha watu ndani ya hadhara yake; badala yake, sasa inatafuta kutenganisha hadhara yake na ulimwengu wote. Yote haya yametokea kutokana na uthabiti wa Ummah wa Kiislamu katika kushikamana na hadhara na kitambulisho chake na kutaka kuregeshwa kwa mamlaka yake.

Kwa hivyo, na kama ishara tu kwamba ulimwengu mzima umekata tamaa ya kuupotoa Ummah wa Kiislamu kutoka kwa msisitizo wake wa kurudi kwenye mfumo wake kamili wa maisha wa Kiislamu, tunasema kwamba katika kumbukumbu ya miaka 105 ya kuvunjwa kwa Khilafah, dunia inajiandaa kwa kurudi kwake.

Ama kuhusu kile ambacho Ummah wenyewe lazima utambue, ni kwamba kusimamishwa kwa Khilafah leo si kitu zaidi ya uamuzi unaochukuliwa na watu wenye nguvu na ulinzi ndani yake, majeshi yake na ungetimizwa ndani ya masaa machache. Ndiyo, masaa machache. Kwa maana watoto wake wote wanatamani mipaka kati yao ifunguliwe, ardhi zao zirudi kama nyumba moja, uwezo wao wa ujana uungane chini ya bendera moja, ili waweze kukabiliana na adui yao, kuregesha matukufu yao, na kutoa rasilimali zao. Hakuna kinachowazuia kutokana na hili isipokuwa miito ya udhaifu na kutoweza, ambayo si chochote ila ni udanganyifu, uongo, na hadithi za kubuni. Jibu rahisi zaidi kwa udanganyifu huu, uongo, na hadithi za ngano ni kwamba Ummah wa Kiislamu ni jasiri, mwepesi, na una lengo moja. Unapotambua kwamba una uwezo wa kufanikisha jambo, unalitimiza kwa mpepeso wa jicho. Tumeuona ukivamia wakandamizaji madhalimu zaidi na serikali za kikatili zaidi na kuzifanya kama alama baada ya maangamizi, huku ikitangazwa kwamba utawala wao ulikuwa umesimama imara na hauwezi kutikiswa na yeyote.

Hivyo, kiza kilichofinika ardhi za Waislamu leo kinaficha nyuma yake matumaini makubwa na afueni ya karibu, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Hii ndio Sunnah ya Mwenyezi Mungu kwa viumbe wake, kama ilivyo thibitishwa na maneno Yake:

[إِن يَمْسَسْكُمْ قَرْحٌ فَقَدْ مَسَّ الْقَوْمَ قَرْحٌ مِّثْلُهُ وَتِلْكَ الأيَّامُ نُدَاوِلُهَا بَيْنَ النَّاسِ وَلِيَعْلَمَ اللّهُ الَّذِينَ آمَنُواْ وَيَتَّخِذَ مِنكُمْ شُهَدَاء وَاللّهُ لاَ يُحِبُّ الظَّالِمِينَ]

“Kama yamekupateni majaraha, basi na hao watu wengine yamewapata majaraha mfano wa haya. Na siku za namna hii tunaweletea watu kwa zamu, ili Mwenyezi Mungu awapambanue walio amini na awateuwe miongoni mwenu mashahidi. Na Mwenyezi Mungu hawapendi madhaalimu.” [Surah Aal-i Imran:140].

Kutokana na hayo, tunakumbuka kumbukumbu ya miaka 105 ya kuvunjwa kwa Khilafah sio kuomboleza hali yetu au kulilia janga letu, bali kuukumbusha Umma wa Kiislamu izza ya nyuma kwamba ni wakati wake sasa kuijadidisha, na heshima iliyopotea ambao wakati wa kuirudisha umewadia. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَنُرِيدُ أَن نَّمُنَّ عَلَى الَّذِينَ اسْتُضْعِفُوا فِي الْأَرْضِ وَنَجْعَلَهُمْ أَئِمَّةً وَنَجْعَلَهُمُ الْوَارِثِينَ]

“Na tukataka kuwafadhili walio dhoofishwa katika nchi hiyo na kuwafanya wawe waongozi na kuwafanya ni warithi.” [Surah Al-Qasas: 5].

Kwa upande wetu, katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir, tutaangazia amali ambazo hizb itaziandaa kote ulimwenguni kwa mnasaba wa kumbukumbu ya mwaka huu, tukitaraji kwamba Mwenyezi Mungu itaifanya iwe ya mwisho kurudi tena bila ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Ni ulinganizi wa wazi kwa kila mtu mwenye kusikia kwa makini huku moyo wake ukiwa wazi, kujiunga nasi ili aweze kujenga upya mujtamaa wa Kiislamu na kuurudisha kama Khilafah Rashida inayowaridhisha wakaazi wa mbinguni na wakaazi wa ardhini.

Mhandisi Salah Eddin Adadah
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizbuttahrir.today
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizbuttahrir.today

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu